Wednesday 4 September 2013

RAMOS ATOA YA MOYO WAKE KUHUSIANA OZIL


Beki kisiki wa Real Madrid, Sergio Ramos, ametoa ya moyoni kuhusiana na kuondoka kwa kiungo Mesut Ozil aliyejiunga na Arsenal.


Ramos amesema kama angekuwa ndiyo anayetoa uamuzi katika suala hilo, basi Ozil angebaki katika kikosi chao.



“Nasema wazi kuwa nimeumia kwa kuwa Ozil ni mtu mzuri, mchezaji hodari na rafiki yangu mkubwa. Sina la kuongeza kwa kuwa yeye na klabu wamefikia uamuzi.



“Namtakia kila la heri kwa uamuzi wake aliouchukua na nitaendelea kumkumbuka kama rafiki wa kweli,” alisema.


Pamoja na Ramos, wachezaji kadhaa wa Madrid walionyesha wazi kutofurahishwa na kuondoka kwa Ozil.


Mashabiki walipiga kelele wakati wa utambulisho wa Gareth Bale wakiusisitiza uongozi kufanya juhudi za kumbakiza kiungo huyo Mjerumani

0 comments: