MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday 21 November 2015

Kauli ya Zitto Kabwe Kuhusu Wabunge wa UKAWA Kuitwa "Watoto" Bungeni

 

WAKATI Rais Magufuli akimpa heko Mbunge wa Kigoma Mjini Kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe kwa kitendo chake cha kutoungana na wabunge wanaowakilisha umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kupiga kelele na kutolewa nnje ya Bunge na Spika Job Ndugai,Zitto ameibuka na kuwaunga mkono wabunge hao.

Akizungumza nje ya bunge, muda mfupi mara baada ya bunge hilo kuhairishwa na Waziri Mkuu Mhe Kasimu Majaliwa,Zitto alisema kuwa hakuna haja ya kuwajadili wabunge hao kwa kuwa demokrasia inawapa haki ya kufanya hivyo.

Zitto ambaye alikuwa akizungumza na Shirika la Habari Tanzania’TBC’ alisema kuwa haoni sababua ya wabunge hao kuitwa wahuni au watoto kama walivyoitwa Bungeni kwa kuwa kufanya hivyo ilikuwa ni sehemu ya kuwasilisha hisia zao kwa walengwa.

Alisema kuwa binafsi hana muda wa kulijadili suala hilo kwa kuwa limeshapita na kinachotakiwa kwa sasa ni kufanya kazi iliyowapeleka bungeni.

Ukawa kuchanga Mil 33.9 kusaidia familia ya Mawazo

 

WABUNGE wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamepanga kuchanga Sh. 33.9 milioni kwa ajili ya kusaidia familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa Geita, Alfonce Mawazo.
   
 Fedha, hizo zimepatika baada ya wabunge 113 wa Ukawa kuchangishana kiasi Sh. 300,000 kila mmoja ambazo zitakabidhiwa familia ya Mawazo ambaye ameuawa kikatili na watu ambao mpaka sasa hawajabainishwa.

Mwenyekiti wa Chadema – Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe alisema hayo wakati akizungumza nasi mjini hapa Dodoma kuhusu maandalizi ya mazishi ya kada  huyo ambaye anatajwa kuwa shujaa katika mapambado ya kutafuta ukombozi Ukawa.

Mbowe amesema licha ya kwamba Mawazo alikuwa mwanachama wa Chadema lakini pia alishiriki vyema katika ukombozi ndani ya Ukawa kwa kutetea masilahi ya Watanzania kwenye mkoa wake wa Geita pamoja na mikoa mingine nchini.

“Kwa ujumla wetu wabunge takribani 113 tumekubaliana kuchanga kiasi cha Sh. 300,000 kila mmoja kwa ajili ya kuiwezesha familia yake ambayo ameiacha.

“Kumbuka kwamba Mawazo amepigania masilahi ya Watanzania wengi katika mkoa wake wa Geita lakini pia katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

“Hivyo tunalazimika kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wetu wa Ukawa na ikumbukwe kuwa, kwa sasa seriali ya CCM inaonesha wazi kutumia vyombo vyake vya dola kudidimiza upinzani,” amesema Mbowe.

Hata hivyo, Mbowe amesema inasikitisha kuona jeshi la polisi linavyotumiwa vibaya na kujikuta linafanya kazi za siasa badala ya kusimamia ulinzi na usalama wa raia.

“Leo (juzi), baada ya viongozi wa Mji wa Mwanza kupambana vikali na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, aliwaambia viongozi wa Chadema kuwa intelejensia imeonesha kuwa, iwapo watafanya mkusanyiko wa ibada kuna uwezekano wa kuzuka machafuko.

“Baada ya kupata taarifa hizo nilipata kuzungunza na IGP na kuniahaidi kunipatia majibu lakini hadi sasa sijafanikiwa kupata majibu lakini jambo lingine na la ajabu ni pale ambapo wamegeuza kibao na kusema hakuna kufanya ibada kwani kwa sasa kuna ugonjwa wa kipindupindu hivyo hakuna mkusanyiko,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema lazima Watanzania watambue kuwa serikali inatumia vibaya vyombo vyake vya dola kuzuia wapinzania wasifikishe ujumbe wao kwa jamii, imekifia hatua ya kuzuia hata watu kuwazika wafuasi wao.

“Sasa angalia kutuuwa wanatuuwa lakini hatua ya kutunyanyasa na kukataa hata tusimzike mtu wetu jambo hilo ni la ajabu sana lakini najua tutafikisha ujumbe kwa njia nyingine ambayo inafaa na kwa ustaarabu,” amesema Mbowe.

Baada ya agizo la rais magufuli hospital ya muhimbili yapokea vitanda 300 ,shuka 600 na baisikeli za wagonjwa


Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya Wabunge wapya zipelekwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya Wagonjwa wanaolala chini, limetekelezwa.
Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, baiskeli za kubebea Wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika hospitali ya taifa Muhimbili.
vitanda
Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vimefungwaJumapili ya November 22 2015 na kisha Rais mwenyewe atakwenda Hospitalini hapo Jumatatu ya November 23 2015 viwe vyote vimefungwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokosa vitanda.
Wadau mbalimbali walichangia kiasi cha shilingi milioni mia mbili ishirini na tano (225)kwa ajili ya kugharamia hafla ya Wabunge baada ya uzinduzi wa bunge la kumi na moja Dodoma lakini Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.

Full Time Man City Ya fungwa goli 4-1 na Liverpool leo November 21

4198
Uingereza ulipigwa mchezo kati ya Manchester City dhidi ya klabu ya Liverpool katika uwanja wa nyumbani wa Man City Etihad, mchezo kati ya Man City dhidi ya Liverpoolulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-1 na kuifanya Man Citykushuka kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Leceister City wanaoongoza Ligi kwa sasa kwa point 28 na Man United wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 27.
3184
Liverpool walianza kupata goli la kwanza dakika ya 8 baada ya mchezaji wa Man City Eliaquim Mangala kujifunga, goli la pili la Liverpool lilifungwa na  Philippe Coutinho dakika ya 23 wakati goli la tatu lilifungwa na Roberto Firmino dakika ya 32 kabla ya Martin Skirtel kuhitimisha kwa kufunga goli la nne dakika ya 81 huku Man Citywakiambulia goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Sergio Aguero dakika ya 44.
5184

Full Time Real Madrid yabigwa 4-0 na FC Barcelona leo november 21 Aangalia hapa

 Ligi Kuu Hispania imeendelea tena leo November 21 kwa kuzikutanisha timu kadhaa kucheza mechi zao za muendelezo wa Ligi Kuu Hispania, miongoni mwa mechi zilizochezwa November 21 ni mchezo wa watani wa jadi kati ya Real Madrid dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.

3334
Real Madrid na FC Barcelona kabla ya mchezo huu wa kihistoria kuchezwa walikuwa wamepishana kwa tofauti ya point tatu, Real Madrid wakiwa nyuma kwa kupoteza mchezo mmoja, huu ndio mchezo ambao kwa sasa una rekodi za kuangaliwa na watu wengi duniani. Licha ya kuwa Real Madrid wanaongoza kwa takwimu ya kumfunga FC Barcelona mara 92 kwa 89 hawakuweza kutamba katika uwanja wao wa nyumbani.
3600
Mchezo ulianza kwa FC Barcelona kupiga pasi nyingi kama kawaida yao na dakika ya 10 Luis Suarez akaanza kuwapa furaha mashabiki wa FC Barcelona duniani kote kwa kufunga goli la kwanza, wakati ambao Real Madrid wanajipanga namna ya kusawazisha goli hilo, Neymar akapachika goli la pili dakika ya 39 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.
3137
Kipindi cha pili kilianza kwa FC Barcelona kuendelea kumiliki mpira hadi dakika ya 52Andre Iniesta akapachika goli la tatu, FC Barcelona ambao dakika 4 baada ya Iniestakufunga goli la tatu walimuingiza Lionel Messi kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic ambaye alienda kuongeza nguvu na dakika ya 73 Luis Suarez akapachika goli la nne. Hadi dakika 90 zinamalizika FC Barcelona 4-0 Real Madrid.

Matukio ya ukatili yaongezeka kanda ya Kaskazini.

Matukio ya ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya Kaskazini yamezidi kuongezeka ambapo katika kipindi cha kuanzia mwenzi january mwaka huu jumla ya matukio 670 ya ubakaji yameripotiwa katika vyombo vya kisheria.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya kaskazini Afande Grace Lyimo na kusema kuwa matukio hayo yanaonekana kuongezeka kutokana na jamii kuwa na muamko wa kutoa taarifa hizo kwenye vyombo vya kisheria.
 
Amesema katika mkoa wa Kilimanjaro jumla ya  matuko ya makosa ya ubakaji yaliripotiwa katika kipindi cha januari hadi oktoba mwaka huu ni 164,mkoa wa  arusha ni 164,mkoa wa tanga ni 243 na mkoa wa Manyarani 99 hali ambayo ni tishio licha ya elimu ambayo imeendelea kutolewa katika jamii.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya Kaskazini meneja Progaramu wa shirika lisilo la kiserikali la kupambana na ukeketaji mkoawa Kilimanjaro (NAFGEM) Honorata Nasuwa amesema mila potofu,imani za kishirikina, ulevi,umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
 
Nao baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu mkoa wa Kilimanjaro wamesema hatua ya serika kutunga sheria ya matumzii ya mitandao ya kijamii imepunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya uzalilishwaji wa utu wa binadamu ikiwemo watoto na wanawake.
 

Umoja wa Wake za Mabalozi kukusanya Milioni 80 wakati wa gulio la mwaka huu jijini Dar es Salaam

.
Umoja wa Wake za Mabalozi  wa nchi za nje hapa nchini unatarajia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 80 wakati wa gulio la mwaka huu lililofanyika katika Shule ya Kimataifa Tanganyika jijini Dar es salaam.
Wake wa Mabalozi wa nchi za mbalimbali waliopo hapa nchini wanatarajia kukusanya kiasi hicho cha fedha kutokana na mauzo ya bidhaa mbalimbali zilizoletwa katika gulio la mwaka huu, na kutumia mapato hayo kugharamia miradi mbalimbali ya kuwakwamua wananchi wanaoishi katika mazingira duni.
 
Mgeni maalum katika hafla hiyo Bi.Jacquline Mengi amewapongeza Wake wa Mabalozi hao kwa kujitolea kwao muda na raslimali zao kwa ajili ya kuchangisha fedha za kugharimia miradi ya kuwakwamua wananchi wa Tanzania.
 
Mapema Mgeni Bi.Jacquiline Mengi alitembelea mabanda ya nchi mbalimbali  zilizoshiriki kuona  bidhaa za nchi hizo  zilizokuwa zinauzwa.
 
Mratibu wa hafla hiyo Bi. Geua Baunsgaard (Tamka Gewa baungad), na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyanchi wamesema Wake hao wa Mabalozi  wamekuwa wakifanya gulio kama hili kwa zaidi ya miaka 10 sasa ili  kukusanya fedha kwa ajili ya kugharimia miradi ya kuwasaidia watu wasiojiweza, ambapo kwa mwaka jana pekee kukusanya shilingi milioni 80.

ujangili waanza kupungua katika mbuga za wanyama za Tanzania

hali ya ujangili wa kutisha ambao ulitikisa nchi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika hifadhi za wanyamapori hapa nchini umeanza kupungua kwa kasi baada ya serikali kufanikiwa kudhibiti mianya iliyokuwa inatumiwa na majangili kuingia katika hifadhi za taifa .

Wanachama 115 wa CHADEMA na CUF Wahamia CCM Wilayani Handeni Mkoani Tanga


 

Wanachama 115 wa Chadema na CUF wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, wamejiunga na CCM kwa madai kuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeshindwa kuelewana hadi kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Wakirudisha kadi na bendera juzi mbele ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Mathew Mganga walisema walikuwa na nia ya kweli ya kuunga mkono Ukawa unaoundwa na vyama vyao lakini kutokana na kutokuwa na msimamo wameamua kuhama.

Katibu wa Chadema Kata ya Kwenjugo, Rajabu Vuli, alisema alifanya hamasa kuhakikisha chama chao kinapata ushindi lakini viongozi wa wilaya hawakuonyesha ushirikiano na watu wa chini.

Mwingine aliyehama ni Katibu wa Vijana wa Chadema wa kata hiyo, Ramadhani Dawa.

Dawa alisema ahadi zisizotimia za viongozi ikiwamo kuwadharau viongozi wa kata ndiyo sababu kubwa iliyosababisha kuhamia CCM.

Alisema kama wasingedharauliwa na mawazo yao kufanyiwa kazi wangebaki Chadema na kukiendeleza chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mvuto mkubwa na Watanzania ambao walitaka kuleta mabadiliko ya kweli.

Mganga alisema wamepokea wanachama hao bila wasiwasi kwani tayari hizo ni kura.

Hivi sasa chama hicho kipo kwenye kampeni za kumuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Handeni Mjini (CCM), Omari Kigoda.

Alisema wameridhika na uamuzi wa wanachama hao wapya kwa kuona CCM inajali ngazi zote za uongozi kuanzia wa chini hadi juu.

Alisema baada ya uchaguzi huo mdogo, watahakikisha yale walioahidi kwa wananchi yanafanyiwa kazi haraka hasa yanayowagusa moja kwa moja ikiwamo elimu, afya, maji na masuala ya miundombinu.

Mgombea ubunge huyo, aliahidi endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, atawaleta maendeleo.
 

UKAWA waweka hadharani Kilichowafanya Walete Vurugu bungeni



UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema mipango yao ya kutomruhusu Rais Dk. John Magufuli kulihutubia Bunge akiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, imefanikiwa.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Freeman Mbowe, alisema  jana kuwa walimua kuzuia Rais Magufuli asihutubie Bunge kwa vile Dk. Shein, muda wake wa kuwa rais ulikwisha tangu Novemba 2 mwaka huu kwa hiyo hakustahili kuhudhuria Bunge hilo.

Alisema kuwa waliamua kufanya vile wakiamini kuwa ilikuwa sehemu muafaka ya kufikisha kilio chao kutokana na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano ule, wakitokea katika nchi za jumuiya ya kimataifa.

“Tulishangaa kumuona Dk. Shein, Pandu Amiri Kificho na Makamu wa Pili wa Rais wakiwa ndani ya Bunge wakati kikatiba hawana uhalali,”alisema Mbowe.

Alisema, baada ya kitendo kile hivi sasa umoja wa vyama hivyo, unatarajia kukutana ili kupeana mikakati ya kuendeleza mapambano ya ndani na nje ya nchi ya kudai haki.

“Uchaguzi wa Zanzibar hauwezi kutenganishwa kikatiba au kisiasa na uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya muungano,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema Ukawa hawako tayari kuinajisi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu viongozi wasio halali kuingia bungeni.

Aidha, Mbowe alisema walitaka shughuli ya ufunguzi rasmi wa Bunge isitishwe kwa sasa na kuahirishwa hadi hapo Rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, atakapotangazwa rasmi na kuapishwa.

Naye Mwenyekiti Mwenza, James Mbatia, alisema haijawahi kutokea katika historia ya Bunge tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kwa vyombo vya dola kuingia ndani ya bunge na kuwatoa wabunge kwa nguvu.

“Wakati sisi tunatafuta majadiliano mezani ilikumaliza mgogoro huu wenzetu Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameamua kutumia majeshi kukandamiza demokrasia,” alisema Mbatia.

Mbatia alisema kuwa hawatakaa kimya bali wataendelea kupigania matakwa ya wananchi hususan kwa upande wa Zanzibara.

“Kuna mambo mengi yanafanywa hovyo na CCM na wapinzani wamekuwa wakivumilia kwa sababu ya kumpenda mama Tanzania lakini hivi sasa wasijaribu kuharibu amani, utulivu na mshikamano uliopo,” alisema.

Mbatia, alisema kwa kawaida mtu anapodhulumiwa haki yake kila mara matokeo yake anachoka kwa hiyo kuna siku ataifuta haki yake hata kwa kusababisha kumwaga damu.

Naye Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa ) wamesikitishwa na kitendo cha serikali ya CCM kuonesha wazi jinsi walivyobaka na kuikanyaga demokrasia nchini.

Alitoa kauli hiyo aipokuwa akizungumza na mwandishi wetu muda mfupi baada ya kutoka bungeni baada ya kufukuzwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya wabunge wa umoja huo kupinga kitendo cha kuruhusiwa kwa Rais wa Zanzibar kuwa sehemu ya Bunge.

Lissu alisema imeonesha wazi kuwa serikali ya CCM ilivyo kuwa ikitumia mabavu ya kuvunja sheria waziwazi sambamba na kuvunja kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari kwa afya ya nchi.

Akizungumzia kutoka kwao nje ya ukumbi wa Bunge alisema serikali ya CCM kwa kutumia kiti cha Spika walionekana kupanga mbinu chafu za kuwazima wabunge wa Ukawa ili wasiweze kufikisha hoja zao mbele za wananchi kupitia bunge hilo.

“Unaweza kuona kwamba serikali ya CCM inavyoweza kuvitumia vibaya vyombo vya dola, kwa utaratibu jinsi ulivyo ili kuruhusu watu waingie katika ukumbi wa bunge ni lazima kutengua kanuni ili watu waeze kuingia lakini kutokana na uovyo na ujinga mkubwa wa serikali ya CCM, ambayo haizingatii sheria na katiba imeweza kuleta askari wengi pamoja na majeshi kwa ajili ya kukabiliana na upinzani.

“Jambo kubwa na baya zaidi na la ajabu ni pale ambapo askali waliovaa magwanda ya polisi na jeshi wakiwa na silaha za moto walivyoweza kuingia katika ukumbi wa bunge kwa misingi ya kutaka kukabiliana na wabunge wa upinzani.

“Jambo hapa ni kwamba hata wao wanajua kuwa Dk. Shein siyo rais halali wa Zanziba lakini kwa ubishi wao wanalazimisha kufanya hivyo na kutokana na hali hiyo ndiyo maana serikali imekuwa ikitumia vyombo vya dola kwa ajili ya kuthibiti wabunge wa Upinzania ambao wametumwa na Umma wasitoe mawazo yao,” amesema Lissu.

Mbali na hilo alisema pamoja na kuwa walizuiliwa kuendelea na bunge, kwa ajili ya kuwasilisha hoja zao kwa watanzania lakini watatumia mbinu nyingi za kufikisha ujumbe kwa jamii kwani kwa sasa kuna kila mikakati ya kuhakikisha wanataka kuuzima upinzani.

Akizungumzia kuhusu kanuni za bunge kwa sasa alisema kama ilivyo katiba ya sasa ilivyo na makosa kibao ndivyo na kanuni za bunge zinavyotakiwa kurekebishwa kwani kuna makosa mengi zaidi.

Kwa upande wao wabunge wa Zanzibar walisema ni dhambi kubwa kwa Dk. Ali Mohamed Shein kuenedelea kung’ang’ania kukaa madarakani wakati muda wake umeisha jambo ambalo linaonesha wazi kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka na dola yake.

“Inasikisha zaidi kuona jinsi Rais wa Zanzibar alivyokuwa siyo muungwana anajua kabisa kwamba hakushinda uchaguzi, lakini ikumbukwe wakati wa kuvunja baraza la wawakirishi wabunge wa CCM walimkataa Maalim Seif Shariff Hamad kama makamu wa kwanza wa rais asiingie katika bunge.

“Lakini kwa uungwana wa kiongozi huyo aliondoka wala hakuhudhuria kikao hicho lakini jambo la kushangaza huyu Dk. Shein amekomaa sasa inafikia hatua anazomewa bila kuwa na aibu sasa huo ni uongozi gani na anamuongoza nani,” amesema.

“Tunamuuliza Rais Magufuli, ni nani akapeleka vifaru na kuongeza askari wengi katika nchi za Zanzibar na ni kwa sababu gani.

“Kwa sasa hali ya Zanzibar si shwali kwani kila jambo sasa limelala kwani hata watalii hawaji kama ilivyokuwa mwanzo, mbali na hilo kuna hali ya sitofahamu ni kwani nguvu nyingi ya vyombo vya dola inaelekezwa Zanzibar,” alisema mmoja wa wabunge wa Zanzibar.

WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUSAFIRISHA MATENGA YA DAWA ZA KULEVYA MOROGORO

  Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kusafirisha matenga nane ya Dawa za kulevya yenye uzito wa kilogramu 120 yaliyokuwa yakisafirishwa kutoka mkoani Singida kwenda jijini Dar es Salamu kwa ajili ya kusambazwa kwa Mawakala.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonardi Paulo amesema tukio hilo limetokea Novemba 21 saa tisa usiku eneo la mikese mizani wakati polisi wakiwa katika opersheni maalumu katika barabara ya Morogoro Dar es Salaam ambapo ameseama watuhumiwa wanahojiwa na Polisi na kwamba baada ya upelelezi kukamili watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
 
 

MATOKEO YA LIGI KUU YA ENGLAND LICHA YA KUSHINDA MORINHO ASEMA ANAUHITAJI WA KUSAJIRI

 
 Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amesema
kuwa hana haki ya kuishinikza Chelsea kununua
wachezaji wapya wakati wa dirisha la uhamisho
mnamo mwezi Januari.
Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wamepoteza
mechi 12 kufikia sasa na wako katika nafasi ya
16 katika jedwali la ligi.
''Ningependa sana kuwa na wachezaji nilio
nao.Nafurahia wachezaji nilio nao, nawaamini
wachezaji hawa'',alisema Mourinho.
Chelsea itaialika Norwich nyumbani katika uwanja
wa darajani siku ya jumamosi.Chelsea
inahusishwa na uhamisho wa nyota wa klabu ya
Barcelona Lionel Messi na kiungo wa kati wa
Juventus Paul Pogba mnamo mwezi Januari.
Hatahivyo,Mourinho anataka wachezaji alio nao
kuiondoa klabu hiyo katika nafasi waliopo sasa.

Matokeo ya Burundi Vs Zanzibar Heroes CECAFA Challenge 2015 …


Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameanza leo November 21 mjini Addis Ababa Ethiopia, ikiwa ni michezo miwili ilikuwa inatarajia kuchezwa leo November 21, timu ya Zanzibar Heroes dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ndio zilikuwa timu za kwanza kufungua dimba kabla ya wenyeji Ethiopia watakaocheza dhidi ya Rwanda.

Burundi ambao walikuwa na nyota wao kadhaa akiwemo Didier Kavumbagu anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya Tanzania walikuwa wakiutawala mchezo kwa wastani kumiliki mpira kwa asilimia 56 katika kipindi cha kwanza wakati Zanzibar walikuwa na asilimia 44 za umiliki wa mpira kwa dakika zote 45 za kwanza.


Mchezo huo ambao Burundi walikuwa wakifika sana langoni kwa Zanzibar Heroes hadi wanaenda mapumziko walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 38. Licha ya kipindi cha pili Zanzibar kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo haikuwezekana.

Maguri Auzwa TP Mazembe Kwa Sh Mil 100


Na Sweetbert Lukonge

STAND United imekubali kumuuza straika wake Elias Maguri kwa TP Mazembe ya DR Congo kwa dau la dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 100.
Timu hiyo imetoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zinazomhusisha Maguri kujiunga na Yanga na TP Mazembe na sasa ipo tayari kumuachia straika huyo mwenye mabao 10 msimu huu.

Maguri ambaye yupo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars kinachoshiriki Kombe la Chalenji huko Ethiopia, amefunga mabao tisa katika Ligi Kuu Bara, pia ana bao moja kwa timu ya taifa alililoifungia Taifa Stars dhidi ya Algeria katika sare ya mabao 2-2 Novemba 14, mwaka huu.
Ofisa Habari wa Stand United, Deokaji  Makomba, ameliambia gazeti la Championi Jumamosi kuwa, klabu yake imekubali kumuuza Maguri kwa dola 50,000 kwa TP Mzembe au timu nyingine ya nje ya nchi inayomtaka.

“Tupo tayari kumuachia Maguri ajiunge na TP Mazembe kwa dau la dola 50,000, kilichobaki sasa ni kufuatwa kwa taratibu za klabu na klabu ili mchezaji aweze kwenda DR Congo.
“Hii si kwa TP Mazembe pekee, timu yoyote ya nje ya nchi inayomtaka Maguri ijue hilo ndilo dau lake lakini kwa timu ya hapa nchini, inatakiwa kulipa Sh milioni 50 ili tuwaachie Maguri,” alisema Makomba.

Yanga ndiyo klabu pekee ya Tanzania iliyotajwa kumuwania Maguri na hata mchezaji mwenyewe aliwahi kunukuliwa kuwa tayari kuichezea timu hiyo badala ya Simba ambayo aliachana nayo hivi karibuni.
Hata hivyo, Maguri ameliambia gazeti hili: “Nilizungumza na Yanga kuhusu kujiunga nayo lakini sasa nimebadili mawazo na akili yangu yote ipo kwa TP Mazembe, nataka kufika mbali zaidi.
“Hata kama Yanga watakuja na dau kubwa kushinda Mazembe, nitaichagua timu hiyo ya DR Congo.”

Friday 20 November 2015

Hamad Ndikumana atemwa Rasimi na stend united ya shinyanga


Mwanasoka wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda na klabu ya Rayon Sports yaRwanda Hamad Ndikumana amerudi tena katika headlines za soka November 20,Ndikumana ambaye ni mume wa muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ametemwa na klabu yake ya Stand United baada ya kocha wa timu hiyo mfaransa Patrick Liewigkutohitaji huduma yake.
a1
Ndikumana ambaye alikuwa na klabu ya Stand United ya Shinyanga kwa kipindi cha miezi minne ametemwa rasmi na klabu hiyo, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru, awaliNdikumana aliwahi kugoma kuichezea klabu hiyo baada ya kutomaliziwa malipo yake lakini msemaji wa Stand United ya Shinyanga Deokaji Makomba amethibitisha kuwa moja kati ya sababu zilizofanya wamuache staa huyo ni umri wake kuwa mkubwa.
Manchester City's Brazilian forward Elano (L) fights for the ball with AC Omonia's Rwandan defender Hamad Ndikumana during their UEFA Cup first round, second leg football match at the City of Manchester stadium, Manchester, north-west England, on October 2, 2008.  AFP PHOTO/ANDREW YATES (Photo credit should read ANDREW YATES/AFP/Getty Images)
Elano wa Man City akiwania mpira na Hamad Ndikumana wakati akiichezea AC Omonia hii ilikuwa ni moja kati ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Kocha amesema hatomuhitaji tena katika kikosi chake sababu kubwa ilitajwa na mwalimu ya kumuacha Hamad Ndikumana ni kuwa na umri mkubwa hivyo mwalimu kaona aachane nae kwani itakuwa ngumu kuendelea nae, Hamad Ndikumana hatupo nae tena na tayari ameshakamilishiwa haki zake” >>> Deokaji Makomba
Ndikumana ambaye amewahi kutamba na vilabu kadhaa anatajwa kuwa na umri wa miaka 37, umri ambao ni mkubwa kisoka, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ndikumanandio jamaa ambaye alimuoa mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo Irene Uwoyana kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume anaitwa Krish.