Monday, 9 December 2013

WALIMU 3 NA MFANYABIASHARA WAHUKUMIWA MIAKA 517 JELA KWA KUHUJUMU SHULE

 

WALIMU watatu na mfanyabiashara mmoja wamehukumiwa kifungo cha miaka 517 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa 68 ya ubadhirifu wa fedha za shule ya msingi Tukoma iliyokuwa katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda sasa halmashauri ya Mlele kiasi cha shilingi Mil 21 kutoka katika kifungu cha Capitation katika mkoa wa Katavi wilaya ya Mlele

Waliohukumiwa kifungo hicho wametajwa kuwa ni walimu watatu Mwalimu Katabi, Mwalimu Mwakyusa na Mwalimu Ngairo wote wa shule ya msingi Tukoma waliokuwa wakituhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za shule hiyo zilizotolewa na 
serikali kwa ajili ya maendeleo ya shule hiyo

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa wilaya ya Mpanda mkoani hapa Chiganga Tengwa alisema Mwalimu Katabi anahukumiwa kutumikia jela jumla ya miaka 157, mwalimu Mwakyusa alihukumiwa kutumikia jela miaka 275 na mwalimu Ngairo alihukumiwa kutumikia jela miaka 200 baada ya kupatikana na hatia kwenye makosa 68 ambapo mwananchi mfanyabiashara wa Mpanda mdugu Mlenje alihukumiwa kifungo cha miaka 33 jela baada ya kupatikana na makosa ya kushirikiana na walimu hao kuihujumu shule ya msingi Tukoma ambapo hukumu hiyo ilitolewa wiki hii Desemba 5,2013

Baadhi ya wananchi mjini Mpanda wameshangazwa kwa hukumu hiyo ambayo inadaiwa kuwa ni ya kihistoria katika mahakama ya wilaya hiyo tangu mahakama hiyo kuanza kazi mjini hapa. ---- via blogu ya HabariKatavi

0 comments: