Sunday, 29 December 2013

ETO’O AIPA USHINDI CHELSEA, LIVERPOOL HOI NA ARSENAL KUVUKA MWAKA 2013 AKIWA KILELENI

LIVERPOOL KRISMASI KILELENI, MWAKA MPYA YAPOROMOKA…YA 5!!LIGI KUENDELEA JANUARI MOSI!!

SAMUEL ETO’O leo alikuwa Shujaa wa Stamford Bridge alipofunga Bao la ushindi wakati ChelseaBPL2013LOGO ilipotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuitwanga Liverpool Bao 2-1 wakati huko White Hart Lane Tottenham waliicharaza Stoke City Bao 3-0.

MATOKEO:
Jumapili Desemba 29
Everton 2 Southampton 1
Newcastle 0 Arsenal 1
Chelsea 2 Liverpool 1
Tottenham 3 Stoke 0

CHELSEA 2 LIVERPOOL 1
ETOO_IN_CHELSEALiverpool walitangulia kufunga katika Dakika ya Tatu tu baada ya Frikiki ya Coutinho kuunganishwa wavuni na Martin Skrtel lakini Dakika 14 baadae Shuti la Eden Hazard lilifanya Chelsea iwe Sare 1-1.
Gwiji la Cameroun, Samuel Eto’o, ndie aliefunga Bao la Pili na la ushindi baada ya kazi njema ya Oscar kwenye Winga ya Kulia.
Kipindi cha Pili, Mamadou Sakho alipiga posti kwa kichwa na Liverpool watarudi kwao wakijuta ‘kunyimwa’ Penati mbili kufuatia kuvaana na John Terry na Eto'o.
MAGOLI:
Chelsea 2
-Hazard Dakika ya 17
-Eto'o 34
Liverpool 1
-Skrtel Dakika ya 3
Ushindi huu umeifanya Chelsea ijizatiti Nafasi ya Tatu na kupunguza pengo lao na Vinara Arsenal kuwa Pointi 2 tu wakati kipigo hiki kwa Liverpool ni cha pili mfululizo na kuzidi kuwaporomosha kwani Siku ya Krismasi wao ndio walikuwa Vinara wa Ligi na sasa wanaingia Mwaka Mpya wakiwa Nafasi ya 5 huku nyuma yao wakiwa ni Mabingwa Manchester United walio Pointi 2 tu nyuma.
 RSENAL: MARA YA KWANZA TOKA 2007/08 KILELENI MWAKA MPYA!
EVERTON YAINGIA 4 BORA!!


NEWCASTLE 0 ARSENAL 1
GIROUDBao la Kichwa la Olivier Giroud katika Dakika ya 65 leo limeifanya Arsenal iifunge Newcastle huko St James Park Bao 1-0 na kutwaa tena uongozi wa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 mbele ya Manchester City.
Ingawa Arsenal walifungua nafasi kadhaa za kufunga lakini ni Newcastle waliokosa Bao za wazi wakati Shuti la Moussa Sissoko lilipookolewa na Kichwa cha Mathieu Debuchy kupiga posti.
Goli hilo la Arsenal lilipatikana baada ya Frikiki ya Theo Walcott kuunganishwa na Giroud.
Ushindi huu umewafanya Arsenal wawe kileleni mwa Ligi Kuu England Siku ya Mwaka mpya kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2007/08.


EVERTON 2 SOUTHAMPTON 1
Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea, Romelu Lukaku, leo Uwanjani Goodison Park ameifungia Bao la Pili na la ushindi Everton walipoichapa Southampton Bao 2-1.
Hilo lilikuwa Bao la Kwanza kwa Lukaku katika Mechi 6.
Everton walitangulia kupata Bao Mfungaji akiwa Fulbeki Seamus Coleman na Southampton kusawazisha kwa Bao la Gaston Ramirez alietokea Benchi.

MAGOLI:
Everton 2
-Coleman Dakika ya 9
-Lukaku 74
Southampton 1
 
TOTTENHAM 3 STOKE CITY 0
Tottenham wameichara Stoke City Bao 3-0 Uwanjani White Hart Lane na kujisogeza karibu ya Timu Nne za juu sasa wakikamata Nafasi ya 7 wakiwa Pointi sawa na Man United walio Nafasi ya 6 na wako nyuma ya Timu ya 4 Everton kwa Pointi 3 tu huku Liverpool ikishika Nafasi ya 5 wakiwa Pointi mbili mbele yao.
Tottenham walipata Bao la Kwanza kwa Penati ya Roberto Soldado ambayo ilitolewa baada ya Shuti la Emmanuel Adebyor kushikwa na Beki Ryan Shawcross.
Bao nyingine mbili zilifungwa na Mousa Dembele na Aaron Lennon.

MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Arsenal 19 19 42
2 Man City 19 33 41
3 Chelsea 19 16 40
4 Everton 19 13 37
5 Liverpool 19 21 36
6 Man United 19 10 34
7 Tottenham 19 -2 34
8 Newcastle 19 5 33
9 Southampton 19 6 27
10 Hull 19 -1 23
11 Swansea 19 -1 21
12 Stoke 19 -11 21
13 Aston Villa 19 -7 20
14 Norwich 19 -16 19
15 West Brom 19 -5 18
16 Cardiff 19 -15 18
17 Crystal Palace 19 -16 16
18 Fulham 19 -22 16
19 West Ham 19 -10 15
20 Sunderland 19 -17 14
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham

0 comments: