MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday 21 February 2016

Wakenya wagawanyika kuhusu ushindi wa Museveni


Museveni na KenyattaImage copyrightUhuru Kenyatta Facebook
Image captionRais Museveni na Rais Kenyatta mwezi Oktoba mwaka 2015
Muda mfupi baada ya Rais Yoweri Museveni kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Uganda, ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta akimpongeza kwa ushindi wake ulipakiwa kwenye kurasa zake Twitter na Facebook.
“Nina furaha sana kumpongeza Mtukufu Rais Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Uganda. Watu wa Uganda wamenena, na wamenena kwa uwazi. Tunaheshimu uamuzi wao wa Rais Museveni.”
Rais Kenyatta alisema Kenya inathamini sana urafiki wa karibu ambao umekuwepo na kwamba anatarajia urafiki huo pamoja na ushirikiano hasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki utaendelea.
“Namtakia Rais Museveni ufanisi anapoendelea kutumikia taifa lake kwa muhula mwingine. Yeye na Uganda wanaweza kutarajia uungaji mkono wangu, na urafiki kutoka kwangu, pamoja na kutoka kwa kaka na dada zao hapa Kenya.”
Lakini hatua hiyo haikuwafurahisha baadhi ya Wakenya mtandaoni na wengi waliandika wakimshutumu.
Saa chache baadaye, kitambulisha mada#UhuruIsNotKenyakikaanza kuvuma kwenye Twitter. Kwenye Facebook, wengi waliandika kumkosoa.
Wakosoaji wake wanasema Rais Kenyatta alimpongeza Rais Museveni yeye binafsi na si kwa niaba yao.
Wengine walishangaa ni kwa nini Rais Kenyatta akaharakisha kumpongeza Rais Museveni ilihali “alichukua muda kumpongeza Dkt John Magufuli” alipotangazwa mshindi Tanzania”.
Lakini kunao wanaosisitiza kwamba Rais Kenyatta ana haki ya kumpongeza Rais Museveni bila "kuomba ushauri kutoka kwa wananchi".
Wengine wanaamini Rais Museveni anawakilisha "Afrika huru".
Rais Museveni amekuwa mmoja wa watu wanaopinga sana kesi zilizowasilishwa dhidi ya viongozi wakuu wa Kenya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Kesi dhidi ya Rais Kenyatta iliondolewa lakini kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang inaendelea.
Rais Museveni amehudhuria sherehe kadha za kitaifa na kupewa muda wa kuwahutubia wananchi.

Bandari ya Tanga Yaamriwa Kurejesha Mita za Kupimia Mafuta


Serikali imetoa wiki moja kwa Mamlaka ya Usimamisi wa Bandari(TPA) mkoa wa Tanga kuhakikisha inarejesha tena matumizi ya mita ya kupimia mafuta (Flow Meters), kabla ya shehena ya meli ya mafuta kutia nanga bandarini hapo.

Hatua hiyo ya serikali inafuatia uamuzi wa TPA kuacha ufungaji wa mita hizo uliofanywa zaidi ya miaka mitano iliyopita ambapo kwa kipindi chote hicho serikali ilikuwa ikiingia hasara na kupoteza mapato.

Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Edwin Ngonyani wakati akizungumza katika majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku moja iliyolenga kuangalia mwenendo wa utendaji wa Bandari ya Tanga.

Katika ziara hiyo, pia Naibu Waziri alifanya ukaguzi wa Flow meters pamoja na matishari matatu ambayo yamedumu kwa zaidi ya miaka minne bila kufanya kazi bandarini hapo.

Mhandisi Ngonyani alisema serikali imesikia kwamba kufungwa kwa mita za kupimia mafuta(Flow Meters)kwenye bandari za hapa nchini kumetokana na ushiriki  wa baadhi ya wafanyakazi wa TPA waliokuwa wamelenga kunufaika kupitia wafanyabiashara wakubwa ambao kimsingi mita hizo zilikuwa zikiwabana katika ulipaji wa kodi.

Pia imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyakazi hao wanajihusisha kufanya uchochezi kwa wananchi ambao walitakiwa kupisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Mwambani, ambao licha ya kulipwa fidia lakini wameendelea kugoma kuachia ardhi hiyo.

“Uamuzi wa kuondoa Flow meters ulikuwa ni wa kipuuzi kabisa na tumesikia uchochezi huu pia ulihusisha baadhi ya wafanyakazi," alisema Ngonyani. "Inasikitisha sana kwani nia yao ilikuwa ni kuwanufaisha wafanyabiashara."

Alisema iwapo watumishi wa TPA wangekuwa na umoja katika kupigia kelele maamuzi yaliyofanywa kipindi hicho, ni dhahiri kuwa hali ya ukwepaji wa kodi kwenye shehena ya mafuta yanayoingia nchini isingefikia ilivyo sasa.

Alisisitiza kwamba serikali itawachukulia hatua za kisheria waliohusika na manunuzi ya matishari matatu kwenye Bandari ya Tanga ambayo hayakidhi vigezo vya kiutendaji.

Aidha, aliitaka Menejimenti ya mamlaka hiyo kupitia upya mkataba wa mzabuni aliyeagiza vifaa hivyo kuona kama wataweza kunusuru kiasi cha fedha zilizotumika.

“Kuna haja ya kuupitia upya mkataba wa mzabuni tuone kama kuna njia yoyote ya kuokoa zile fedha lakini bado tuendelee pia kuangalia namna ya haya matishari yatakavyotumika kwa njia mbadala.

"Kama alivyosema Waziri Mkuu (juzi) nasisitiza kwamba aliyehusika tutamshughulikia.”

Mhandisi Ngonyani alisisitiza kuwa wananchi wajenge imani na serikali ya awamu ya tano kwamba Bandari mpya ya Mwambani itajengwa na kamwe haitakuwa ndoto; hatua itakayoenda sambamba na ujenzi wa njia ya reli kutoka Tanga mpaka Musoma.

Awali, Kaimu Meneja wa TPA Mkoa wa Tanga, Kapteni Andrew Matillya alisema kwa wastani wa kila mwezi Meli ya moja ya shehena ya mafuta inapukuliwa bandarini hapo na kwamba utaratibu unaotumika kupima mafuta hayo si wa flow meters kwani ziliondolewa tangu mwaka 2011.

“Kila mwezi kuna wastani wa meli moja inapakua mafuta kwenye bandari hii lakini utaratibu unaotumika ni wa bye-pass kwa maana kwamba flow meters hazitumiki kupima kiasi cha mafuta kinachoingia nchini,” alisema.

Naye Mbunge wa Jimbo la Tanga, Mussa Mbaruku (CUF), aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa hatua mbalimbali inazochukua kama kurudisha matumizi ya Flow meters na ahadi ya ujenzi wa bandari ya Mwambani.

Alisema maamuzi hayo yanajenga matumaini mapya kwa wananchi wa Tanga ambao walishakata tamaa.

Hivi karibuni Serikali ilimsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Bandari, Bernadina Mwijarubi.
Mwijarubi ndiye anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.

Rafiki Yangu Ameniomba Nilale na Mume Wake Nipate Mimba Niwazalie Mtoto.....



Nina rafiki yangu lakini tunaishi nchi tofauti tunakutana mara 3-5 kwa mwaka hua mie nikienda nchi anayoishi anakuja kunitembelea na yeye akija ninakoishi anafikia kwangu.Yeye hajabahatika kupata mtoto mwaka wa 5 sasa tangu ameolewa, jana wakati tuna kula akaniomba tuonge kitu muhimu baada ya chakula, nikamwambia inshallah tutaongea.

Basi baada ya chakula na mambo mengine nikaenda kuwalaza watoto nikaenda chumbani kwake haya nimekuja tuongee, basi akanambia kama unavyojua sina mtoto na nimejaribu dawa zote unazozijua za kizungu na miti shamba sijafanikiwa kupata ujauzito sasa tumeshauriyana na mume wangu nikamwambia changua rafiki yangu yoyote mimi nitaongea nae ili atupatie mtoto.

Mie macho niliyatoa nakutetemeka juu, nikamwambia sijafahamu unamaanisha nini ukisema rafiki yako akupe mtoto je unataka nikupe mwanangu ule au vipi? Kasema NO nataka ulale na mumewangu nilimshangaa lakini sikutaka ahisi vibaya ilibidi nijikaze nikamwambia na ilikuwaje nikawa mie?

Kasema ndani ya moyo wangu nili wish mume wangu akuchague wewe na aliposema bora wewe ndio nikafurahi zaidi.Waungwana nilimpa maneno mengi yakumpa moyo lakini naomba nisema kua sijakubaliana na ombi lake na nimemwambia anisamehe sitoweza kufanya hicho kitu ila nitamsaidia kwa hali na mali.

Nitamuulizia kwa watu kama kuna tiba lakini kwa mimi siwezi na mumewe pia niliongea nae nikamwambia wanisamehe sitoweza, je nimekosea kuwakatalia?
Sijapenda lakini sina choice naipenda Family yangu sana na hata hili jambo silifikishi kwa Mr.

By Nimpendenani/JF...

Wata Watatu Watiwa Mbaroni Kwa Kuvamia Kituo Cha Polisi Na Kuvunja Mlango Ili Kuwatoa Wenzao



Watu watatu wamekamatwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuvamia Kituo cha Polisi cha Duthumi na kuvunja mlango kwa lengo la kuwatoa wenzao watatu wanaotuhumiwa kwa wizi wa mifugo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Graifton Mushi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12.40 jioni.

Alisema polisi walilazimika kutumia silaha za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao.

Mushi alitaja silaha hizo kuwa ni mapanga, shoka na marungu. Hata hivyo, alisema wakati watu hao wanavamia kituo hicho watuhumiwa hao walishaondolewa kituoni hapo na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati. Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Katika tukio jingine; watu zaidi ya 20 wa Kitongoji cha Mazizini Kijiji cha Maseye Wilaya ya Morogoro wamevamia eneo la mwekezaji Ayubu Mngimbwa na kuteketeza vibanda vilivyokuwa na vifaa mbalimbali vya uchimbaji wa madini na kumshambulia kwa vipigo.

Kaimu Kamanda huyo alisema thamani ya vibanda na vifaa vilivyoteketezwa bado haijafahamika.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati ya wananchi wa kitongoji hicho na mwekezaji anayedaiwa kutiririsha maji yenye kemikali za sumu.

ACT Wazalendo Chamvua Uanachama Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar Kwa Kuhudhuria Vikao Vya ZEC

 

Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.

Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.

Hatua hiyo dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya chama hicho kudai kuwa alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar, Khamis Iddi Lila kuwahujumu.

Awali, Lila alisimamishwa uanachama kwa madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha.

Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati maalumu ya Zanzibar imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya 22 (1) (2) (4).”

Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.

“Huku ni kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.

Vyama vilivyowachukulia hatua viongozi wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU), kilichomfukuza aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed Zonga, huku Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa mlezi wake, Hamad Rashid Mohamed

Saturday 20 February 2016

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu Atangaza Oparesheni Kamata Bodaboda Nchi Nzima


MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewaagiza makamanda wa Polisi kote nchini, kuendesha oparesheni kali ya kuwachukulia hatua za kisheria, waendesha bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani.

Ametaja makosa yatakayosababisha waendesha bodaboda hao kukamatwa kuwa ni pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu na kutovaa kofia ngumu.

IGP Mangu alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na maofisa wakuu wa Polisi, wakiwemo makamanda wa Polisi wa mikoa, vikosi na makao makuu katika kikao kazi kilichofanyika Dar es Salaam hivi karibuni ambacho kilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani, lakini sasa mwisho wao umefika na kuwataka makamanda wa Polisi wa mikoa kote nchini, kutekeleza maelekezo hayo, ili kuleta nidhamu kwa bodaboda katika kufuata sheria za usalama barabarani.

IGP Mangu alisema suala la kufuata sheria za usalama barabarani kwa bodaboda halina mjadala na kila Kamanda ahakikishe kuwa wote wasiofuata sheria na kukaidi, wanakamatwa bila kuoneana muhali kwa kuwa wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuzuilika.

“Pamoja na kuendelea kudhibiti uhalifu wa aina zote, natoa maelekezo kwa kila mkoa kuhakikisha unaendesha oparesheni kali dhidi ya bodaboda, ili kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda.

 “Wengi wao hawataki kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, tusiwaonee muhali maana maisha ya watu ni muhimu sana na jambo la msingi ni kusimamia sheria tu,” alisema IGP Mangu.

Awali akifungua kikaokazi hicho Waziri Kitwanga alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea na mapambano yake dhidi ya uhalifu na wahalifu, ili usalama wa raia na mali zao uendelee kuimarika na Watanzania waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila hofu ya kutendewa uhalifu.

ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO ZA LIGI KUU TANZANIA BARA

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Yanga imefuta rekodi ya kocha Jackson Mayanja ya ushindi mfululizo baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu hizo kwenye mchezo wa marudiano.
Ushindi huo ni wa pili kwa Yanga dhidi ya Simba ndani ya msimu huu wa 2025-16 baada ya awali kupata ushindi kama huo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma AbdulBeki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Bao la kwanza la Yanga limefungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 baada ya Hassan Kessy kutoa pasi fupi kwa golikipa wake Vicent Agban ambayo ilinaswa na mzimbabwe huyo na kuwekwa kambani mapema kipindi cha kwanza.
Yanga walipata bao la pili kutoka kwa nyota wa mchezaji wa zamani wa Simba Amis Tambwe dakika ya 72 kipindi cha pili.
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njanoAdbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Rekodi unazotakiwa kujua
  • Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba tangu iwe chini ya kocha Jackson Mayanja tangu kocha huyo atangazwe kuchukua mikoba ya Dylan Kerr.
  • Simba ilikuwa haijafungwa zaidi ya goli moja tangu iwe chini ya Mayanja, Yanga wamekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba zaidi ya goli moja baada ya kuifunga bao 2-0.
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya SimbaRaha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
  • Amis Tambwe ni mchezaji pekee katika msimu huu kuifunga timu yake ya zamani katika mechi mbili ndani ya msimu mmoja.
  • Amis Tambwe, Hamisi Kiiza na Ally Mustafa ni wachezaji ambao leo walikuwa wanacheza dhidi ya timu zao za zamani. Wachezaji hao wamewahi kucheza kwenye vilabu hivyo kwa nyakati tofauti kisha kuhamia kwenye upande pinzani.
  • Yanga inapanda kileleni mwa ligi kwa mara nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 45 baada ya michezo 20.
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanzaMashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
  • Yanga imeshinda kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa taifa baada ya mechi mbili za ugenini. Ilifungwa 2-0 na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga kabla ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons.
Mashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga
Mashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi YangaMashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga
  • Magoli ya mechi ya leo yamedungwa na wachezaji wa kigeni Donald Ngoma (Zimbabwe) na Amis Tambwe (Burundi).
  • Simba imefungwa na Yanga kwenye mechi zote (mbili) za msimu huu (2-0) 26 September, 2015, (2-0) 20 February, 2016.
Nini Kinafuata kwa timu hizo baada ya mchezo wa leo?
Simba itakuwa mwenyeji wa Mbeya City March 6, 2016 kwenye mchezo wao ujao wa VPL kwenye uwanja wa taifa.
Yanga wataialika Mtibwa Sugar kwenye mchezo unaofuata katika liga, mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa February 24, 2016.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja mbalimbali
Mgambo JKT 1-1 Tanzania Prisons
Stand United 1-1 JKT Ruvu
Mbeya City 0-3 Azam FC
Toto Africans 1-1 Kagera Sugar

Comments

Kutoka Kampala, mshindi wa kura za Urais Uganda 2016 ametangazwa..


Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali yalianza kutolewa kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa naYoweri Museveni ambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais toka mwaka 1986ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigye akikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.
KTN 2
Museveni 2
Rais Museveni alipokutana na Viongozi waangalizi wa uchaguzi Mzee Obasanjo na Banda nyumbani kwa Rais eneo la Rwakitura.