Saturday, 28 December 2013

SUNDERLAND MAMBO MAGUMU WATOA SARE NA CARDIFF CITY 2-2!

 LEO NI CHELSEA v LIVERPOOL, NEWCASTLE v ARSENAL!
JANA USIKU, Timu ya mkiani Sunderland, iliambua Sare ya Ugenini baada ya kutanguliwa Bao 2-0BPL2013LOGO na kufunga Bao 2 katika Dakika 7 za mwisho, Bao la pili likiwa katika Dakika ya Mwisho ya Dakika za Majeruhi, na kutoka 2-2 na Cardiff City ambayo ilikuwa ikicheza Mechi yao ya Kwanza tangu imtimue Meneja wao Malky Mackay.

MATOKEO:
Jumamosi Desemba 28
West Ham 3 West Brom 3
Aston Villa 1 Swansea 1
Hull 6 Fulham 0
Man City 1 Crystal Palace 0
Norwich 0 Man United 1
Cardiff 2 Sunderland 2

Wenyeji Cardiff City walitawala Mechi hii na Shuti la Jordon Mutch lilimbabatiza Modibo Diakite na kuandika Bao la Kwanza kisha Fraizer Campbell akawafungia Bao la Pili na kuongoza 2-0.
Lakini kwenye Dakika ya 83, Steven Fletcher, alietoka Benchi, aliipa Sunderland Bao la Kwanza na katika Dakika ya Mwisho ya Dakika za Majeruhi baada Dakika 90 kwisha, Shuti la Jack Colback lilimbabatiza Sentahafu Steven Caulker na kufanya Mechi imalizike 2-2.

MAGOLI:
Cardiff 2
-Mutch Dakika ya 6
-Campbell 58
Sunderland 2
-Fletcher Dakika ya 83
-Colback 90

Sare hii imewafanya Cardiff wawe Pointi 2 Juu ya Timu 3 za mkiani ambalo ndio eneo hatari la kushushwa Daraja na wapo Pointi 4 mbele ya Sunderland ambao wamebaki
 
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Man City 19 33 41
2 Arsenal 18 18 39
3 Chelsea 18 15 37
4 Liverpool 18 22 36
5 Everton 18 12 34
6 Man United 19 10 34
7 Newcastle 18 6 33
8 Tottenham 18 -5 31
9 Southampton 18 7 27
10 Hull 19 -1 23
11 Swansea 19 -1 21
12 Stoke 18 -8 21
13 Aston Villa 19 -7 20
14 Norwich 19 -16 19
15 West Brom 19 -5 18
16 Cardiff 10 -15 18
17 Crystal Palace 19 -16 16
18 Fulham 19 -22 16
19 West Ham 19 -10 15
20 Sunderland 19 -17 14

0 comments: