ADAI: ‘INAWAPA NAFASI NZURI KUJITAYARISHA KWA MECHI!’
>>SUAREZ KUIVAA CHELSEA MARA YA KWANZA TANGU ‘AMNGATE’ IVANOVIC!!
Liverpool wanacheza na Chelsea Jumapili Uwanjani Stamford Bridge na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho
anaamini Ratiba ‘nyepesi’ ya Liverpool, bila ya michuano ya Ulaya,
itawasidia sana Liverpool kumudu presha ya mbio za Ubingwa kwa Msimu
huu.
Chelsea wanaingia kwenye Mechi hii
wakiwa Nafasi ya Tatu na Pointi 1 mbele ya Liverpool ambayo Juzi
ilichapwa Bao 2-1 na Man City huko Etihad na kuporomoshwa kutoka
kileleni mwa Ligi hadi Nafasi ya 4.
Ingawa Mourinho anaamini Man City ndio
wenye nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa lakini anakubali Luis Suarez ndie
anaeipa Liverpool makali yanayoifanya iwe juu Msimu huu.
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 18 | 18 | 39 |
2 | Man City | 18 | 32 | 38 |
3 | Chelsea | 18 | 15 | 37 |
4 | Liverpool | 18 | 22 | 36 |
5 | Everton | 18 | 12 | 34 |
6 | Newcastle | 18 | 6 | 33 |
7 | Man United | 18 | 9 | 31 |
8 | Tottenham | 18 | -5 | 31 |
9 | Southampton | 18 | 7 | 27 |
10 | Stoke | 18 | -8 | 21 |
Mourinho amesema: “Wanaweza kutwaa Taji
kwa vile ni wazuri, kwa vile Brendan Rodgers ni mzuri lakini pia wana
muda wa kutosha kujitayarisha kimbinu kwa vile hawamo UEFA CHAMPIONZ
LIGI na EUROPA LIGI!”
Pia Mourinho alieleza: “Wachezaji wangu
watacheza Mechi 60 Msimu huu na Liverpool Mechi 40. Hii ni tofauti
kubwa. Vipaji pamoja na ari pamoja na msaada huu, ndio unaweza kuwafaya
wawe Mabingwa!”
Mechi hii ya Chelsea na Liverpool
inamkutanisha Mourinho na Brendan Rodgers ambae alikuwa Kocha wa Timu ya
Vijana na baadae Timu ya Rizevu ya Chelsea wakati Mourinho yuko
Stamford Bridge katika Kipindi chake cha Kwanza kati ya Mwaka 2004 na
2007.
Uso kwa Uso- Chelsea v Liverpool:
-Chelsea wameshinda Mechi mbili tu kati ya 13 za Ligi walizocheza na Liverpool (Ushindi: 2, Sare: 4, Kufungwa: 7).
-Mechi 5 kati ya 7 walizoshinda Chelsea zilikuja kwenye himaya ya Jose Mourinho.
-Luis Suarez ndie aliefunga Mabao ya kusawazisha, yote Kipindi cha Pili, katika Mechi mbili za Ligi Msimu uliopita.
Macho kwenye Mechi hii yatakuwa juu ya
Luis Suarez na Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic kwani hii ni mara ya
kwanza kukutana uso kwa uso tangu Mwezi Aprili kwenye Mechi ambayo
Suarez alimng’ata Meno Ivanovic, bila Refa kuona, na baadae Suarez
kufungiwa Mechi 10 kwa kosa hilo, Kifungo ambacho kilimalizika mwanzoni
mwa Msimu huu.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Chelsea: Cech; Ivanovic, D Luiz, Terry, Cole, Ramires, Mikel; Mata, Oscar, Hazard; Torres
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Sakho, Cissokho, Henderson, Allen, Lucas, Sterling, Suarez, Coutinho
REFA: Howard Webb
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Desemba 28
1545 West Ham v West Brom
1800 Aston Villa v Swansea
1800 Hull v Fulham
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Norwich v Man United
2030 Cardiff v Sunderland
Jumapili Desemba 29
1630 Everton v Southampton
1630 Newcastle v Arsenal
1900 Chelsea v Liverpool
1900 Tottenham v Stoke
0 comments:
Post a Comment