MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday 24 July 2016

Vikongwe wawili wauawa kwa tuhuma za uchawi

Picha na makitaba

Vikongwe wawili mke na mumewe wa Kitongoji cha Nyag’holongo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wameuawa kwa kutumia silaha za jadi na watu wasiojulikana wakituhumiwa kuwa ni wachawi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Isack Msengi alisema tukio hilo lilitokea Julai 22 saa tatu usiku nyumbani kwao.

Aliwataja wanandoa hao kuwa ni Machene Magina (80) na Mkewe Genke Bundara (75) ambao waliuawa na wananchi wakiwatuhumu kwa uchawi.

Msengi alisema watu watano wanashikiliwa na polisi na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea. Diwani wa Kata ya Nanda, Jumamosi Mathias alisema kundi la watu ambalo halijulikani lilivamia nyumbani kwa familia hiyo wakati wakijiandaa kulala na kufanya ukatili huo.

Mathias alisema akiwa nyumbani kwake, alisikia kelele za watu wakisema; “Tumechoshwa na hawa wachawi. Kwa kuwa hawa wazee ni majirani zangu, nilianza kuhangaika ili kuona jinsi ya kudhibiti maafa hayo,” alisema Mathias.

 Hata hivyo, alisema kabla ya kutoa taarifa polisi, watu hao waliivamia nyumba hiyo na kufanya mauaji hayo ya kinyama kwa vikongwe hao.

Alilaani kitendo kilichofanywa na watu hao kuwa ni cha kikatili dhidi ya wazee kwani tangu aishi nao kijijini hapo hakuwahi kusikia tuhuma za uchawi dhidi yao.

Mathias alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuwahisi wazee kuwa ni wachawi na kujichukulia sheria mkononi, badala yake wawathamini na kuwalinda kwani wazee ni hazina ya Taifa.

Askofu Gwajima amjibu,Yusuf Makamba aliyemuita muongo

 


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na maguta. 

Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, mimi nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia. 

Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni muongo na kuwa uongo wake unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho. 

Alisema Gwajima amekuwa akisema uongo kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete hataki kuachia madaraka ya uenyekiti wa chama hicho, kitu ambacho Rais huyo mstaafu alikanusha akisema ni yeye alikwenda kumshawishi Dk John Magufuli kuchukua nafasi hiyo kabla ya muda wa uliopangwa kikatiba. 

Katika mahubiri hayo, Gwajima pia alisema mafunzo aliyoyapata tangu akiwa mdogo ni kuogopa kugombana na watu wa aina tatu, walevi, wazee na wagonjwa. 

“Baba yangu alinifundisha nisigombane na walevi, wazee na wagonjwa kwani ukimpiga kidogo mtu wa aina hiyo anaweza kufa,” alisema Gwajima. 

“Hata nyie waumini wangu nawaomba msigombane na watu wa aina hiyo kwani mnaweza kupata matatizo,” alisema. 

Kiongozi huyo aliongoza mamia ya waumini wake kumuombea Rais Magufuli kwa kushinda uenyekiti wa CCM akisema kofia hizo mbili zimempa meno ya kung’ata na zitamwongezea kasi ya kutatua matatizo ya wanyonge nchini.

Rais Magufuli juzi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata kura zote 2,398 alizopigiwa na wajumbe wa mkutano huo. 

Kutokana na ushindi huo, Gwajima alisema Magufuli amepewa meno ya `kung’ata’ kila upande tofauti na alipokuwa na kofia moja ya urais. 

Alisema kwa muda mfupi aliokaa madarakani, elimu ya msingi na sekondari zimeanza kutolewa bure kitendo ambacho maskini na wanyonge wa nchi hii wameanza kuuona mwanga. 

Alisema ataendelea kumwombea Magufuli kwa sababu kazi anazozifanya zinawanufaisha wanyonge na maskini ambao kwa muda mrefu walipuuzwa katika nchi yao.

“Kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti ni zawadi kwetu Watanzania, tuendelee kumwombea kila siku ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi,” alisema. 

Alisema nafasi hiyo mpya itamwezesha kupambana na rushwa tatizo ambalo ameonyesha kuwa `atalivalia njuga’ hata ndani ya chama hicho. 

Mbali na Rais Magufuli, Gwajima aliwaombea pia Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri na Spika wa Bunge kwamba Mungu awalinde ili wamsaidie Rais kutekeleza majukumu yake. 

Kwa mwezi mzima, Askofu Gwajima amekuwa akitafutwa na Polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais mstaafu Kikwete afikishwe mahakamani kwa makosa yote yaliyofanyika katika utawala wake. 

Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Magufuli asipewe uenyekiti ambao umekuwa ukishikiliwa na Kikwete. 

Baada ya sauti hiyo, Gwajima aliondoka nchini kwenda Japan lakini Polisi waliendelea kumsaka hadi Julai 12 walipomkamata katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), aliporejea. Alihojiwa na kuachiwa siku hiyohiyo.

Diwani Akwepa Risasi sita akipambana na majambazi Moshi


Diwani wa Kata ya Kiborlon (Chadema) katika Manispaa ya Moshi, Frank Kagoma ameonyesha ujasiri wa hali ya juu alipopambana na majambazi waliokuwa na silaha za moto.

 Alinusurika kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na bastola kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata hivyo, hazikumpata. 

Tukio hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya majambazi hao kuvamia duka la jumla la kuuza mitumba linalomilikiwa na Menti Mbowe na kupora Sh10 milioni. 

Katika tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la Kiborlon, majambazi hao walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia mabasi ya Machame Safaris. 

Hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri. Akisimulia tukio hilo, diwani huyo alisema siku hiyo akiwa maeneo ya Kiborlon, alipigiwa simu kuwa mfanyabiashara huyo amevamiwa na majambazi ndipo alipoendesha gari lake hadi eneo la tukio. 

“Nilipofika pale wale majambazi watatu ndiyo walikuwa wanatoka kwenye duka. Nikampelekea gari yule aliyekuwa ameshika bunduki. Kuona hivyo akafyatua risasi hewani,” alisema Kagoma. 

“Yule mwenye bunduki akaingia uchochoroni kuelekea Barabara ya Stendi ya Kidia. Mwenzake aliyekuwa na bastola naye akawasha risasi nyingine hewani kunitisha,” alisema. 

Baada ya hali hiyo, diwani huyo alilazimika  kujificha kwenye gari na majambazi hao walidandia pikipiki na kuanza kukimbia kuelekea Barabara ya Msaranga, naye akawafuata kuelekea huko. 

“Wakati huo tayari vijana wangu wa bodaboda wakawa nao wamesikia hilo tukio tukaanza kusaidiana kuwafukuza lakini mbele kidogo pale Msaranga wale majambazi wakasimamisha pikipiki yao umbali wa mita 30 kutoka nilipokuwa na mmoja wao mwenye bunduki alifyatua risasi mbili na mwenye bastola risasi mbili kuelekea uelekeo wangu. 

“Nililazimika kujificha kwenye kiti, wale majambazi wakajua wameniua. Wakapanda tena pikipiki ili watoroke. Nikawasha tena gari huku vijana wangu nao wakinisaidia tukaanza kuwafukuza,” alisema. 

Kagoma alisema majambazi hao walipita maeneo ambayo gari haliwezi kupita wakaelekea eneo la Mabogini Moshi Vijijini hadi lango la TPC na baadaye wakaelekea Rundugai wilayani Hai. 

“Kuna eneo vijana wangu wanasema kulikuwa na vumbi sana, ndipo walipowapoteza na majambazi wakatoroka kupitia njia ya reli ili kukwepa polisi waliokuwa wakiwasubiri mbele,” alisema na kuongeza:“Hatukuwa na silaha, lakini tulijitahidi kupambana nao kwa ujasiri. Tatizo nafikiri tulikosea kidogo. Ilitakiwa wakati tukifukuzana nao tuwape polisi uelekeo wa majambazi.” 

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa Jeshi lake litatoa taarifa rasmi kwa wanahabari leo kuhusiana na msako unaoendeshwa na jeshi hilo. 

“Kuna mambo tumeyafanya tangu tukio hilo litokee lakini kesho (leo) saa sita mchana tutatoa taarifa rasmi pamoja na mafanikio tuliyofikia hadi sasa. Tunaendelea vizuri na upelelezi,” alisema.

Kamanda Mutafungwa, alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwamo kuwafichua wahalifu na mbinu wanazozitua akisema polisi wamejipanga kukabili wimbi jipya la ujambazi.

Mtandao wa haki za binadamu walia na Jeshi la Polisi




Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umelitaka Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuwafikisha mahakamani wanachama wake wanne linaowashikilia kwa siku 12 sasa. 

Mtandao huo umedai kuwa watu saba wilayani Longido wanatuhumiwa kutoa taarifa kwa mwanahabari wa Sweden, Susana Nurduland ambaye anafuatilia kwa karibu migogoro ya ardhi wilayani humo. 

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa alisema uendeshaji wa madai hayo umegubikwa na upendeleo wa wazi jambo lililo kinyume na matakwa ya sheria za nchi kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai. 

“Hadi sasa watetezi wanne wamenyimwa dhamana wakati wengine wenye nafasi za kisiasa wamepewa. Hii si sawa,” alisema Olengurumwa. 

Aliwataja walionyimwa dhamana kuwa ni Samwel Nangiria, Supuk Olemaoi, Clinton Kairung na Yohana Mako wakati walioachiwa ni mbunge wa zamani wa Ngorongoro, Mathew ole Timan, Diwani wa Ololosokwani, Yanick Ndina Timan na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mundoros, Joshua Makko. 

Alieleza kuwa watetezi hao wamenyang’anywa vitendea kazi vyao pamoja na vifaa vya mawasiliano zikiwamo simu za mkononi na kompyuta mpakato. 

Wakili wa Kujitegemea wa kampuni ya Law Guards Advocates, Jebra Kambole alisema hiyo ni kinyume na sheria zinazosimamia haki za binadamu nchini. 

“Kumshikilia mtu muda mrefu bila dhamana pamoja na kunyimwa uwakilishi ni kinyume na Katiba ya nchi. Ni kinyume na Azimio la Umoja wa Mataifa la Watetezi wa Haki za Binadamu la mwaka 1998,” alisema Kambole baada ya kueleza kuwa watuhumiwa hao wamenyimwa haki ya kuwatumia mawakili. 

Licha ya ombi hilo kwa Polisi, mwanachama wa mtandao huo, Rose Sarwatt alimuomba Jaji Mkuu kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisha haki inatendekea. 

Aliziomba asasi za kimataifa kukemea na kuishauri Serikali juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea huko Loliondo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jeshi lake linasimamia na kutekeleza sheria za nchi na halichagui wa kumkamata kama amefanya kosa la jinai.

 “Lazima ukamatwe labda uwe na kinga. Hata mimi, japo kazi yangu ni kukamata lakini nikifanya jinai nitakamwa tu,” alisema na kubainisha kuwa taratibu zinaendelea kuzingatiwa na zikimalizika, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.

Kapombe afuata nyayo za Messi, Aguero

Category: 
Team: 
Azam FC
U
NAWEZA ukashangazwa lakini huu ndio utambulisho mpya wa beki wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, ambaye ameamua kuja na staili mpya ya kufuga ndevu zake kuelekea msimu ujao.
Kapombe amewashangaza watu wengi kufuatia staili yake hiyo, aliyoanza kuonekana nayo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, tokea alipoanza mazoezi mepesi ya gym Jumanne iliyopita.
Beki huyo ameanza mazoezi baada ya kupona ugonjwa wa Pulmonary Embolism (donge la damu kuziba mishipa ya damu katika mapafu), uliokuwa ukimsumbua na kumfanya akae nje ya dimba kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz kuhusu staili yake hiyo mpya, Kapombe amesema staili hiyo ndio itakayomtambulisha msimu ujao na kudai kuwa hawezi kuzinyoa ndevu hizo mpaka pale atakapofunga ndoa na mchumba’ke aliyekuwa naye sasa.
“Mchumba’ngu ndio kaniambia nifanye hivi, ameniambia napendeza sana nikiwa na ndevu hizi, nasikiliza ushauri wake na nitazinyoa tutakapofunga ndoa hivi karibuni,” alisema.
Kapombe, 23, aliyecheza jumla ya dakika 3188 msimu uliopita, amefuata nyayo za wachezaji mahiri duniani kutoka Argentina, Mchezaji Bora wa Dunia, Lionel Messi na staa wa Manchester City, Sergio Aguero waliowahi kufuga ndevu zao lakini wao wakikamia ubingwa wa Copa America mwaka huu.
Wawili hao waliweka kiapo cha kutonyoa ndevu hizo wakati wakiiongoza Argentina kwenye michuano ya Kombe la Copa America wiki chache zilizopita wakiamini kuwa ni uchawi utakaowapa taji la michuano hiyo na kuondoa mkosi wa kukosa mataji, lakini walishindwa kwa kufungwa na Chile kwa mikwaju ya penalti 4-2 kwenye mchezo wa fainali.

Martial kuchukizwa kwa namba yake ya jezi kupewa Ibrahimovic

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambaye kajiunga na Man United msimu huu akitokea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kama mchezaji huru, jina lake linazidi kuingia kwenye headlines baada ya kuchukua jezi namba 9 iliyokuwa inavaliwa na Anthony Martial.
Stori kutoka 101greatgoals.com zinaeleza kuwa Zlatan baada ya kuwasili, viongozi waMan United walimwambia achague namba ya jezi ambayo angependa kuvaa, Zlatanakachagua namba 9 na viongozi wakakubali pasipo kumuhusisha kwa namna yoyote ileAnthony Martial ambaye alikuwa akiivaa jezi hiyo.
Screen-Shot-2016-04-23-at-21.16.57
Headlines za Martial kuvuliwa jezi namba 9 na kupewa Zlatan Ibrahimovic bila ridhaa zinapata nguvu kutokana na Anthony Martial kuripotiwa kuunfollow account za Man United za Instagram na twitter, kwa sasa mashabiki wa Man United wanatajwa kuwa na hofu na Martial kuendelea kusalia kikosini kwa muda mrefu.
Screen-Shot-2016-07-24-at-12.07.55-AM
Screen-Shot-2016-07-24-at-12.07.25-AM (1)
Screen-Shot-2016-07-24-at-12.07.25-AM

Lulu Michael Afunguka Kuhusu Chama Anachokifagilia Bongo....



Alipoulizwa yeye shabiki wa chama gani cha siasa?, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijibu hivii; "Mimi sina chama, ndiyo maana hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, sijaonekana kwenye jukwaa lolote. Miye naamini kura ni siri na nilifanya hivyo ili nisifungamane na upande wowote." Alifanya vizuri au alichemka

Kauli ya CHADEMA baada ya wanachama wake kutangaza kujiunga CCM

Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.

"Kamati Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema mjumbe huyo.

Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana jana na leo katika vikao vya dharura ikiwa na lengo kubwa la kujadili mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Saturday 23 July 2016

Bei ya jezi za nyumbani za Man United watakazovaa 2016/2017



Baada ya Man United kutambulisha jezi zao za ugenini zenye rangi ya blue watakazotumia katika msimu wa 2016/2017, leo Jumamosi ya July 23 Man Unitedwametambulisha rasmi tena jezi zao mpya watakazotumia katika mechi za nyumbani.
36866C9B00000578-3704477-image-a-17_1469261720740
Jezi za nyumbani za Man United huwa na rangi nyekundu utofauti huwa ni muundo tu,Man United kwa sasa jezi zao zitakuwa na rangi nyekundu iliyokolea upande mmoja na upande pili rangi nyekundu iliyopooza, kama utakuwa unahitaji jezi ya Man United ya mikono mifupi bila jina na namba ni pound 60 ambazo ni zaidi ya Tsh 170000.
368644E900000578-3704477-image-a-4_1469263315673
Kwa upande wa mashabiki watakaopenda kuvaa jezi za nyumbani za Man United za mikono mirefu watalazimika kulipa pound 65 ambazo ni zaidi ya Tsh 180,000, bukta pound 30 ambazo ni zaidi ya Tsh 80,000, soksi pound 13 ambazo ni zaidi ya Tsh 35,000, kwa watakaopenda kuvaa full itakuwa pound 103 ambazo ni zaidi ya Tsh 290,000.
36866C9300000578-3704477-image-a-19_1469261753952
3686438100000578-3704477-image-a-6_1469263374448
36866C9700000578-3704477-image-a-21_1469261792568

Alichokiandika Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kupewa uenyekiti wa CCM


Leo July 23 2016  Rais John Pombe Magufuli amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM   baada ya kupigiwa kura za ndio 2398  kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika
Baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…
>>>’Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda
Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.’ –Zitto Kabwe
Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.‘ –Zitto Kabwe
Screen Shot 2016-07-23 at 7.08.01 PM

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufunguliwa Kwa Mfumo Wa Udahili Wa Pamoja (CAS) Unaoratibiwa Na NACTE

Na Kutangazwa Kwa Majina Ya Waombaji Udahili Waliochaguliwa Kujiunga Na Kozi Za Cheti Na Diploma

Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni  tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.



Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.



Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina  ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. 

Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). 

Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa. Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.  



Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.



Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 22 Julai, 2016

DEAL DONE: Pogba Avunja Rekodi ya Uhamisho wa Dunia


WAZUNGU wanasema kwa Kiingereza chao, Deal done. Yaani biashara imekwishamalizika. Watu wananyanyuka katika viti vyao, wanapeana mikono, wanakumbatiana, wanaondoka. Uhamisho wa Paul Pogba inasemekana umemalizika.

Manchester United imefanikiwa kumnasa kiungo huyo mahiri wa Juventus kwa dau la Pauni 100 milioni ambalo litaweka rekodi mpya ya uhamisho duniani na kulipiku dau la Pauni 85 milioni ambalo Real Madrid walilipa mwaka 2013 kumchukua Gareth Bale kutoka Tottenham.

Licha ya kulipa dau hilo, United watamlipa Pogba mshahara wa pauni 210,000 kwa wiki kwa mkataba wa miaka mitano ikiwa ni miaka minne tangu alipomruhusu kuondoka bure kwenda Juventus Julai 2012 akiwa mchezaji kinda.

Bosi wa Man United, Ed Woodward alikacha kwenda katika ziara ya United nchini China na alikutana na Wakurugenzi wa Juventus, Giuseppe Marotta na Fabio Paratici, pamoja na wakala wa Pogba, Mino Raiola kwa ajili ya kumaliza dili hilo.

Juventus iling’ang’ania dau hilo licha ya Man United kujaribu kushusha, lakini mwishowe Man United imekubali kulipa dau hilo kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye amezaliwa nchini Ufaransa na wazazi wake waliotokea Guinea barani Afrika.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho alikuwa anamtaka staa huyo kabla ya pambano la ngao la hisani kati yao na Leicester City Agosti 7 na atajiunga nao mara baada ya timu hiyo kurejea katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini China ambako wametua juzi.

Pogba aliondoka Old Trafford katika utawala wa kocha mkongwe, Sir Alex Ferguson baada kushindwa kuhakikishiwa nafasi katika kikosi cha kwanza kilichokuwa kimesheheni mastaa wakongwe kama Paul Scholes ambaye Ferguson hakutaka kumuweka benchi na alimuamini zaidi.

Tangu hapo, Pogba ameibuka kuwa mmoja kati ya viungo bora barani Ulaya huku akiiwezesha Juventus kutwaa ubingwa wa Serie A mara nne, akiifikisha pia katika fainali za Ulaya pamoja na kuipeleka Ufaransa katika fainali za Euro 2016 ambapo walichapwa 1-0 na Ureno.

Mfaransa huyo atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Man United dhini ya Mourinho baada ya kuwanasa Eric Bailly kutoka Villarreal, Zlatan Ibrahimovic aliyenaswa bure kutoka PSG na Henrikh Mhkitaryan aliyechukuliwa kutoka Borussia Dortmund.

Wakati dau la Pogba likianza kulalamikiwa na wadau wengi wa soka kwamba haliendani na kiwango chake, tayari nyota huyo ameanza kupata watetezi akiwemo staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry.

“Sahau kuhusu Ufaransa, nadhani anaweza kuwa mmoja kati ya viungo bora katika historia. Ana ubora wa kufanya hivyo. Anahitaji kuwa makini tu na kitu anachoweza kukifanya vizuri.” Alisema Henry katika michuano ya Euro.

Friday 22 July 2016

Vigogo wote Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Watumbuliwa MAJIPU

 

SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi.

Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi.

Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi.

Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo.

Waziri Maghembe alisema Mohamed Kilongo aliyesimamishwa kazi Januari 5, mwaka huu uchunguzi umeonekana hana hatia na hivyo anaendelea kuwa Mkurugenzi Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu.

Alisema Wizara imeamua Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Gladnes Mkamba ahamishiwe Idara ya Mipango makao makuu na nafasi hiyo kuteuliwa Dk Ezekiel Mwakalukwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi.

Aidha Monica Kagya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, anakuwa Mtafiti Mwandamizi Idara ya Nyuki (Tawiri). Alisema Kagya ni mtaalamu wa masuala ya nyuki, hivyo atahamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, ili ashughulikie utafiti wa masuala ya nyuki.

Pia alisema katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa anakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Herman Kerayo ambaye anahamishiwa Idara ya Mipango Makao Makuu.

Profesa Ramadhan Kideghesho, yeye anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Mweka wakati Mabula Misungwi aliyekuwa Meneja Mradi Selous, anakwenda Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na nafasi yake inachukuliwa na Jaffary Lyimo, huku Robert Mande akipelekwa kuwa Kaimu Mkurugenzi msaidizi Uzuiaji Ujangili.

Waziri Maghembe alisema Majjid Ally ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Haji Mpya ambaye amehamishiwa Shamba Jipya Songea kuwa Ofisa Misitu Alisema Julai 18, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikutana na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo na watendaji wakuu na watumishi wa TFS na kuagiza kufumuliwa na kusukwa upya kwa wakala huo.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alitaka kuondolewa kwa utitiri wa vituo vya ukaguzi na kuwekwa vituo vichache na kuondolewa kwa ofisi za makontena yanayotumiwa na ofisi ya TFS, badala yake watumishi wanaofanya ukaguzi wasimame mahali pa wazi ili kuondoa mianya ya rushwa na kuweka uwazi katika utendaji.