MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Wednesday 30 April 2014

KOCHA WA SIMBA LOGARUSIC ATAKA WACHEZAJI 25 TU SIMBA



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, ameutaka uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi kusajili wachezaji 25 tu msimu ujao wa ligi kuu ambapo amependekeza kuwa na makipa watatu.

Loga amekabidhi ripoti yake hivi karibuni kabla ya kwenda nchini kwao Croatia kwenye mapumziko huku akisubiri majibu iwapo ataitwa kuendelea na timu hiyo au la ambapo mkataba wake unaisha Juni, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema ripoti hiyo ya kocha aliyoiwakilisha imependekeza kusajili wachezaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukabidhi majina ya wachezaji wanaotakiwa na wasiotakiwa kubaki msimu ujao ambapo idadi kamili anayoitaka ni wachezaji 25.
“Loga amependekeza wachezaji kadhaa wabaki ambao anaona wanafaa kuwatumia kwa ajili ya msimu ujao ambapo amesema anataka wachezaji 25 tu katika timu nzima na iwapo idadi itaongezeka basi itakuwa ni ya viongozi.
“Anahitaji kila nafasi iwe na wachezaji wawili huku kwa upande wa makipa amependekeza waongezwe wawili ili kuwa na jumla ya makipa watatu pamoja na Ivo Mapunda.
“Kuna nafasi mbalimbali ambazo ametaka zisajiliwe, hivyo tutaangalia mahitaji yake iwapo nafasi hizo kuna wachezaji wa Tanzania watakaofaa au kuangalia nje ya nchi kwa kuwa kuna namba nyingine ni lazima tuzipate nje.

“Pia kuna baadhi ya  wachezaji ambao amewapendekeza wasajiliwe kutoka katika timu mbalimbali za ligi kuu, lakini siwezi kuwataja kwa kuwa ni mapema mno,” alisema Kamwaga.

PAUL NONGA ASEMA YANGA SIMBA, NO! ATAKA KUBAKI MBEYA CITY


NONGA (WA KWANZA KULIA)AKIWA NA KIKOSI CHA MBEYA CITY.

Mshabuliaji wa Mbeya City, Paul Nonga, amezikataa timu za Simba na Yanga kwa kusema kuwa hafikirii kuondoka katika timu hiyo.


Nonga ameonyesha kiwango cha hali ya juu akiwa na timu hiyo ya mkoani Mbeya ambayo imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu na amesema anataka kuendelea kukaa kwenye timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Nonga alifunguka kuwa, hafikirii kuondoka Mbeya City kwa kuwa mtazamo wake ni kuhakikisha anaisaidia timu hiyo ili iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu ujao.
“Kwa kweli sifikirii kuondoka Mbeya City  kwani ndiyo timu iliyoniibua na nitabaki hapahapa kwani ushindani tulioutoa kwenye ligi iliyoisha unatokana na mshikamano tuliokuwa tukiuonyesha.

“Tunavyoishi katika kambi ya Mbeya City ni kama ndugu. Hakuna tatizo lolote kwani tumezoea mazingira hayo ikiwa ni pamoja na uongozi kutupa ushirikiano wa kutosha.
“Unadhani wote tukijazana Simba na Yanga nani ataijenga Mbeya City?  Kwani inaweza kubomoka msimu ujao iwapo wachezaji wengi wataondoka na kuifanya timu ishuke kiwango, lengo letu ni kutwaa ubingwa msimu ujao tukiwa na Mbeya City.

“Kiujumla ligi ilikuwa ngumu kwa kuwa kila timu tuliyokuwa tukikutana nayo ilikuwa inatukamia na kutufanya tupoteze rekodi yetu ya mzunguko wa kwanza ya kutofungwa, tulifanya makosa na wenzetu wakayatumia, katika mzunguko wa kwanza walikuwa hawatujui,” alisema Nonga.
SOURCE: CHAMPIONI

AL AHLY YAPANGWA KUNDI LA ‘KIFO’ KOMBE LA SHRIKISHOB


VIGOGO wa Misri, Al Ahly wamepangwa katika Kundi B la Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2014 pamoja na Sewe Sport ya Ivory Coast, Etoile du Sahel ya Tunisia na Nkana FC ya Zambia.
Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wababe wa Cameroon, Coton Sport wametupwa Kundi A pamoja na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, AS Real ya Mali na AC Leopards ya Kongo Brazzaville.
Kundi la kifo; Al Ahly imepangwa kundi gumu Kombe la Shirikisho Afrika 


Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na Juni 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22-24 na washindi wawili wa kila kundi watasonga Nusu Fainali.MAKUNDI KOMBE LA SSHIRIKISHO:
KUNDI A: AC Leopards, ASEC Mimosas, AS Real Bamako na Coton Sport
KUNDI B: Al Ahly, Etoile du Sahel, Sewe San Pedro na Nkana FC

MAYWEATHER AONYESHA JEURI YA FEDHA, ATAKA KUNUNUA TIMU MAREKANI

KAMA anavyotamba katika ngumi za kulipwa hadi sasa akiwa hajapoteza pambano licha ya kupigana na mabondia wakali duniani, Floyd Mayweather anataka kununua klabu ya mpira wa kikapu Marekani, inayomilikiwa na milionea anayekabiliwa na kashfa ya ubaguzi.
Hakuna ajabu kwa mkali huyo wa kutupa mikono kwenye miili ya wenzake, anayekwenda kwa jina la utani Money Mayweather juu ya hilo, kwa sababu ana uwezo kifedha.
Floyd Jnr anataka kutoa dola za Kimarekani Milioni 40 ambazo ni sehemu tu ya pato lake la pambano la Jumamosi wiki hii, atakalolipwa dola bilioni 1.8 ili kuinunua  Los Angeles Clippers.

Mutu ya fweza: Floyd Mayweather akiwasili ukumbi wa MGM Grand kuelekea pambano lake na Marcos Maidana
Kuhusu Marcos Maidana, Muargentina anayetarajiwa kupambana naye mjini Las Vegas, Mayweather amesema: "Amekuwa babu kubwa katika mapambano yake manne yaliyopita. Ana wastani wa asilimia 80 ya Knockout (KO). Hivyo siwezi kumdharau huyu jamaa,".
Kuhusu Clippers, ambayo mmiliki wake Donald Sterling amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya mpira wa kikapu baada ya kupatikana na hatia ya kuwatolea maneno ya kibaguzi watu weusi wa timu yake wakiwemo wachezaji, Mayweather amesema: "Ninataka kuinunua Clippers? Ndiyo. Naweza kuwaunganisha pamoja watu ambao watakuwa tayari.
"Kununua timu ya Ligi Kuu ya kikapu ni kitu fulani ambacho nataka kuongeza katika kampuni yetu inayokua kwa kasi ya Mayweather Promotions, ambayo sasa si kwa ajili ya ngumi tu, bali tunajihusisha pia na mavazi, muziki na sinema,"alisema.
Banned for life: Los Angeles Clippers owner Donald Sterling cannot be involved in the team's operations after racist comments allegedly made by him were made public
Kifungo cha maisha: Mmiliki wa Los Angeles Clippers, Donald Sterling hawezi kujihusisha na masuala ya mpira wa kikapu baada ya kutoa kauli ya kibaguzi hadharani

UPITIAJI WA RASMU YA KATBA YA CLUB YA SIMBA WAMALIZIKA

 
unnamed (5)
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Rasimu ya Katiba ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba baada ya wanahabari kutaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya Katiba na uchaguzi wa Klabu hiyo.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali za waandishi leo jijini Dar es Salaam.
Akijibu moja ya hoja iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika upatikanaji wa Katiba ya Club ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji wa Katiba umemelizika na kuonekana kuwa na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha katiba hiyo.
“Mchakato wa upitiaji wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini kumekuwepo na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha Katiba hiyo” amesema Bw. Thadeo.
Akifafanua zaidi Bw. Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande wa kisheria ambapo mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana tofauti na Katiba ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya marekebisho hayo mapema na kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya kuidhinishwa.
Aidha Bw. Thadeo amewataka waandishi wa habari pamoja na wanachama wa Club ya Simba kuwa na subira ili waweze kupata Katiba itakayokidhi malengo ya Club yao kwani mchakato wa upitiaji wa Katiba ulihitaji umakini. 

Na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)

WAFANYAKAZI 'KATIBA NA SHERIA ' WAASWA KUCHPA KAZI

 ts Baraza 2
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde. (Picha na Martha Komba – Wizara ya Katiba na Sheria).
Baraza 1
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014).
Baraza 3


Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo (Alhamisi April 30, 2014) jijini Dar-es-salaam.
“Uwajibikaji ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar-es-salaam.
Aidha, Katibu Mkuu huyo aliwasihi watumishi wote wa Wizara yake kuungana na wafanyakazi wote nchini na duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi zinazofanyika kesho (Alhamisi, Mei 1, 2014).
Awali akiongea katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.
“Tunapodai maslahi ni lazima pia tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai maslahi bora,” alisema Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya Wizara hiyo.
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia na kuridhia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2014/2015. 

Na Martha Komba, Dar es Salaam

HATARI:TANESCO YAFUNGA NYAYA JUU YA MTI BAADA YA NGUZO KUVUNJIKA

 
unnamed
Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi.
unnamed (1)
Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti.
unnamed (2)
Hizi  ni waya zilizopita chini kabisa katika Geti la mtu na ndani ya miti.
unnamed (3)
Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
unnamed (4)
unnamed (5)
Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika.
unnamed (6)
Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
*****
Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni   jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na  miundo mbinu mbalimbali .
Uharibifu mkubwa na wahatari  ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika  na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.
Katika eneo la Mlalakuwa  mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe  pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika  kabisa na nyingine mbili zimelegea  katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni  mti huo si mkavu ni mbichi.
Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?
Tunaomba  muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapobaadae  kwani ni hatari sana
Picha na Dar es salaam yetu Blog.

HALMASHAURI KUU YA CCM LUDEWA YAMPONGEZA MBUNGE FILIKUNJOMBE


 Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya  leo kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) kutoka Ludewa Elizabeth Haule 
........................................................................................................................................
CHAMA  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe  kimempongeza mbunge wa  jimbo  hilo Deo Filikunjombe kwa  jitihada zake  mbali mbali za utekelezaji  wa ilani ya CCM katika jimbo hilo.

Pongezi  hizo  zimetolewa na mwenyekiti  wa CCM wilaya  hiyo Stanley Kolimba  wakati  akifungua  kikao  cha Halmashauri  kuu ya CCM  wilaya mjini Ludewa leo

Kolimba  alisema  kuwa mbunge utendaji kazi  wa mbunge huyo umeendelea  kuwa chachu ya  kimaendeleo  katika jimbo  hilo na  kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani kubwa na CCM.

Alisema mbunge huyo amekuwa mfano wa  kuigwa katika kufanikisha utekelezaji  wa ilani ya CCM na  kudai  kuwa jitiihada kubwa zinazofanywa na Filikunjombe zitasaidia  kuwafanya  wananchi  kuendelea  kuwa na mapenzi zaidi na CCM.

"Kweli  mbunge  wetu  amekuwa ni mfano wa  kweli katika kufanikisha maendeleo ya jimbo letu na wilaya  na hata majirani wamekuwa  wakipongeza utendaji kazi  wake "

Katika  hatua  nyingine CCM  wilaya  ya  Ludewa  kimewapa pore wananchi wa kata ya Rupingu ambao wamepatwa na majanga  ya mali zao mbali mbali yakiwemo mazao kuharibiwa na mvua kubwa  zinazoendelea kunyesha katika maeneo  mbali mbali  hapa nchini.

"Mbali ya  mvua  zinazoendelea  kunyesha kusaidia  kutupa neema  ya mazao  yetu  ila wenzetu  wa Rupingu  wamepatwa na majanga  makubwa  kutokana na mvua  hizo hivyo tunawapa pore kwa majanga  haya yaliyowakuta."

Hata  hivyo  baadhi ya wajumbe  wa Halmashauri kuu ya  CCM Ludewa  walipongeza  jitihada  za  serikali ya  awamu ya nne  na jitihada za mbunge  wao katika  suala  zima la uboreshaji wa miundo mbinu katika  wilaya  hiyo ya Ludewa kutokana na kuwa na miundo  mbinu rafiki isiyosumbua sana ukilinganisha na maeneo mengine.

Pia  waliiomba serikali kwa  mwaka huu  kuangalia  uwezekano wa  kutenga  bajeti  kubwa  zaidi ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa mahindi ya  wananchi wote  kutokana na kuwepo kwa dalili nzuri  zaidi ya wakulima katika  wilaya  hiyo  kupata mazao zaidi  ukilinganisha  na miaka iliyopita.

Kwani  walisema kutokana na jinsi ambavyo  wakulima wengi  walivyopata mazao na kulima  zaidi  upo  uwezekano  wa  wakulima  kukosa  soko la mazao  yao yote ama  wenye  fedha  ndio  watakaonufaika  zaidi na soko  hilo.

Kwa  upande  wake  mbunge Filikunjombe  aliipongeza  serikali ya Rais Jakaya  Kikwete kwa  kuendelea  kuboresha maisha ya  wana Ludewa kwa  kufungua milango  mbali mbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza  uboreshaji wa miundo mbinu ya  wilaya  hiyo.

Kwani  alisema  mbali ya kuanza  uboreshaji wa miundo mbinu  hiyo tayari  wilaya ya  Ludewa  kwa mara  ya kwanza  toka nchi ipate  uhuru  wake  mwaka 1961  kwa  kipindi  hiki ambacho amekuwa mbunge wa  jimbo  hilo tayari  wananchi  wa Ludewa  wameanza  kuona ujenzi wa barabara ya lami ukianza pamoja na  wananchi wa pembezoni ambao hawajafanikiwa kuwa na umeme  hivi sasa zoezi la kuwafikishia  umeme  limeanza.

AJALI YAUA MMOJA YAJERUHI 40 WILAYANI SUMBAWANGA

MTU mmoja amefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa baada ya ajali ya gari lililokuwa likitokea  katika kijiji cha Mkima Wilayani Sumbawanga kuacha njia na kupinduka na kutumbukia mtaroni.

Gari hilo aina ya Fuso lililokuwa limebeba  wachezaji wa mpira ambao walikuwa wakielekea  kijiji cha Mkima wakitokea Ilembo kwa ajili ya mechi ya kirafiki na kusababisha ajali baada ya kutumbukia mtaloni.

Kamanda wa polisi Mkoani Rukwa Jacob  Mwaruanda alisema mara baada ya gari hilo kupinduka lilisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Enani(18) aliyekuwa kapanda juu ya bomba na kusababisha kifo chake.

Kamanda Mwaruanda aliwataja baadhi ya majeruhi waliotibiwa na kuondoka kuwa ni Edmundy Nkalawa,Henrk Kaulule,Revokatus Malambika,Philibeth Zumba,Omary Jeusha,Joel Raphael na Lukas Kang’nga.

Wengine ni Daudi Sabino,Novakatus malambika,Seris Kisanzo,Aman Shaban,Crispin Nkalawa na Menady Msumbachika  ambao wote ni wakazi wa Lembo na  walitibiwa na kuondoka katika Hospital ya Mkoa.

Jeshi la polisi  lisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea dererva huyo alitoroka na upelelezi wa awali unafanyika na mara atakapo kamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayiomkabili.
 
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga

JOSE CHAMELEONE KESHO KUSHEREHEKEA MEI MOSI VILLA PARK MWANZA.

SIKILIZA MPANGO MZIMA.
MSANII Maarufu kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone, anaye Sherehekea siku yake ya kuzaliwa leo tarehe APRIL 30, anatarajia kushuka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa burudani ya mtikisiko kwa mikoa ya Mwanza na Geita wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi duniani (MEI MOSI na Siku inayofuata).


Meneja wa Burudani wa Klabu ya burudani Villa Park Resort Ramadhan Maganga, alisema kwamba Uongozi wa Villa Park Resort ya jijini Mwanza na Alpha Hoteli ya mkoani Geita wameshirikiana kumleta mwanamziki huyo ili kukata kiu ya wakazi wa mikoa hiyo iliyowashika kwa kipindi kirefu.

“Ni kipindi kirefu watu wanashuhudia kazi zake kupitia Luninga (TV) na kuzisikia kwenye vipindi vya Redio, na chakutamanisha zaidi ni pale wanapoona Chameleone anapozindua nyimbo mpya zilizo kali na kumkosa kwenye majukwaa ya maeneo yao hivyo kuzidisha kiu na hamu, sasa hii ni fursa ya pekee kwao kumshuhudia live akilitawala jukwaa” alisema.

Rama ameongeza kuwa, Dr. Chameleone wa sasa ni tofauti na wa kipindi cha nyuma, kwanza ameongeza orodha ya nyimbo  mpya kali na nzuri zikiambatana na Albam zake zinazokubalika na kupendwa na mashabiki wa burudani ya muziki, pili ameboresha zaidi mitindo ya uingiaji jukwani ikiwemo mavazi yanayo muweka katika hadhi na mwonekano wa juu zaidi kimataifa.

“Ratiba itaanza siku ya MEI MOSI  kwa Dr. Chameleone kutoa show kali kwa wakazi wa Jiji hili (Mwanza) na kutoka sehemu mbalimbali Kanda ya ziwa watakaokuwa mametoka kuhudhulia Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi Duniani kwa kingilio cha shilingi 15,000/= mlangoni watamshuhudia mkali huyo akisindikizwa na Bendi ya Muzuki wa Dansi Super Kamanyola ya jijini hapa” alisema.

Aidha alieleza kuwa kwa sasa Dr. Chameleone aliye maliza ziara yake hivi majuzi nchini Uingereza akitamba na nyimbo zake kali kama Valuvalu, Badilisha na wimbo wake mpya wa Tubonge, ameahidi kutoa Burudani ya kiwango zaidi tofauti na kile kilichozoeleka na mashabiki wake.

Burudani ya Disco na Muziki wa Mwambao iko palepale kama ilivyo kawaida ya siku zote, hivyo watakaolipa kingilio cha sh. 15,000/= mlangoni watapata fursa ya kushuhudia burudani yote bila kutozwa tena kingilio cha ziada mlangoni.

“Ratiba ya burudani kwa mwanamuziki Dr. Chameleone itamalizikia kwa kufanya show kali kwa wakazi wa Mji wa Geita na maeneo ya jirani siku ya Ijumaa, Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Omega Resort Hotel  kwa kingilio cha shilingi 15,000/= tu mlangoni”alisema

Meneja huyo ametoa wito kwa wapenzi wa burudani na wafanyakazi bora watakaozawadiwa kusherehekea kwa pamoja ndani ya Villa Park Resort pamoja na kupata show kali kutoka kwa Dr. Chameleone ambapo pia kutakuwa na chakula na vyinywaji mbalimbali, ulinzi wa mali umeimalishwa kwa asilimia 100, akiwataka wapenzi wa burudani kuwahi ili kupata nafasi na tiketi zitapatikana mlangoni tu.
HAPPY BIRTHDAY DR. JOSE CHAMELEONE
Say's G. Sengo.

LISHE ASILI NI DAWA YA WAGONJWA WAMOYO

 
140430034802_kula_vyakula_asili_inazidisha_miaka_ya_wagonjwa_wa_moyo_512x288_bbc_nocredit_c9f25.jpg

Wanasayansi nchini Marekani wanasema watu waliowahi kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi maisha marefu iwapo watakula zaidi vyakula ambavyo havijapitia viwandani.
Watafiti walichunguza zaidi ya watu elfu nne waliowahi kupata mshituko wa moyo na kubaini kuwa wana uwezekano mkubwa wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula vyakula hivyo .
Vyakula ambayo havijapitia viwandani vina nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa husaidia katika kuwezesha binadamu kwenda haja bila matatizo.
Vyakula ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.
Hatahivyo wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.CHANZO BBC

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MJUMBE WA RAIS WA BURUNDI IKULU DAR

 
ru1
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika na ujumbe wake kuwasilisha ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam April 29, 2014.
ru2
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Sheikh Mohamed Rukara, ujumbe  maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza, aliyeuwasilisha  ujumbe huo Ikulu jijini Dar.
ru3
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Sheikh Mohamed Rukara, Mjumbe maalum wa Rais wa Burundi Mhe Pierre Nkurunzinza, alipofika  kuuwasilisha ujumbe huo Ikulu jijini Dar.(Picha na IKULU).

SHILINGI 2,000 ZILINIPONZA NIKAIBIWA MTOTO

 
boka 7a13d

Aprili 6, mwaka huu ni siku ambayo mkazi wa Kijiji cha Kibanda wilayani Kyela, Mboka Mwakikagile (20) haitaisahau.

Ni siku ambayo aliibiwa mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na umri wa siku saba tu.
Akisimulia tukio hilo, Mboka anasema alijifungua salama Machi 30 akiwa nyumbani kwa wazazi wake ambao ni Lupalo Mwakikagile (90) na mkewe Nelly Kyusa (49).
Anasema akiwa katika siku ya saba, alipigiwa simu na mzazi mwenzake (jina linahifadhiwa) kwamba mama yake mkubwa atafika nyumbani kumwona mtoto.
Anasema baada muda mfupi mwanamke huyo alifika kwa pikipiki akiwa na mkoba uliokuwa na nguo za mtoto, sabuni na vifaa vingine. "Baada ya kumkaribisha na kusalimiana na wote , mwanamke huyo alimchukua mtoto na baadaye alinishauri twende Zahanati ya Njisi akatibiwe jicho ambalo lilikuwa linamsumbua kidogo,''anasema.
Mboka na mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pikipiki na kwamba baada ya kufika hapo, daktari aliwataka wanunue daftari na mwanamke huyo alitoa Sh2,000 na kumtaka akanunue.

''Nilipokea fedha hizo na kumwachia mtoto pamoja na simu yangu wakati mimi nikielekea kununua daftari kwenye duka lililo mbali na zahanati hiyo,'' anasema.
Anasema mara baada ya kurudi dukani alishtuka kutomwona mwanamke na mtoto wake.'Kitendo hicho kilinishtua zaidi kwani mzazi mwenzangu aliondoka bila ya kunishirikisha kwamba tukaripoti polisi na kibaya zaidi yeye ndiye aliyedai kwamba ni mama yake mkubwa,'' anasema 
CHANZO MWANANCHI 
Na Hudugu Ng'amilo

HIVI NDIVYO RONALDO ALIVYO AVUNJA REKODI YA MESSI

 
140429194121_cristiano_ronaldo_real_madrid_512x288_afp_nocredit_79dc4.jpg

Nyota wa Real Madrid ya Uhispania Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi katika ligi ya mabingwa barani Uropa alipoifungia timu yake mabao mawili na kuisaidia kuichapa Bayern Munich mabao 4-0 katika nusu fainali jana usiku
Mreno huyo mwenye umri wa miaka , 29,alifunga bao lake la 15 na 16 msimu huu katika uwanja wa Allianz Arena.
Kufuatia ushindi huo Real Madrid ilifuzu kwa fainali ya mchuano huo kwa jumla ya mabao 5-0.
Ronaldo sasa amefunga mabao 16 katika mechi kumi za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mbili zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona .
Rekodi hiyo ya mabao 14 ilikuwa ikishikiliwa kwa pamoja kati ya Messi (2011-12, Barcelona), Ruud van Nistelrooy (2002-03, Manchester United) na Jose Altafini (1962-63, AC Milan).
Kwa jumla Ronaldo amefunga mabao 67 katika ligi hiyo ya mabingwa barani ulaya sawa na Messi na ni mabao manne tu nyuma ya rekodi ya idadio kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji wa zamani wa Real na Schalke Raul.CHANZO BBC, NA MBEYAGREENNEWSBLOG

SEMINA YA WAANDISHI KUHUSU UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU YAFANYIKA ZANZIBAR

PICT2016
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
TATIZO la Wananchi  kujichukulia hatua mikononi mwao na matumizi ya nguvu zisizo za lazima kwa baadhi ya vyombo vya dola ni changamoto kubwa inayodhoofisha utekelezaji wa haki za binadamu.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria Zanzibar HarusiMiraji Mpatani kwenye  mafunzo ya Haki za Binadamu yaliyoandaliwa kwa ajili ya Waandishi wa habari katika  Ofisi ya Kituo hicho  Migombani Mjini Zanzibar.
Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao  pale inapotokea tuhuma  inayopelekea kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Amesema licha ya juhudi zinazochukuliwa katika kuhakikisha kuwa sheria ya haki za binadamu zinafikiwa kwa jamii,  bado matukio ya uvunjwaji na ukiukwaji  wa Haki za binadamu yanaendelea kutokea nchini.
“Watoto na walemavu wamekuwa ni wahanga wakubwa wa matukio ya unyanyasaji na udhalilishaji wa kingono, mbali na hali dhaifu ya kimaumbile waliyonayo bado jamii haijabadili mtazamo kuwa kundi hili linahitaji kulindwa kutokana na vitendo hivyo”, alifahamiisha Bi Harusi.
Aidha ameeleza kuwa waandishi wa habari wanawajibu katika kusimamia haki hizo kwa kutoa taaluma juu ya haki za binadamu kwa jamii wanayoifanyia kazi kwa kutumia vyema kalamu zao ili kujiepusha kuandika habari zinapelekea  uchochezi na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu.
Amewataka Waandishi kufuatilia bila ya woga matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ili kuweza kuibua matukio mbali mbali ili  sheria iweze kuzifanyia kazi na kuondosha matatizo hayo.
Mada nane zinatarajiwa kujadiliwa katika mafunzo hayo zikiwemo Ufafanuzi wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Haki za Binadamu na nafasi ya Waandishi wa habari katika kusimamia Haki za Binadamu, Utawala bora pamoja na Utawala wa Sheria.
Mafunzo hayo  ya siku mbili yametaarishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar  na yanawashirikisha waandishi wa vyombo mbali mbali  vya Habari vya Serikali na biinafsi nchini.

KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI AMKARIBISHA RAIS KWETE ARUSHA

 
katibu eac 
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Richard Sezibera akimkaribisha Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo unaofanyika leo (picha na Freddy Maro).

HIVI NDIVYO BFT WALIVYO MPONGEZA MH BERNAD MEMBE

index 
Shirikisho la ngimi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Waziri  wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Bernard Membe kwa hatua na jitihada alizozifanya  za kutafua na kufanikisha  kambi ya mazoezi kwa Timu ya Taifa ya ngumi  inayojiandaa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini Scotland.
Kwa hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na maandalizi ya Timu  yetu ya Taifa kwa kuitafatia  kambi ya mazoezi ya kimataifa Nchini Uturuki na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika hali duni  bila ya kuwa na vifaa vya kisasa kulingana na mabadiliko ya mchezo wa ngumi duniani.
Kwa kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri ya ushiriki waTanzania katika mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa mara ya kwanza Tanzania ilishiriki mwaka 1972 na Tanzania  kupata medali ya kwanza ya kimataifa baada ya   Tanzania kupata  uhuru, iliyoletwa na Bondia (LYTUS SIMBA) na baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta medali ni kama wafuatao:

MICHAEL YOMBAYOMBA   :  (Dhahabu)
HAJI  MATUMLA                     :   (Fedha)
MAKOYE ISANGURA             :   (Shaba)
MWAMBEYA   BAKARI        :   (Shaba)
WILLY  ISSANGURA              :   (Shaba)
LUCAS MSOMBA                   :   (Shaba)
Bado BFT tunamuomba azidi kutusaidia  vifaa zaidi hasa ulingo wa kisasa na Computer inayotumika  kuhesabia point za ushindi wakati wa mashindano kwani Nchi zote duniani ndizo wanazozitumia na niagizo kutoka chama cha ngumi cha dunia kwa wanachama wote lazima waitumie katika mashindano..