MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Monday 30 June 2014

KOMBE LA DUNIA: UFARANSA YAITUPA NJE NIGERIA, YAICHAPA 2-0

 DAKIKA ZA LALA SALAMA


Mabao ya Pogba dakika ya 79 na Yobo la kujifunga dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo, yaimepeleka Ufaransa Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Nigeria 2-0usiku huu    nchini Brazil.

haya ndiyo madhara ya kutazama televisheni



Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari ya kuaga dunia mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache.
Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani.
“Utazamaji sana wa wa runinga ni tabia ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna ongezeko la mienendo ya kila aina ya tabia za kukaa tu,” mtafiti mkuu Miguel Martinez-Gonzalez, profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko Pamplona, nchini Uhispania, alisema katika taarifa ya shirika hilo.
“Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo.”
Watafiti hao waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda wa kutumia tarakilishi na muda wa kuendesha gari.
'Sababu nyinginezo'
Vijana hao walioshiriki, ambao walikuwa na umri wa wastani wa miaka 37 na ambao asilimia 67 walikuwa wanawake, walifuatiliwa kwa takriban miaka 8.2. mwishowe, vifo 97 viliripotiwa, vikiwemo vifo 19 vilivyotokana na mishipa na moyo, 46 kutokana na saratani na mengine 32 vilivyotokana na sababu nyinginezo.
Utafiti huo ulionyesha hatari kubwa ya kuaga dunia ilikuwa mara mbili zaidi kwa washiriki walioripoti kutazama runinga kwa saa tatu au zaidi kwa siku ikilinganishwa na wale waliotazama kwa saa moja au chini ya saa.
Watu 19 waliripotiwa kufariki kutokana na kutizama TV kwa muda mrefu
Hatari hii mara mbili zaidi ilidhihirishwa pia baada ya kutoa hesabu ya safu kubwa ya vigezo vingine vinavyohusiana na hatari kubwa ya kuaga dunia.
Watafiti hao hawakupata ushirikiano kati ya muda unaotumiwa na mtu anapotumia tarakilishi au kuendesha gari na hatari kubwa ya kuaga dunia mapema kutokana na sababu zote.
Pia waliongezea kuwa utafiti zaidi unapaswa kufanywa ili kudhibitisha ni athari zipi zilizopo kati ya kutumia tarakilishi na kuendesha gari katika viwango vya vifo, na pia kutathmini taratibu za kibayolojia zinazoweza kueleza uhusiano huo.
“Watu wanapoendelea kuzeeka, tabia za kukaa tu zitaenea zaidi, hasa kutazama runinga, na hili litasababisha mzigo mkubwa katika ongezeko la matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuzeeka,” Martinez-Gonzalez alisema.
“Matokeo ya utafiti wetu yanapendekeza watu wazima wajihusishe katika mazoezi ya viungo, waache kukaa tu kwa muda mrefu, na wapunguze kutazama televisheni kwa zaidi ya saa mbili kila siku.”

KUMBE :Wachezaji 7 wa Costa Rica hawakutumia dawa zaa kulevya



Wachezaji 7 wa Costa Rica hawakutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini
Wachezaji saba wa Costa Rica waliolazimishwa na maafisa wa FIFA kupimwa mkojo punde baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya Italia wamedhibitishwa kuwa hakutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Maafisa wa Afya na wale wa kuchunguzi utumiaji wa madawa ya kututumua misuli yaliyopigwa marufuku walliwavamia wachezaji punde baada ya ushindi huo mkubwa na kuwatenga hadi pale walipochukua mkojo kwa ajili ya kupima chembe chembe za damu .
Tukio hilo lilikuwa la kustaajabisha kwani timu hiyo ilikuwa baadhi ya timu zilizokuwa zimeshukiwa kutokana na mchezo wao mzuri.
Wachezaji 7 wa Costa Rica hawakutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini
Awali wachezaji kadha walilazimika kupimwa punde baada ya mechi ambayo Costa Rica iliizaba Uruguay mabao 3-1.
Mfumo huu wa kupima mkojo wa wachezaji punde baada ya mechi imeiwacha FIFA ikishtumiwa kwa kupendelea timu fulani kushamiri katika kombe la dunia huku timu ambazo hazikutarajiwa kunawiri zikishurutishwa kupimwa dawa za kututumua misuli zilizopigwa marufuku.
Aliyekuwa mchezaji wa wa Argentina Diego Maradona aliiunga shirikisho la soka la Costa Rica kuikashifu FIFA akisema mbinu hiyo mpya inalenga kuwazonga wachezaji na mawazo kabla ya kipute hicho kumalizika nchini Brazil.

ANGALIA :ROONEY AAMUA KULA ZAKE 'MIBATA' NCHINI MAREKANI


Baada ya timu ya england kuwatolewa katka  kombe dunia rooney amuakula bata nchini marekani asema ngoja apumzike










Polisi 2 wauawa karibu na Ikulu ya Misri


 
Maafisa wawili wa polisi waliuawa wakitegua mabomu yaliyokuwa yametegwa karibu na ikulu ya rais

Mabomu mawili yamelipuka karibu na Ikulu ya Rais mjini Cairo, nchini Misri na kuwaua maafisa wawili wa polisi.
Bomu la kwanza lilimuua afisa wa polisi na kuwajeruhi wengine watatu.
Bomu la pili lililipuka maafisa wa polisi walipokuwa wanajaribu kulitegua na kumuua polisi mwingine.
Wapiganaji wa kiisilamu wanadaiwa kutega mabomu hayo katika eneo hilo wiki jana.
Shambulizi hili limetokea katika siku ya maadhimisho ya maandamano ambayo yalisababisha jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Muhammad Morsi.
Mkuu wa ulinzi wa mjini Cairo ameambia BBC kuwa mkuu wa idara ya kutegua mabomu Generali, Alaa Abdel Zaher, alikuwa miongoni mwa wale waliojeruhiwa.
Wakati huo huo, naibu mkuu wa ulinzi amesema kuwa wataalamu wa kutegua mabomu walitegua mabomu mengine mawili yaliyopatikana nje ya ikulu ya Rais.
Abdul Fattah al-Sisi.

Hata hivyo ratiba ya Rais Abdul Fattah al-Sisi haikubadilishwa kutokana na mashambulizi hayo.
Mashambulizi ya mara kwa mara yamesababisha vifo vya mamia ya watu wakiwemo maafisa wa usalama tangu Morsi kuondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Wapiganaji wa kiisilamu wameongeza mashambulizi katika kujibu operesheni ya kijeshi dhidi ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, ambapo zaidi ya watu 1,400 wameuawa na wengine 16,000 kujeruhiwa.

Hivyo ndivyo Rais wa Uruguay alivyotukana maafisa wa FIFA

Rais Jose Mujica amesema maafisa wa FIFA wamuadhibu Suarez kwa unyonge wake
Rais wa Uruguay Jose Mujica amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa'' au "a bunch of old sons of bitches".
Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumpiga marufuku mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.
Mchezaji huyo aliitaja adhabu hiyo ya marufuku ya miezi minne ikiwemo kutocheza mechi 19 za kimataifa kama adhabu ya kinazi.
Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika hoistoria ya kombe la dunia kwa kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.
Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneo yake pamoja na ukali wa matamshi yake.
Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kubanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika awamu ya muondoano.
Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema , lakini wandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi.Pia aliwaambia kuyachapisha matamshi yake alipohojiwa ikiwa alitaka kujirekebisha.
Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.
Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historia ya FIFA.

NHIF YATETA NA WADAU WAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akifungua mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Malimu Nyerere Conference Centre jijini Dar es salaam kuzingumzia mambo mbalimbali kuhusu huduma hiyo ya bima ya afya, wadau waliohudhuria katika mkutano huo n kutoka wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni mkoani Dar es salaam, Lengo kuu likiwa kuhamasisha na wananchi kujiunga na mfuko huo na kufikia asilimia 30% ifikapo mwaka 2015, Pia kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa malengo hayo na kuzitatua.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2 
Baahi ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo 7 8 9 
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndungulile akiwa katika mkutano huo. 10 
Anjela Mziray (kushoto) Meneja masoko kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akisoma taarifa za mkutano huo ulipokuwa ukiendelea.  11 

HOT NEWS :MWANAFUNZI WA RUCO ALIYECHOMWA MOTO AFARIKI.

                                          R.I.P DANIEL LEMA: 

 R.I.P Daniel Lema
Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde, mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha RUCO kilichopo mkoani Iringa Daniel Lema aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoani Iringa baada ya kuchomwa moto amefariki dunia.

Lema aliyekuwa mwanafunzi wa kitivo cha sheria, wiki iliyopita akiwa katika maeneo ya Kihesa manispaa ya iringa alishambuliwa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto akidhaniwa kuwa ni mwizi.

Kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda ni kwamba Lema alikuwa akitoka kutizama mpira/michuano ya kombe la dunia akiwa amelewa pombe majira ya saa 5 usiku katika harakati za kutafuta chakula katika migahawa ghafla mlinzi wa nyumba ya kulala wageni iliyokuwa jirani(Masai) alimhisi ni mwizi kisha kupiga kelele za kuomba msaada akidai kuwa alikuwa mwizi.

Kikundi cha watu wachache kilijitokeza na kuanza kumshambulia kwa kumpiga kisha kumwagia mafuta na kumuwasha moto wakati wakiwa katika harakati za kumpeleka polisi kisha baadhi ya wasamalia wema wakajitokeza na kuuzima moto.

Marehemu alikimbizwa katika hospitali ya mkoa ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu wiki iliyopita lakini haikuwa riziki Mungu kampenda zaidi mapema mchana wa leo ameaga dunia.

Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Lema itafanyika kesho asubuhi majira ya saa moja kamili katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya iringa kisha kuanza safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayo fanyika siku ya juma tano.

Mpaka sasa mlinzi wa gest (Mmasai) aliyemsababishia kifo kijana huyo anashikiliwa na polisi mkoani iringa.

Kwa taarifa zaidi endelea kuisikiliza Ebony fm radio kutoka katika chumba cha habari ili kupata muendelezo wa ratiba ya mazishi.
 
Lema wakati akipatiwa matibabu katika hospitali kuu ya mkoa

Daniel Lema wa kwanza kutoka kushoto akiwa na wanafunzi wenzake enzi za uhai wake.

LOUIS VAN GAAL KUMBADILI RVP KWENYE MECHI, NI SALAMU SPESHO MAN UNITED!


LVG-RVPWACHAMBUZI huko Uingereza wametafsiri kuwa kumbadili Nahodha wa Netherlands Robin van Persie wakati Holland iko nyuma kwa Bao 1-0 walipocheza na Mexico ni ujumbe tosha toka kwa Louis van Gaal kwa Klabu yake mpya Manchester United kuwa hatakuwa na masihara akianza rasmi kibarua chake.
Akizungumzia kumtoa Robin van Persie, ambae ni Nahodha na ndie Mfungaji wao mkuu, huku wakiwa nyuma kwa Bao 1-0 na Dakika zikiwa zimebaki 10, Louis van Gaal, ambae ndie Kocha wa Holland, ameeleza: “Kumbadili ni kubadili mbinu. Tusisahau yeye alijiunga na Timu akitokea kwenye Majeruhi. Ni ngumu kwake kucheza Dakika 90 katika hali ya Joto kama lile.”
Wakati akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Klaas Jan Huntelaar ambae ndie aliefunga Bao la ushindi kwa Penati ya Dakika ya 94, Van Persie alioonyesha alikuwa mchovu ikiwa ni wazi Joto lilimmaliza.
Hata Meneja wa Mexico, Miguel Herrera, alikiri Joto liliathiri uchezaji kwa kusema: “Hatukuona Mechi nzuri. Hata Timu nzuri kama Netherlands inaathirika kwa Joto -hamna kasi, uchezaji hupungua!”
Alipomwingiza Klaas Jan Huntelaar, Louis van Gaal ilibidi abadilishe Mfumo kwa mara ya 3 kwenye Mechi hiyo kwani alianzia 5-3-2 kwenda 4-3-3 na zikibaki Dakika 10 huku wakiwa nyuma 1-0, alitumia 4-4-2 na kuwatumia Klaas Jan Huntelaar na Dirk Kuyt kama Mastraika wawili mbele.
Van Gaal ameeleza: “Tulikuwa na Mapumziko ya kujipoza, kunywa Maji na hapo niliweza kuanza na Mpango B na kuwaambia wote. Tumefanyia mazoezi kuwatumia Huntelaar na Kuyt kama Mastraika na kutumia Mipira mirefu. Baada ya kusawazisha nilimrudisha Kuyt kucheza Fulbeki na tukatumia 4-3-3 kwa mara nyingine. Hapo ndipo tukawa tunampata Robben mara nyingi na ndio maana akalazimisha Penati.”
Wachambuzi wanadai ni wazi maamuzi kama hayo yategemewe na Wachezaji wa Man United Msimu ujao.
Mifumo itabadilika, uchezaji utabadilika kufuatana na Mechi yenyewe na hakuna Mtu atakayepona kubadilishwa hata kama Staa namna gani.
Akijibu swali kwa nini alimbadila Van Persie, Van Gaal alisisitiza: “Kocha huyu anataka ushindi. Ndio maana amefanya mabadiliko. Hamna ugumu zaidi ya hilo.”

YANGA YASHANGAA NGASSA KWENDA BONDENI! SOUTH AFRIKA

 
KATIBU MKUU wa Yanga, Beno Njovu, ameripotiwa kushangazwa na taarifa kuwa Straika wao Mrisho Ngassa alikwenda Afrika Kusini kwa Majaribio na Klabu ya Free State Stars FC.
Njovu alisema kuwa walichokuwa wanajua wao ni kuwa Free State Stars FC walionyesha nia ya kumtaka Straika huyo mahiri na wakapewa masharti ya kumnunua.
Miongoni mwa hayo ni kutaka Klabu hiyo ya Afrika Kusini isubiri hadi Ngassa atakaporudi Nchini, akitokea Botswana alikotakiwa kuwepo kwenye Kambi ya Taifa Stars kama wao Yanga walivyofikiria ndiko yuko, ili wazungumze nae kuona kama ataikubali Klabu hiyo ili waendelee na majadiliano ya Uhamisho.
Njovu alitoboa kuwa hapo Juni 20 waliwaambia Free State Stars FC kuwa thamani ya Ngassa ni Dola 150,000.
Njovu alieleleza: “Tulichokuwa tunajua ni kuwa Ngassa yuko na Timu ya Taifa huko Botswana na hatujui lolote kwenda huko Afrika Kusini kufanya Majaribio na kufuzu upimwaji afya!”
‘WAPINZANI’ YANGA WAINGIA MITINI KUJIANDIKISHA!
MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Baraka Kizuguto, amesema Zoezi la Kuandikisha Wanachama wao wanaopinga Mwenyekiti Yusuf Manji kuongezewa Mwaka mmoja kwenye uongozi na ndipo ufanyike Uchaguzi Mkuu limefungwa.
Kizuguto alisema Zoezi hizo limefungwa baada ya Siku 5 zilizotolewa kufanywa Uandikishwaji kumalizika bila ya ‘Wapinzani’ hao kujitokeza.
Mwenyekiti Manji alipitishwa na Wanachama 1522 kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika hivi karibuni kuendelea kukaa madarakani kwa Mwaka mmoja zaidi na kisha ufanyike Uchaguzi Mkuu lakini baadae kukaibuka Kikundi kilichopinga hilo.
Ndipo Manji akaamua ‘Wapinzani’ hao wajiandikishe na ikiwa watafika idadi ya 1522 basi yeye ataitisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.
Kizuguto amesema suala hilo sasa limefungwa na wao wanaelekeza nguvu zao kwenye Usajili wa Wachezaji pamoja na maandalizi ya Msimu mpya wa Ligi unaoanza Agosti 24.

ANGALIA: AVEVA ALIVYO SHINDA KWA KISHINDO KTK UCHAGUZI SIMBA SC

  

 10
HATIMAE Klabu ya Simba imepata Uongozi mpya baada kufanya Uchaguzi Mkuu hapo Jana huko Bwalo la Maafisa wa Polisi, Oyster Bay, Jijini Dar es Salaam.
Evans Aveva ndie aliibuka Mshindi kwa uchaguzi wa Rais kwa kumtupa Andrew Tupa kwa kuzoa Kura za kishindo 1452 dhidi ya 387 za Tupa.
Ushindi huo wa Aveva ulitangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damas Ndumbaro, ambae pia alimtaja Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kuwa Mshindi wa cheo cha Makamu wa Rais baada kuwabwaga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Swedi Nkwabi na Bundala Kabulwa.
Uchaguzi huo ulihudhuriwa na Wanachama wa Simba zaidi ya 2,000 na ulisimamiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Dar es Salaam [DRFA], Amin Bakhresa, huku Mbunge wa Ilala, Mussa Azan ‘Zungu’ akiwa Meza Kuu pamoja na aliekuwa Rais wa Simba, Ismail Aden Rage, Mbunge wa Tabora Mjini toka CCM.
Awali, Michael Wambura, mmoja wa Wagombea wa Urais wa Simba alieleta ‘tafrani’ ya kusababisha vuta nikuvute kati yake, Simba na TFF na hatimae kuzuiwa kushiriki, alifika hapo Bwalo la Polisi lakini akazuiwa kuingia baada kuambiwa Jina lake halipo miongoni mwa Wanachama wa Simba lakini inasemekana baadae aliruhusiwa kuingia Ukumbini.
Uchaguzi huo pia ulichagua Wajumbe Watano wa Kamati Kuu ya Simba na Majina yao tutaleta baadae.

ANGALIA PICHA JINSI WANACHAMA WA SIMBA WALIVYOPIGA KURA LEO KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA

Wanachama wa Simba wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Klabu ya Simba katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande)
Wagombea wa nafasi ya Urais katika Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) na Andrew Tupa na wakipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Hassan Dalali akipiga kura.
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage wakipiga kura.
 Rais wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage akiagana na mgombea wa Urais wa Simba, Evans Aveva (katikati).
 Wagombea wakitafakari.
 Wanachama wakihakiki kadi zao.
Mgombea wa Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akizungumza na baadhi ya wanachama kabla ya uchaguzi.
Mgombea akiomba kura......Tukiwezeshwa tunaweza.
 Mgombea akijinadi.
 Mgombea wa nafasi ya Kamati ya Utendaji wa Simba, Asha Muhaji akijinadi mbele ya wapiga kura.
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiwa Rais aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
 Ibrahim Masoud Maesto akijinadi.
 Mbunge wa Mtwara, Mohamed Murji, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
 Tunaomba kura zenu..............
 Nitaleta Maendeleo mkinichagua mimi..........................
 Simba Oyeeeeeee......................
 Jamhuri Kihwelo akielekea kujinadi kwa wanachama wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Simba.
 Jamhuri Kihwelo 'Julio' akiomba kura.
 Wagombea wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Andrew Tupa, Evans Aveva.
 Wagombea wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Andrew Tupa (kupara), Swed Nkwabi,  Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Evans Aveva.
 Jamhuri Kihwelo 'Julio'akimwaga sera zake.
  Jamhuri Kihwelo 'Julio'akimwaga sera zake.
  Jamhuri Kihwelo 'Julio'
 Kaburu akijinadi kwa wapiga kura.
Jamhuri Kihwelo 'Julio' akiteta na Evans Aveva.
 Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba, Amin Bakhressa.
 Evans Aveva akijadiliana jambo na Hans Pope.

 Mgombea wa nafasi ya Urais, Andrew Tupa akijinadi.
 Mgombea wa nafasi ya Urais, Evans Aveva akijinadi.
 Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba, Amin Bakhressa akionesha fomu za uchaguzi.
 Mmeona hakuna kitu humu....
 Asha Muhaji akipiga kura.

KABURU ' NDIYE MAKAMU WA RAIS SIMBA SC

Geoffrey Nyange 'Kaburu' ameshinda Umakamu wa Rais Simba SC baada ya kupata kura 1043 akimshinda mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo ni taarifa za awali, matokeo kamili yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi baadaye.