Tuesday 3 September 2013

HOFU YA NJAANCHINI ZIMBABWE ZAIDI YA MILION MOJA NA NUSU WAKABILIWA NA NJAA



WFP linasema kuwa bei ya nafaka imepanda sana ikiwa moja ya sababu ya upungufu wa chakula

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa linasema kuwa zaidi ya watu milioni mbili nchini Zimbabwe wanakabiliwa na tisho la njaa katika miezi michache inayokuja.
Shirika hilo la , WFP, linasema kuwa mtu mmoja kati ya watu wanne katika maeneo ya vijijini wanahitaji msaada wa chakula.

Idadi hii ya watu wanaohitaji msaada inasemekana kuwa kubwa zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 2009 wakati ambapo zaidi ya nusu ya wananchi walihitaji msaada kama huo.

Tatizo hilo ni mbaya zaidi Kusini mwa Zimbabwe ambako mavuno hayakuwa mazuri mwaka huu.
WFP linasema kuwa tisho la uhaba wa chakula limesababishwa na hali mbaya ya anga , bei ghali ya nafaka na ukosefu wa mbegu za hali ya juu, mbolea na mahitaji mengine ya kilimo bora.

Ili kukabiliana na hali nchini Zimbabwe, shirika la WFP na washirika wake litaweza kutoa nafaka, mafuta na mboga kwa watakaokabiliwa na hali mbaya zaidi.

Mnamo mwaka 2012,kwa mara ya kwanza serikali ya Zimbabwe ilitoa mbegu za thamani ya dola milioni 10 kwa wakulima kutokana na mradi walioshirikiana nao na shirika la WFP na washirika wake wengine kwa wilaya 37.

Ili Kuwasaidia watu kukabiliana na njaa, shirika la WFP limekuwa likiendesha mpango wa kuwapa watu pesa badala ya chakula katika maeneo ya vijijini tangu mwezi Juni.
Chini ya mpango huu jamii ambazo zinakabiliwa na tisho kubwa zaidi hupokea chakula au pesa wakati wakijihusisha na miradi ya kusaidia jamii kama vile ujenzi wa mabwawa.

0 comments: