MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday 11 January 2015

EPL: SOTON WAVUNJA REKODI YA MIAKA 27 DHIDI YA MANCHESTER UNITED


Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena jioni ya leo kwa michezo miwili kucheza katika viwanja tofauti nchini humo – moja ya mechi ilikuwa inawakutanisha timu zinazogombania kuendelea kuwemo kwenye 4 bora – Man United vs Southampton.
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford umeshuhudia rekodi ya miaka 27 ya Soton kutokuifunga Man United katika uwanja wa nyumbani kwenye EPL ikivunjika.
Goli la dakika ya 69 la Tadic limewapa Southampton ushindi ambao pia umewapandisha mpaka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.
Katika mchezo mwingine wa leo hii Arsenal waliifunga Stoke City 3-0 na kupanda hadi nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi.

SERIKALI YATOA SHILLINGI MILLIONI 21 MIKOPO KWA AJIRI YA VIJANA

Serikali imewataka vijana kuitumia vyema mikopo wanayopata katika kuteketeza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa  Ufutiliaji na Tathimini  toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi.Verdiana Mushi wakati alipotembelea Ofisi ya Halmashauri ya Nzega na kwa ajili ya kukabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 21 itakayosaidia kukopesha vikundi vya vijana walioko chini ya Vijana Saccoss Nzega.
“Serikali inaendelea kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwa kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itawaongezea kipato na kuwaondolea umasikini kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya nchi” Alisema Bi.Mushi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nzega Bw. Abrahaman Mndeme ameishukuru serikali kwa kuwapatia mkopo huo vijana wa Nzega kwani kwa kupitia mkopo huo vijana watafaidika sana na pia watachangia kukua kwa pato la Halmashauri na kupunguza vijana wanaoka vijiweni na kushauriana mambo yasiyo na maendeleo katika jamii.
PIX 2
Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Nzega Bw. Abrahaman Mndeme akipokea  barua pamoja na hundi zenye jumla kiasi cha shilingi millioni 21 kutoka kwa  Afisa Vijana wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni  na Michezo hivi karibuni.
“Uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Saccoss ya Vijana Nzega utasimamia gawio la fedha hizo kwa vikundi husika na kuhakikisha miradi iliyoandikwa na vikundi hivyo inatekelezwa, pamoja na kufuatilia urejeshwaji mikopo hiyo kwa wakati ili vikundi vingine viendelee kunufaika na mikopo hiyo inayotolewa na serikali”,alisema Bw.Mndeme
Akitoa hamasa kwa vijana Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Eliakim Mtawa aliwaasa Vijana kuunda vikundi na kujiunga katika Saccoss za Vijana zilizopo katika halmashauri zao ili waweze kuomba mkopo  utakao wasaidia kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi badala ya kukaa vijiweni.
PIX 3
Afisa Vijana wa Halmashauri ya Nzega Bi.Frida Lwani (watatu  kulia) akifafanua jambo kuhusu maendeleo ya vikundi vya vijana vya  hapo kwa Maafisa kutoka Wizara ya habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo walipowatembelea katika ofisi ya halmashauri ya Nzega hivi karibuni.
“Serikali imedhamiria kwa dhati kuwakomboa vijana kiuchumi kwa kutambua changamoto ya ajira iliyopo katika taifa letu  kwa sasa na dunia nzima kwa ujumla”,alisema Bw.Mtawa.
Pamoja na hayo naye Mwenyekiti wa Vijana Saccoss Nzega Bw.Emmanuel Mambo, ameishukuru serikali kwa niaba ya vijana wa Nzega kupitia Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuwapatia fedha hizo walizoomba kwa ajili ya kufanya miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji na kilimo itakayoongeza kipato chao.
 

MTUKURU waua mtoto wa mwaka mmoja Singida

DSC03164
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
POLISI mkoani Singida inamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma ya kusababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja na mama mtoto kulazwa baada ya kunywa pombe ya ‘Mtukuru’ nyumbani kwa  mtuhumiwa.
Kamanda wa polisi mkoa, Thobias Sedoyeka alimtaja mwanamke anayeshikiliwa kuwa ni Anastazia Kadama (35) mkazi wa kijiji cha Msule, Misughaa wilayani Ikungi mkoani Singida.
Alisema kuwa tukio hilo ni la Jan 07 mwaka huu majira ya saa 3.15 asubuhi kijijini hapo.
Alisema kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa Anastazia aliandaa pombe ya kienyeji iitwayo ‘Mtukuru’ kwa ajili ya kuwaalika majirani kwenda kumsaidia kulima shamba lake lakini kwa bahati mbaya siku hiyo mvua kubwa ilinyesha kiasi cha kuzuia shughuli hiyo kufanyika.
Kutokana na kuhofu pombe hiyo kuharibika, mtuhumiwa inadaiwa kuwa aliamua kuigawa kwa watu ili wainywe bure; mmoja wa watu hao akiwa mama wa mtoto aliyekufa, Magdalena Muna.
Alisema kuwa baada ya Magdalena kuionja pombe hiyo alimpa mtoto wake wa mwaka mmoja, Josephat Ntui, naye akanywa.
Kamanda Kamwela alisema kuwa baada ya Magdalena na mtoto wake kunywa pombe hiyo, walianza kutapika na kuharisha jambo lililosababisha wakimbizwe hospitali ya misheni Makiungu kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa mtoto huyo alizidiwa njiani kisha akafariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini lakini mama yake alifika akiwa hai na bado anaendelea na matibabu.
Kufuatia tukio hilo, Kamanda Kamwela amewataka wakazi wa mkoa huu kuwashirikisha wataalamu wa afya katika shughuli zao mbalimbali  za kuchinja, kuandaa chakula au pombe za kienyeji ili kuepukana na matatizo yasiyo ya lazima.

TRA MKOA WA SINGIDA, YATOA MSAADA WA MADAWATI WILAYA YA MKALAMA

DSC03256
Meneja TRA mkoa wa Singida, Samson Jumbe (kushoto) akimkabidhi Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Isanzu wilaya ya Mkalama, Sadick Mbiro Abdallah, msaada wa madawati 25 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili. Katikati mwenye miwani ni Afisa elimu kwa umma (TRA),Zakaria.
(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Mkalama
Meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) Tanzania mkoani Singida, Samsoni Jumbe,amewahimiza  viongozi/watendaji na watu wenye uwezo kiuchumi kujenga utamaduni  wa kushiriki ukarabati  majengo na miundombinu mingine ya shule/vyuo walikosomea, ili iendelee kuvutia kama ilivyokuwa wakati wa enzi zao.
Jumbe ametoa wito wakati akizungumza na uongozi wa shule ya msingi ya Isanzu Wilaya ya Mkalama, muda mfupi kabla hajakabidhi  madawati 25 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili.
Alisema uzoefu unaonyesha shule nyingi  pamoja na vyuo mbalimbali vilizojengwa miaka  mingi, vingi zimechakaa vibaya na majengo yake mengi hayafai kutumiwa na wanafunzi  na walimu.
Aidha, Jumbe alisema kuwa majengo na miundombinu mingine ya aina hiyo inafika mahali haivutii tena na yanakuwa ni hatari kwa usalama wa wanafunzi na walimu hao.
DSC03252
Meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Singida, Samson Jumbe akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Isanzu iliyojengwa na Wajerumani mwaka 1934.Wanafunzi hao wamekalia madawati 25 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili yaliyotolewa msaada na TRA mkoa wa Singida.
“Shule za Msingi walikopita viongozi wa ngazi  mbalimbali wakiwemo wa kitaifa na wabunge,  na wafanya biashara  wa ngazi mbalimbali, zimejengwa miaka mingi kama hii ya Isanzu iliyojengwa na Wajerumani mwaka 1934. Ni lazima zichakae kwa hiyo zinahitaji ukarabati  mkubwa ambao gharama zake kwa kawaida ni kubwa”,alifafanua meneja huyo.
Jumbe alisema viongozi waliosomea katika shule/vyuo hivyo hawana budi kushirikiana kwa karibu na uongozi wa shule /vyuo kutafuta fedha ikiwemo kwa kuandaa harambee kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya ukarabati wa majengo na miundombinu mingine na ununuzi wa madawati.
Awali mwalimu mkuu wa shule hiyo Sadick Mbiro Abdallah, alisema shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya  600, inahitaji madawati 204 yaliyopo ni 110 mapungufu ni dawati 94.
DSC03262
Moja ya madarasa yaliyojengwa mwaka 1934 na Wajerumani ya shule ya msingi Isanzu wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida.Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Iramba mashariki Mgana Msindai na David Holela aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ushirika wamesoma katika shule hiyo.Kwa sasa darasa hilo bado linaendelea kutumika.
Katika hatua nyingine mwalimu Abdallah alisema shule hiyo ambayo imetoa wasomi wengi wakiwa ni akina Mgana Msindai  Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Singida na  David Holela aliyewahi kuwa Naibu waziri wa ushirika, inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mwamko duni wa elimu kwa  wazazi/walezi wengi wa wanafunzi wa shule hiyo.
Akifafanua, alisema wazazi/walezi wengi wa wanafunnzi wa shule hiyo wamekuwa wakiwatisha watoto wao na kuwaagiza wahakikishe hawafaulu hasa mtihani wa Taifa wa Kumaliza elimu ya Msingi.
“Mwanafunzi anaweza kuwa na uwezo mzuri darasani kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Lakini utashangaa matokeo  ya mtihani wa Taifa na darasa wa darasa la saba   kwani, atafanya vibaya mno”,alifafanua.na kuongeza; “Hali hii inachangiwa na wazazi/walezi kuwaonya watoto wao kwamba wakifaulu kwenda sekondari watajisomesha wao wenyewe.
Kwa mujibu wa Mwalimu Abdallah mwaka juzi wanafunzi 15 kati ya 66 walifaulu mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi mwaka jana wanafunzi 10 kati ya 66 walifaulu mtihani wa Taifa wa Darasa la saba.

NAIBU WAZIRI WA MAJI AZINDUA MIRADI YA MAJI MIWILI KATIKA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.

NA 







Naibu waziri wa maji na Mbunge wa jimbo la mvomero Mh, Amos Makala amezindua miradi ya maji miwili ilioko katika wilaya ya Mbeya, mmoja umejengwa katika kata ya tembela kijiji cha galijembe na mmoja umejengwa katika kata ya Igale na Shongo.

Aidha Makala ameahidi kupeleka shilingi milioni mia moja tisini na tano katika kata ya Iwindi wilaya ya Mbeya vijijini ikiwa fedha hizo anatarajia kutok  serikalini.

Friday 9 January 2015

Stars maboresho kuivaa Rwanda

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).
Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.
Kocha Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kitakusanyika Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na siku moja baadaye kwenda jijini Mwanza.

Bangi yamtia jela mwanawe Jackie Chan

Jackie chan na mwanawe Jacee Chan
Jacee Chan mwana wa mwana nyota wa filamu Jackie Chan amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kutumia mihadarati.
Chana mwenye umri wa miaka 32 alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya wiliaya ya mjini Beijing Dongcheng kwa kuwaficha wengine ili kutumia dawa za kulevya.
Polisi walivamisa nyumba yake mnamo mwezi Agosti na kupata gramu 100 za marijuana.
Alikabiliwa na hukumu ya miaka mitatu.
Kukamatwa kwake kunajiri kufuatia msako wa dawa za kulevya nchini Uchina ambapo watu kadhaa mashuhuri walikamatwa.
Jacee Chan na babaake jackie Chan
Mnamo mwezi Juni mwaka 2014,rais Xi Jinping aliwaagiza polisi kutumia mikakati mikali ili kusitisha utumizi wa mihadarati.
Kukiri kwa mwana wa mcheza filamu mashuhuri nchini Uchina kunatoa ujumbe muhimu kutoka kwa serikali ya Uchina.
Hakuna aliye na kinga nchini Uchina katika msako huo wa dawa za kulevya.
Chan na nyota wa filamu kutoka Taiwan Kai Ko mwenye umri wa miaka 23 walikamatwa pamoja katika nyumba ya Beijing mnamo mwezi Agosti huku polisi wakisema kuwa walipatikana wametumia bangi.

Washukiwa wa mauaji Ufaransa wauawa

Vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kwamba washukiwa wawili waliohusika na mauaji ya Charlie Hebdo wameuawa.
Wawili hao walisakwa kwa siku mbili na polisi baada ya kutoroka baada ya kuwaua wandishi habari wa jarida la Charlie Heblo.
Maafisa wa usalama walivamia eneo ambako vijana hao walikuwa wamejificha wakiwa na mateka mmoja na kuwaua vijana hao ambao walikuwa ndugu.
Milio ya risasi ilisikika huku moshi mkubwa ukionekana kufuka kutoka katika jengo hilo huku makomando wakionekana wakivamia jengo hilo.
Duru zinasema washukiwa hao walikuwa wamejihami walifyatulia risasi makomando hao kabla ya kuuawa.
Walisema waliwaua wandishi wa habari kama hatia ya kulipiza kisasi hatua ya wahariri wa jarida hilo kuchora vibonzo kumkejeli mtume Mohammed wa dini ya kiisilamu.
Iliarifiwa walikipora kituo cha mafuta wakiwa mbioni huku wakiwateka mateka na kwenda nao katika kiwanda ambako walikuwa wamejificha.
Mateka mmoja aliweza kuokolewa.
Kwingineko milipuko na milio ya risasi ilisikika ndani ya duka la jumla la kiyahudi, Kaskazini mwa mji huku watu watano waliokuwa wametekwa nyara na mshambuliaji mmoja wakiuawa.
Baada ya operesheni ya polisi kukamilika baadhi ya matyeka wlaiokuwa wamezuiliwa ndani ya duka hilo walionekena wakitoka nje.

WillY m -- Hope u need me( official video)