Wednesday, 25 December 2013

KESHO LIGI KUU ENGLAND BIG MECHI MAN CITY V/S LIVERPOOL UWANJA WA ETIHAD

  JE MAN CITY INAWEZA KUMZUIA SUAREZ?

NI ‘PIGA UA’ ALHAMISI, BOKSING DEI HUKO ETIHAD!!
JUMAPILI LIVERPOOL WAPO STAMFORD BRIDGE KUIKWAA CHELSEA!
NI WAZI Msimu huu Timu za Ligi Kuu England huwa zinagwaya kwenda Etihad kupambana naLUIS_SUAREZ-JUL14Manchester City ambako katika Mechi zao 8 za Ligi wameshinda zote kwa Jumla ya Bao 35.
Miongoni mwa Mechi hizo 8, City, walio chini ya Meneja Manuel Pellegrini, imeshusha vipigo kwa Mabingwa Watetezi Man United Bao 4-1, Tottenham 5-0 na Arsenal 6-3.
Lakini, safari hii, wageni wa City ni Liverpool ambao wanaongoza Ligi katika Kipindi hiki cha Krismasi kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2008/09 na wanae Straika bora kwa sasa Luis Suarez ambae ndie Mfungaji Bora akiwa na Bao 19.

JE WAJUA?
-Liverpool wameshindwa kuwa Bingwa katika mara zote tatu za mwisho walizoongoza Ligi wakati wa Krismasi.
-Mara hizo 3 ni 1990-91 walipomaliza Nafasi ya 2, Mwaka 1996-97 walipomaliza Nafasi ya 4 na 2008/09 walipomaliza Nafasi ya 2 nyuma ya Man United.
Hata hivyo, Liverpool wakiwa Ugenini ni nyanya kidogo na katika Mechi zao 8 za Ligi za Ugenini wamefungwa Bao 13
Wachambuzi wengi walikuwa na hamu na Mechi hii kuwaona Mastraika wanaong’ara Sergio Arguero wa City na Luis Suarez wakipambana uso kwa uso lakini, kwa bahati mbaya, Aguero hatakuwepo kwa vile ni Majeruhi na badala yake City wanaweza kumchezesha Alvaro Negredo au Edin Dzeko.

USO kwa USO:
-Mechi 6 kati ya 9 zilizopita za Ligi kati ya City na Liverpool zilimalizika kwa Sare huku City wakishinda 2 na Liverpool 1 Uwanjani kwao Anfield kwa Bao 3-0.

Lakini nguzo kubwa ya Timu ya City ni Kiungo chao hatari ambacho Msimu huu kimeimarika baada kumpata Fernandinho ambae ameonyesha ushirikiano mzuri sana na Yaya Toure kiasi cha kuwaruhusu David Silva na Jesus Navas kuwa huru kutiririka na Soka lao lenye akili ambalo huzichanganya ngome nyingi na kutoa mwanya wa Goli nyingi.
Kwa kawaida kukosekana kwa Mkongwe na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, kungekuwa pigo kubwa kwa Liverpool lakini katika Mechi za hivi karibuni kutokuwepo kwake kwa sababu ya maumivu kumefungua njia kwa Liverpool kutumia Viungo Chipukizi, kina Allen, Lucas, Henderson, Coutinho na Sterling,   wanaokwenda mbio mithili ya umeme na kumlainishia umaliziaji Luis Suarez.

LIGI KUU ENGLAND:
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Liverpool 17 23 36
2 Arsenal 17 16 36
3 Man City 17 31 35
4 Chelsea 17 14 34
5 Everton 17 13 34
6 Newcastle 17 2 30
7 Tottenham 17 -5 30
8 Man United 17 8 28
9 Southampton 17 4 24
10 Stoke 17 -4 21
11 Swansea 17 0 20
12 Hull 17 -6 20
13 Aston Villa 17 -6 19
14 Norwich 17 -14 19
15 Cardiff 17 -12 17
16 West Brom 17 -5 16
17 West Ham 17 -8 14
18 Crystal Palace 17 -16 13
19 Fulham 17 -17 13
20 Sunderland 17 -18 10

RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Alhamisi Desemba 26
1545 Hull v Man United
1800 Aston Villa v Crystal Palace
1800 Cardiff v Southampton
1800 Chelsea v Swansea
1800 Everton v Sunderland
1800 Newcastle v Stoke
1800 Norwich v Fulham
1800 Tottenham v West Brom
1800 West Ham v Arsenal
2030 Man City v Liverpool
Jumamosi Desemba 28
1545 West Ham v West Brom
1800 Aston Villa v Swansea
1800 Hull v Fulham
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Norwich v Man United
2030 Cardiff v Sunderland
Jumapili Desemba 29
1630 Everton v Southampton
1630 Newcastle v Arsenal
1900 Chelsea v Liverpool
1900 Tottenham v Stoke

0 comments: