Ni kutokana na viongozi wake kusema hadharani bila ya kutumia vikao vya chama
Dar es Salaam. Waziri wa zamani
katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na katika Awamu
ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, Dk Juma Ngasongwa amesema kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kinababaika katika kutekeleza majukumu yake.
Vilevile, chama hicho kimekumbwa mgawanyiko kati ya watendaji wake na Serikali na kwamba taifa lina ombwe la uongozi.
Kutokana na hali hiyo, Dk Ngasongwa ambaye pia ni
kada wa CCM amemshauri Rais Kikwete kuwa mkali katika kusimamia
watendaji wake anaowateua ndani ya chama na Serikali yake na kufuatilia
na kupima utekelezaji wa yanayokubaliwa .
Alikuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na
gazeti hili nyumbani kwake mkoani Morogoro anakoendesha maisha yake kwa
kilimo cha mpunga baada ya kustaafu.
Dk Ngasongwa alisema kuwa mgawanyiko huo kati ya
watendaji wa Serikali na CCM, umeondoa umoja siyo tu katika vyombo
hivyo, bali pia miongoni mwa wabunge wa chama hicho tawala.
Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kutokea mambo
mengi ikiwamo matukio ya mawaziri kushinikizwa kujiuzulu kama
ilivyotokea hivi karibuni na kwamba kwa Serikali ya Awamu ya Nne hali
hiyo imekuwa ikijirudia.
Na Exuper Kachenje, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment