Thursday 24 April 2014

SIMBA YAMALIZWA NA MABADILIKO YA BENCHI LA UFUNDI!!

DSC0659-610x400 
Baraka Mpenja  , Dar es salaam
MABADILIKO ya mfululizo katika benchi la ufundi imetajwa kuwa moja ya sababu ya Wekundu wa Msimbazi kufanya vibaya msimu wa 2013/2014 uliomalizika aprili 19 mwaka huu kwa timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na watani zao wa Jadi, Yanga SC. Simba walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 4 baada ya kujikusanyia pointi 38 pekee katika michezo 26. Ally Mayay Tembele, beki na nahodha wa zamani wa Yanga sc na sasa kocha wa mpira wa miguu amesema kuwa kubadili benchi la ufundi mara kwa mara kunaleta athari ya moja kwa moja katika kikosi. “Kila mwalimu ana falsafa yake, kwahiyo unapobadili kocha ujue kabisa unaleta mfumo mpya katika klabu ambao utahitaji muda ili wachezaji wazoee”. “Msimu wa 2011/2012 alikuwepo kocha Mserbia Milovan Circovic, baadaye akaja mfaransa Patric Liewig. Akiwa ameshaanza kuijenga Simba ya vijana na sasa wanaanza kumuelewa, akaondolewa na kuletwa Abdallah Kibadeni. Hawa ni walimu watatu tofauti na wana aina yao ya ufundishaji” “Wachezaji ndani ya muda mfupi walijikuta wakilishwa mifumo tofauti. Sasa walishindwa kushika kwa haraka kwasababu wakianza kuzoea kunatokea mabadiliko”,
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

0 comments: