Saturday, 7 December 2013

SIMANZI KUBWA ZATAWALA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI DAR

Raia wa Afrika Kusini akiomboleza ubalozini Dar es Salaam.

Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar es Salaam, jana ulijaa simanzi na huzuni wakati Balozi wa nchi hiyo Thunduyise Chiliza, akitangaza kifo cha rais mstaafu Nelson Mandela na kutoa salama zake za rambirambi.

Wakati balozi huyo akizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya raia wa Afrika Kusini akiwamo Cidi Stando walikuwa wakilia muda wote kufuatia kifo cha Mandela.


Stando alisema alikuwa Dar es Salaam kusalimia wanae na alipata taarifa za kifo hicho na kuwa na huzuni kwa kuwa Mandela alikuwa ngome ya maisha yake.


Balozi Chiliza alisema Mandela atakumbukwa kwa vita ya ukombozi na harakati za kuleta na kuendeleza utamaduni wa kudumisha amani nchini Afrika Kusini.


Aliwafahamisha waandishi kuwa licha ya kifo cha Mandela kutarajiwa watu wameupokea msiba wake kwa hisia tofauti na kwamba hadi anafariki alikuwa amelala nyumbani kwake kwenye chumba cha kihospitali kilichoandaliwa kwa ajili ya uangalizi maalumu wa kimatibabu. 
SOURCE: NIPASHE
7th December 2013

0 comments: