MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday 28 September 2013

MFUNGWA ANASWA AKIJIUZA


AIBU:MFUNGWA ANASWA AKIJIUZA-NI YULE MCHUMBA WA MTU ALIYEHUKUMIWA MIEZI 6

BAADA Mei mwaka huu kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kufanya ukahaba, mkazi wa jijini Dar, Blandina Barton amekamatwa tena kwa kosa  hilohilo ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kumaliza kifungo chake, Risasi Jumamosi linakupa mkasa mzima.
 

Habari za uhakika zilizopatikana katika Mahakama ya Jiji, Dar es Salaam zinasema kwamba mfungwa huyo alitumikia kifungo chake katika Gereza la Segerea jijini Dar na alipobakiza miezi michache kumaliza alionewa huruma na bibi jela na kutakiwa kumalizia kifungo hicho uraiani.
Inadaiwa kuwa kabla ya kuachiwa, bibi jela alimsihi Blandina kuhakikisha harudii kosa lililompeleka gerezani pindi atakapokuwa akimalizia kifungo chake nje ya gereza.

Blandina akamhakikishia bibi huyo kwamba atakuwa mtu safi kwani amejifunza vya kutosha.

 

Katika hali ya kushangaza, Jumatano iliyopita Blandina alipandishwa tena katika Mahakama ya Jiji iliyopo Barabara ya Sokoine jijini Dar akiwa amerudia kosa lililompeleka Segerea miezi michache iliyopita.
 

Imeelezwa mahakamani hapo kwamba, Septemba 24, mwaka huu Blandina na wenzake wanne walinaswa Buguruni usiku wakiwa katika mawindo ya ukahaba.
Bahati mbaya kwa Blandina alipofikishwa mahakamani hapo alikutana na hakimu yuleyule aliyemhukumu kifungo cha miezi sita kwa kosa la ukahaba.

 

Hakimu huyo, Timothy Lyon alipigwa na butwaa baada ya kumuona Blandina akiwa amesimama mbele yake.
Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na wenzake, Husna Amos, Monica Denis, Esther Chizai na Angela Emmanuel wote kwa pamoja walisomewa mashtaka yao na kukana.

Hakimu Lyon aliwaambia watuhumiwa hao kwamba dhamana iko wazi na kuwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili na shilingi laki mbili.

 

Sharti hilo lilionekana kuwa gumu kwa watuhumiwa wote, hivyo walipandishwa karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Oktoba 15, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena mahakamani hapo.
 

Mei mwaka huu gazeti dada na hili la Ijumaa liliandika habari za kifungo cha Blandina mara baada ya kuhukumiwa kwenda jela huku ikidaiwa kwamba msichana huyo ni mchumba wa mtu.
Source:GPL

Tuesday 24 September 2013

MPANGO WAKULIPUA BOMU ZANZIBAR DARAJANI WAFELI

Picture
Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Mkadam Khamis Mkadam
Watu wasiofahamika bado, usiku wa kuamkia jana Jumatatu walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililokuwa katika mfano wa 'sausage' karibu na eneo la biashara kando ya Barabara ya Darajani mjini Zanzibar.

Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis Mkadam akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu taarifa hiyo alisema, mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour (36), aliyekuwa kazini kwenye
 Duka la Sahara, aliona idadi ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakitokea Bwawani kuelekea Mkunazini, walikwenda uelekeo wa dukani alipokuwa akilinda, na walipofika hapo walipunguza mwendo, ndipo mmoja wao aliporusha guruneti upande wake, na kitu hicho kilitua katikati ya masanduku yaliyokuwa mbele ya duka hilo.

"...lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa, Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," "Kwa bahati, Amour alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku," alisema Mkadam akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti kubwa dakika chache baadaye.

Polisi walifanikiwa kupata mabaki ya unga unga na kukusanya kokoto zilizotokana na athari ya mlipuko huo.

Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, na kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa. 

 

Friday 13 September 2013

KUKU AIFIKISHA HALIMASHAURI MAHAKAMAIN

Picture
HALMASHAURI ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, imeshinda
 kesi iliyofunguliwa na mkazi wa Kijiji cha Nyamakobiti, wilayani humo, Bw. Charari Chacha, akipinga halmashauri hiyo kuuza kuku wake kwa gharama ya sh. 1,000 baada ya kukataa kulipa mchango wa ujenzi wa Shule ya Msingi Nyamakobiti
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Goody Pamba, alisema kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2000 na hukumu kutolewa katika Mahakama ya Rufaa jijini Mwanza.

Alisema Bw. Chacha alifungua kesi hiyo namba 46.2008 baada ya kushindwa katika kesi ya awali namba 18/2000 aliyoifungua katika Mahakama ya Mkoa. Aliongeza kuwa, Mahakama ya Rufaa jijini 

Mwanza, ilitoa hukumu Septemba 3 mwaka huu, ambapo Bw. Chacha, alishindwa tena kwa mara ya pili.

Bi. Pamba alisema, hadi sasa gharama zilizotumika kuendesha kesi hiyo tangu mwaka 2000 hazijafahamika. Diwani wa kata hiyo, Bw. Rashidi Mugare, alisema kuanzia mwaka 2000-2013, maendeleo y a kijiji hicho yalirudi nyuma kutokana na wananchi kutochangia shughuli za maendeleo.

“Kila mtu alipotakiwa kuchangia shughuli za maendeleo, alitishia kwenda mahakamani kama alivyofanya Bw. Chacha, wachache ndiyo waliokubali kuchangia. Baadaye Bw. Chacha alimkomboa kuku wake kwa gharama ya sh. 1,000, hadi sasa kijiji chetu ni cha mwisho katika suala zima la maendeleo kulingana na sumu iliyomwagwa, kimsingi kesi hii ilikwamisha mambo mengi ya maendeleo,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho, kuchangia maendeleo ya elimu ambayo ndio dira ya maisha badala ya kuendeleza malumbano na kufungua kesi mahakamani.Aliwataka wasijiingize kwenye gharama wasizoweza kuzimudu kwa kufungua kesi ambazo hazina tija yoyote kwani suala la maendeleo ni kwa faida ya wananchi, Taifa kwa ujumla. 

Veronica Modest, 
MAJIRA, Serengeti

 

MWALIMU ACHAPWA VIBOKO 30 NA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA KUMBAKA MWANAFUNZI MKOANI NJOMBE

Mahakama ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na kuchapwa viboko 30 mwalimu wa shule ya msingi Ingwachanya. Mwalimu huyo Bw. Romanus Msango mkazi wa  Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) na kumuumiza vibaya sehemu za siri.

Akisoma hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Bw. Fredrick Lukusa, alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka amabao haukua na shaka yoyote.

Alisema mshakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 1309(!) na 31(!) cha kanuni ya adhabu ya 
mwaka 2002 hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine. “Natoa adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii kwani vinaleta madhara makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa ya kuambukiza,” alisema.

Awali ilidaiwa na mwendesha mashtaka, Edson Kasekwa kuwa, mshtakiwa alitenda ukatili huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika kijiji cha Masimbwe, Kata ya Mlangali. Alisema kabla mshtakiwa hajatenda kosa hilo, alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na kumlawiti jambo ambalo limemsababishia maumivu makali.

“Serikali ilimpa mshtakiwa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvu kazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yake, kuidhalililsha taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundishokwa walimu wengine,” alisema.

Bw. Kusekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani wakati akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda  kijijini kutoa taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.

Wakati huo huo, watu wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve, wote wakazi wa Milo, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia maumivu makali.

Nickson Mahundi, 
MAJIRA, Ludewa

 

Saturday 7 September 2013

SERENGEIT FIESTER SEPTER 6 MBEYA 2013 YA FUNIKA KULIKO ZOTE TICKET ZILIISHA KABLA SHOW


 

Fiesta mbeya 6
Ni show ambayo ticket zimeisha na inaingia kwenye list yangu ya show za Fiesta zilizovunja rekodi mwaka huu…. Thank you watu wangu wa nguvu Mbeya 87.8, sasa inafata zamu ya Iringa 92.9 Jumapili hii september 8 2013 tunakuja hapo.
Fiesta Mbeya 7
Fiesta mbeya 8
Fiesta Mbeya 4
fiesta Mbeya 5
fiesta mbeya 3
Fiesta Mbeya 2
2
1
4

WACHIMBA MIGODI (A.K )WAREJEA KAZINI AFRIKA KUSINI

 
Wachimba migodi wanaounga mkono chama cha wafanyakazi nchini Afrika Kusini
Wengi wa wachimba migodi wa dhahabu ambao wamekuwa wakigoma tangu Jumanne nchini Afrika Kusini wamerejea kazini baada ya waajiri wao kukubali kuwapa nyongeza ya mishahara.
Kwa mujibu wa maafisa wa chama cha kitaifa cha wafanyakazi, kampuni nne kati ya saba zimekubali kuwapa nyongeza wafanyakazi hao ambayo inaaminika kuwa asilimia 8.
Chama hicho kilikuwa kinataka 60%, wakati waajiri wao wakipendekeza kuwapa asilimia sita ikiwa sawa na kiwango cha mfumuko wa bei nchini humo.
Wachimba migodi walikuwa wametishia kuwa mgomo wa muda mrefu ungesababisha migodi kufungwa na maelfu ya watu kupoteza kazi zao, kufuatia kushuka kwa bei ya dhahabu.
Wanasema kuwa bei ya kuzalisha madini hayo imepanda kwani wamelazimika kuchimba mita nyingi chini ya ardhi kupata madini hayo.

Kwa miaka mingi Afrika Kusini ilikuwa nchi yenye kuzalisha dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote duniani uikiwa ni asilimia 68 mapema miaka ya sabini lakini mambo yamebedilika sasa ikiwa inazalisha tu asilimia sita ya dhahabu yote duniani, hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP

Chama cha wafanyakazi NUM kinawakilisha takriban asilimia 64 ya wachimbaji wa dhahabu kote nchini humo.
Mwaka jana wananchi wengi waliachwa vinywa wazi wakati polisi walipowaua wafanyakazi 34 wa migodi ya platinum wakati wa mgomo haramu ulioitishwa na chama hasimu cha wafanyakazi.

 

ENGLAND YAIPASUA MOLDOVA 4-0 NA KUONGOZA KUWANIA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA






England: Hart, Walker, Cole (Baines, 45), Cahill, Jagielka, Gerrard, Walcott, Lampard, Wilshere (Barkley, 59), Welbeck, Lambert (Milner, 70)
Subs not used: Ruddy, Forster, Smalling, Carrick, Cleverley, Young, Sterling, Townsend, Defoe
Goals: Gerrard 12, Lambert 26, Welbeck 45, 50
Booked: Welbeck.
Moldova: Namasco, Armas, Golovatenco, Epureanu, Bulgaru (Suvorov, 57), Bordiyan, Ionita (Onica, 19), Antoniuc, Dedov, Gheorghiev (Pascenco, 84), Sidorenco
Subs not used: Pascenco, Cebanu, Racu, Boestean, Erhan, Cebotaru, Gheorghe Andronic, Doros, Grosu
Ref: Ivan Kruzliak.


Attendance: 61,607.




ANGALIA WAKAZI WA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE FURSA YA VIJANA NA CLOUDS MEDIA NDANI YA TEKU.

  


 Sehemu ya vijana waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikijadiliwa ukumbini humo.
Muwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika mapema leo  kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
Mmoja wa Vijana Wajasiliamali ,ambaye ana mradi mkubwa wa kuuza juisi,Gasto Sony mkazi Uyole mkoani Mbeya,akieleza zaidi kwa vijana wenzake waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo,namna ambayo ameweza kuitumia fursa alioipata na kuwa mjasiliamali wa kuuza juisi kisasa kabisa.
  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza na wakazi wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,filiofanyika leo asubuhi ndani ya ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU),kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.Kampuni ya Serengiti ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2013 linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja Sokoine.
  Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. 
 Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea
 Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza jambo na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitway Niki wa Pili ndani ya semina ya Fursa kwa vijana.
Muwakilishi kutoka shirika la TPSF,Bwa.Louis Accaro akifunguka kuhusiana na mambo ya fursa kwa vijana na nanmna ya kuzichangamkia mara zipatikanapo.
 Mdau wa Kilimo kutoka mkoani Mbeya,Bwa.Yona Daniel akizungumzia fursa zinazopatikana kwenye kilimo,ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye suala zima la kilimo.

 Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea.Semina kama hii imekweíshafanyika kwenye mikoa ya Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara na leo mkoani Mbeya.

SHULE YA MSINGI LUKUNG WILAYA YA MISUNGI MKOA WA MWANZA YA KABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO

Picture
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungi Mkoani Mwanza wakifurahia kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni yaVodacom walivyokabidhiwa ilikushiriki vema katika shughuli za michezo wawepo shuleni.  Vifaa vilivyotolewa ni jezi seti mbili za mpira wa soka, seti moja ya mpira wa pete, mipira na fulana za mazoezi.


 

TAARIFA YA JWTZ KUHUSU USHIRIKI WAKE KWENYE OPERESHENI YA AMANI KONGO

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo : “NGOME” Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo : DSM  22150463      
Telex : 41051  
Sanduku la Posta 9203,
DAR ESSALAAM.

06 Sep

Ushiriki wa Tanzania katika Operesheni ya Ulinzi wa Amani nchini DRC, unatokana na mgogoro kati ya Serikali DRC na waasi hususan kikundi cha waasi cha M23. Mgogoro huo ulianza mwezi Aprili 2012 ambapo kikundi cha M23 kilijitoa katika Jeshji la serikali ya DRC na kuanzisha mapigano hali iliyopelekea hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.

Kufuatia hali hiyo mbaya ya usalama, wakati wa kikao cha International Conference on the Great Lakes Region kilichofanyika tarehe 12 Julai 2012 mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mhe. Rais Joseph Kabila aliwasilisha ombi kwa 
Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambazo Rwanda, Uganda, Tanzania,  na DRC akaomba nchi wanachama wa Maziwa Makuu zisaidie kuwapokonya silaha waasi wa M23.

Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu walikubaliana na ombi hilo na kutoa maelekezo kwa Mawaziri wa Ulinzi ambao walikutana tarehe 01 hadi 2 Agosti 2012  na kujadili maelekezo ya Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu. Mawaziri wa Ulinzi walikubaliana kuwa ni muhimu kwa vikundi vyote vya Waasi (ADF, FDLR na M23) kushughulikiwana wakawasilisha mapendekezo yao kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu.

Tarehe 7 Agosti 2012, Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu walikutana tena mjini Kampala, Uganda na kupanga mkakati wa kuanzishwa kwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na nchi wanachama wa Nchi za Maziwa Makuu zikaombwa kuchangia askari watakaounda ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ ambapo Tanzania iliombwa na ikahadi kuchangia kikosi kimoja. Kikao hiki kilitoa maelekezo ya hatua inayofuata kwa Mawaziri wa Ulinzi wa Maziwa Makuu.

Tarehe 7 hadi 8 Sep 2012, Mawaziri wa Ulinzi wa maziwa Makuu, walikutana na kujadili utekelezaji wa uanzishwaji wa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’. Wakaunda ‘Military Assessment Team (MAT)’ kufanya tathmini ya tishio. Timu hiyo ililifanya tathmini na kuwasilisha taarifa yake kwenye kikao cha Mawaziri wa Ulinzi kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2012 mjini Goma, DRC na baadaye taarifa hiyo iliwasilishwa kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambao waliagiza kushirikishwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika(AU) na Umja wa Mataifa(UN) ili kufanikisha mkakati huo.

Nchi wanachamma wa SADC na Nchi za Maziwa Mkuu kwa pamoja walikubaliana na kupendekeza SADC Standby Brigade ipelekwe DRC kama ‘Neutral Intervention Force (NIF)’. Kufuatia ridhaa hiyo nchi wanachama wa SADC ziliombwa kuchangia ambapo nchi mbalimbali wanachama zilikubali kuchangia, lakini Umoja wa Mataifa(UN) ilizipitisha nchi za Tanzania, Afrika Kusini na Malawi kuchangia askari nguvu ya Brigedi moja kuunda NIF ya MONUSCO.

Aidha, Umoja wa Mataifa mwezi Januari 2013 uliridhia mapendekezo ya Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu na Nchi wanachama wa SADC ya kuundwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na kupelekwa DRC. Kufuatia idhini hiyo tarehe 28 Machi 2013, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha     Azimio (Resolution) namba 2098 (2013) na kutoa jukumu maalumu la ulinzi wa amani nchini DRC, likijumuisha ushiriki wa Neutral Intervention Force (NIF) kama sehemu ya MONUSCO, na ikaitwa ‘Force Intervention Brigade (FIB)’ ambayo kikosi cha Tanzania ni sehemu ya Brigade hiyo.

Kwa mantiki hiyo ieleweke kwamba, Kikosi cha Tanzania kilichopo DRC ni sehemu ya SADC standby brigade iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO). Kinafanya kazi chini ya Force Commander, MONUSCO na majukumu yake ni:

    1. Kuzuia waasi kujitanua (Prevention of Expansion)
    2. Kuvunja nguvu za waasi (Neutralization)
    3. Kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.

Kwa kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa ya MONUSCO, inamanisha kuwa Operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa,  Tanzania haipigani na M-23 na haina tatizo na Rwanda kuhusiana na Operesheni hiyo na ridhaa ya kikosi chetu kwenda DRC ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni mwanachama wa nchi za Maziwa Makuu. Aidha, Rwanda imesaidia sana kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha watu, vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.

Friday 6 September 2013

ANGALIA CHEKA ALIVYOTINGA BUNGENI, PINDA, MWAKYEMBE WAJITOKEZA KUMPONGEZA

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AKIWA NA BINGWA MPYA WA DUNIA WA WBF, FRANCIC CHEKA NA FRANCIS MIYEYUSHO WALIPOTEMBELEA BUNGENI
WAZIRI WA UCHUKUZI, HARRISON MWAKYEMBE (WA PILI KULIA) AKISHOO LOVE KWA CHEKA, WANAYEMPA MKONO NI GEORGE MKUCHIKA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.

PICHA YA PAMOJA, CHEKA, MKEWE, PINDA NA MAPROMOTA WALIOONGOZANA NAYE BUNGENI. KUSHOTO NI MWALIMU WA NGUMI NCHINI, SUPER D.

CHEKA, MIYEYUSHO, PROMOMOTA BAWAZIRI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MBUNGE MAARUFU KATIKA MICHEZO, MAJI MAREFU BAADA YA KUTUA BUNGENI. PICHA ZOTE NA SUPER D

GARETH BALE KUANZIA BENCHI KATIKA TIMU YAKE YA TAIFA

 
BALE MAZOEZINI NA WALES, JANA.

Nyota mpya wa Real Madrid, Gareth Bale yuko tayari leo kuichezea timu yake ya taifa ya Wales katika mechi dhidi ya Macedonia itakayopigwa leo jioni katika mji wa Skopje, lakini huenda ‘akakalia ubao’.



Bale ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi kwa sasa amekuwa akiendelea vizuri na mazoezi lakini bado inaonekana hayuko fiti.


Kocha Msaidizi, Kit Symons ambaye ataiongoza timu hiyo baada ya bosi wake, Chris Coleman kuchemsha katika suala la pasi ya kusafiria na kulazimika kubaki Wales, amesema hawana uhakika na ufiti wa Bale.


“Amekuwa akifanya vizuri mazoezi na wenzake, lakini tunaamini hayuko fiti asilimia mia kwa kuwa hakufanya mazoezi ya kutosha katika pre season.


“Hivyo tunaangalia, lakini ikiwezekana ataanzia benchi,” alisema Symons.

Hata hivyo imekuwa ikielezwa, Bale kutoichea Wales katika mechi iliyopita ilikuwa ni janja ya kuikwepa Spurs ambayo tayari aliwaambia yeye ni mgonjwa.

ANGALIA PICHA ZOTE ZA VURUGU ZA BUNGE HAPO JANA NAFREEMAN MBOWE ALIVYO ONDOLEWA BUNGENI

Picture
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kukaa chini, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma jana
Jana, wakati wa kuchangia muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ukisomwa, wabunge wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walitoka nje wakishinikiza muswada huo usisomwe hadi maoni ya wadau kutoka Zanzibar yapatikane.

Leo, Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walitoka nje baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe kuamriwa atolewe nje na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai.

Hali hiyo ilitokea wakati wa Majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013.

Mhe. Mbowe alisimama ili achangie lakini aliamriwa na Job Ndugai kukaa chini jambo ambalo hakuliafiki na kuendelea kusimama, jambo lililomsukuma Ndugai kuwaamuru askari wa bunge kumtoa nje Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kitendo kilichozua mzozo.

Mhe. Mbowe aligoma kutolewa nje ya bunge baada ya askari kufika alipokuwa amekaa kwa lengo la kumtoa nje, ndipo mzozo mkubwa ulipotokea ndani ya bunge na kutamatia kwa Wabunge wote wa CHADEMA kutoka nje.
Picture
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa ameng'ang'ania microphone ya sehemu ya kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma. Mic hiyo iling'oka na polisi wakafaikiwa kumtoa nje.
UKUMBI wa Bunge leo uligeuka kuwa ulingo wa ngumi baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kutunishiana misuri na askari wa bunge hilo ambapo  Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe alipoamliwa kutoka nje na Naibu Spika Job Ndugai.

Hatua hiyo ilitokana  baada ya wabunge hao kupiga kura za kukubali au kukataa kuhusu kupitishwa kwa kujadili Mswaada wa Katiba uliopelekwa Bungeni hapo na Serikali ili kuweza kujadiliwa na bunge hilo.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe walipinga matokeo hayo na kuamua kusimama na wakati huo huo Spika Ndugai aliwataka kukaa chini ili kuendelea na kuchangia hoja za msingi za kujadili mswaada huo.

Ndugai aliwataka wabunge hao kukubaliana na matokeo yaliyotokea na kwa pamoja waweze kujadili mswaada huo 
ambao ni faida kwa taifa lakini mbali na ombi hilo kambi ya upinzani walikaidi ndipo Spika alitoa dakika tano kwa za kiongozi huyo kutoka ili bunge liendelee,ambapo hata hivyo kiongozi huyo alikaidi amri hiyo.

Baada ya mabishano hayo ndipo Spika alipotumia kiti chake na kuwataka askari wamtoe kwa nguvu nje ya ukumbi wa bunge, amri ambayo ilizua taflani na hekeheka kupelekea wabunge wa kambi ya wapinzani kuungana na kuwatunishia misuri askari hao wakimkingia kiongozi huyo kutolewa nje.

Tukio hilo lililochukua dakika zaidi ya 30 lilipelekea Bw. Job Ndugai kuwatolea macho askari hao akiwaamuru kutumia mabavu ili kuweza kumtoa nje ya ukumbi Bw. Mbowe.

Sakata hilo lilifanikiwa baada ya askari hao kutii amri ya Naibu Spika huo kwa kutumia mabavu kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzani ambapo aliungwa mkono na wabunge  kutoka nje ya ukumbi na kususia kikao hicho.

Katika tukio hilo Mwenyekiti wa vyama vyenye wabunge wengi bungeni na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjari Agustino Mrema alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge wezake si cha kungwa na na kinaleta fedheha kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema yeye kutokutoka kwake nje haimaanishi kuwa ni kibaraka wa CCM na  si ndicho alichotumwa kufanya na wananchi wake,hivyo haungi mkono hata kidogo na haeleweke hivyo kuhusu msimamo wake.

"Hatoki mtu hapa nitakaa ndani ya bunge mpaka kieleweke na mnielewe kwamba mimi ndiye kiongozi wao vyama vyote tisa,hivyo nastahili kuheshimiwa na sikubaki humu ndani kwa sababu mimi ni kibaraka wa CCM bali  kinachopiganiwa ni maslahi ya taifa na ndicho nilichotumwa na wananchi wangu sikutumwa nije kutoka nje au kususia bunge."alisema Mrema.

Naye, Mbunge wa Same Mashariki na Bi Anne Kilango Malecella aliitaka Serikali kusimama imara na isiogope vitisho vinavyotolewa na wasioitakiwa mema nchi katika kupigania maslahi ya taifa.

Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wapinzani bungeni hakina nia njema katika kupata katiba mpya na wajumbe 156 waliopiga kura wanavigenzo vya kuweza kuchangia Mswaada huo kujadiliwa.

Vurugu za bunge hilo ziliaza toka awali katika kipindi cha muongozo wa Spika ambapo vijembe,kashifa kwa wabunge kuzungumza bila kufuata utaratibu ilimradhimu Naibu Spika Job Ndugai kusimama mara kwa mara kujaribu kurejesha utulivu katika matukio yaliyotawala Ukumbini humo.

Mara baada ya kutolewa mwongozo ulioombwa na wabunge juzi wakidai Muswada wa Mabadiliko ya rasimu ya katiba umeingizwa vipengele kinyemele, na Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu, wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na wale wa CCM walikuwa wakituhumiana kusema uongo kuhusiana na hatua hiyo ya uandaaji wa mchakato wa Rasimu wa Katiba mpya.

Hali hiyo ilipekea wabunge hao kuchambua vipengelee mbali mbali vya sheria vya kutafasili kanuni za bunge kwa wabunge ambao wanasema uongo bungeni ambapo msemaji wa Kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu alisema Kanuni ya 61 A inawataka wabunge kutotoa taarifa zisizo na ukweli bungeni huku kipengele 63 (3)kinamtaka mbunge mwingine anayeweza kusimama nakusema mbunge aliyesema kabla yake alisema uongo hivyo Tundu Lissu alisema mwenyekiti wa Katiba juzi alisema uongo kuwa wazanzibar wametoa maoni katika kamati ya katiba.

Lissu alisema yeye akiwa ni mmoja wa wanakamati waliambiwa kamati haiwezi kwenda zanzibar kwa sababu za kiusalama hivyo mwenyekiti huo amelidanganya bunge.

Muongozo huo ulipelekea Waziri Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Sera wa shughuli za Bunge William Lukuvi kutaka kiti cha Spika kichukue hatu zidi ya wanaotumia bunge ambalo ni chombo cha sheria kudanganya na fitirisha pamoja na kutumia jina la rais kwa dhihaka.

Alisema kuwa msemaji huyo wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu ameshawishi wabunge na wananchi kuamini uongo kuwa uteuzi wa rais katika uundwaji wa kamati ya maoni ya katiba amelenga watu anao wafahamu kwa maslahi yake na si kwa maslahi ya watanzania.

Lukuvi alifafanua kuwa uteuzi wa rais katika uundwaji wa tume hiyo umezingatia matakwa ya sheria kwa kushirikisha mapendekezo ya kila Sekta ikiwemo vyama vya hiari,walemavu,taasisi za dini,vyama vya maendeleo ya Jamii na vyama vya Siasa kikiwemo Chadema ambapo kati ya majina yaliyopendekezwa ni pamoja Tundu Lissu hakuchaguliwa kwa sababu hakuwa na sifa ya kumzidi Professa Baregu kati ya majina yaliyopendekwaza na Chama hicho.

Akiomba ufafanuzi muwasilisha wa mjadala huo bungeni Ally Hamisi Seif aliomba hoja ya kuondolewa kwa msaada huo wa sheria kwakua hakuna ushirikishwaji wa kutosha kwa wazanzibar katika mchakato wa kuandaa rasmu ya Katiba mpya kutokana na kamati kutokupokea maoni ya wananchi wa zanzibar.

Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freem Mbowe lililohoji kuwa msaada huo una maeneo makubwa yatakayoleta ufa nchini , hivyo yakafanyiwe malekebisho kabla ya mswaada wake kujadiliwa bungeni.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu swali hilo alisema  kuwa hakuna haja ya mswaada huo kuondolewa kwani kabla ya  kuletwa bungeni kulikuwa kunafursa kwenye kamati mbalimbali,na tofauti zilizopo zinazungumzika ili uweze kujadiliwa.

Naye, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia alishauri Serikali umuhimu wa majadiliano hayo kufanyika kwa uwazi kabla ya kisheria ili kusaidia maana halisi ya kuunda dola kwani kura ya maoni ya zanzibar inaeleza wazi mgogoro wa kikatiba uliopo ambapo ulipelekea hata mamlaka ya kugawa ardhi aliyonayo rais wa Tanzania hufanywa na rais wa zanzibar katika ardhi ya zanzibar.

Akijibu swali hilo  Pinda alisema hana tatizo na ushauri wa Mbatia ila ungekuwa na nafasi endapo katiba mpya isingekuwepo kwani ndiyo itakayofuta tofauti zilizopo.

Hata hivyo Sakata hilo liliaza Juzi jioni  wakati wabunge wa CHADEMA na CUF kuwa kitu kimoja na kuamua kutoka nje baada ya Tundu Lissu kuwsiliha maoni ya kambi hiyo huku akieleza kuwa wananchi wazanzibar hawakushirikishwa kwenye maoni ya rasmi ya katiba mpya.