Saturday, 28 December 2013

LIGI KUU ENGLAND MAN CITY YAITOA ARSENAL KILELENI NA MAN UNITED WAZIDI KUPANDA!

>>MABINGWA MAN UNITED WAZIDI KUPANDA!
>>HULL YAFUMUA 6-0, BAO ZOTE KIPINDI CHA PILI!

 BPL2013LOGO
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Desemba 28
West Ham 3 West Brom 3
Aston Villa 1 Swansea 1
Hull 6 Fulham 0
Man City 1 Crystal Palace 0
Norwich 0 Man United 1
2030 Cardiff v Sunderland

NORWICH 0 MAN UNITED 1
Danny Welbeck, akitokea Benchi na kuingizwa Kipindi cha Pili, aliifungia Man United Bao 1 na la ushindi huko Carrow Road na kuitungua Norwich City Bao 1-0.
Meneja wa Man United, David Moyes, leo alibadilisha Wachezaji watano toka Kikosi kilichoifunga Hull City 3-2 Juzi kwa kuwachezesha Nemanja Vidic, Michael Carrick, ambae hii ilikuwa Mechi yake ya kwanza tangu Oktoba, Ryan Giggs, Shinji Kagawa na Javier Hernandez huku Wayne Rooney akikosekana kabisa.
Huu ni ushindi wa nne mfululizo kwenye Ligi na umewapaisha hadi Nafasi ya 6 kwenye Msimamo.

Refa: Phil Dowd
MAN CITY 1 CRYSTAL PALACE 0
Edin Dzeko aliifungia Man City Bao moja na pekee walipocheza na Crystal Palace Uwanjani Etihad na kuwafanya wachukue uongozi wa Ligi wakiwa Pointi 2 mbele ya Arsenal.
Refa: Andre Marriner

ASTON VILLA 1 SWANSEA 1
Aston Villa leo wamemaliza wimbi lao la kufungwa Mechi 4 mfululizo za Ligi kwa kutoka Sare ya 1-1 na Swansea City Uwanjani Villa Park.
Villa ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Gabriel Agbonlahor la Dakika ya 7 na Swansea kusawazisha katika Dakika ya 36 kwa Bao la Roland Lamah.

Refa: Roger East

HULL 6 FULHAM 0
Hull City, wakiwa kwao KC Stadium, leo wameifumua Fulham Bao 6-0 huku Bao zote zikifungwa Kipindi cha Pili.
Bao za Hull City zilifungwa na Ahmed Elmohamady, Robert Koren, Bao 2, George Boyd, Huddlestone na Matty Fryatt.

Refa: Robert Madley
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Man City 19 33 41
2 Arsenal 18 18 39
3 Chelsea 18 15 37
4 Liverpool 18 22 36
5 Everton 18 12 34
6 Man United 19 10 34
7 Newcastle 18 6 33
8 Tottenham 18 -5 31
9 Southampton 18 7 27
10 Hull 19 -1 23
11 Swansea 19 -1 21
12 Stoke 18 -8 21
13 Aston Villa 19 -7 20
14 Norwich 19 -16 19
15 West Brom 19 -5 18
16 Cardiff 18 -15 17
17 Crystal Palace 19 -16 16
18 Fulham 19 -22 16
19 West Ham 19 -10 15
20 Sunderland 18 -17 13
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Desemba 29
1630 Everton v Southampton
1630 Newcastle v Arsenal
1900 Chelsea v Liverpool
1900 Tottenham v Stoke
Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham

0 comments: