Saturday 21 November 2015

Umoja wa Wake za Mabalozi kukusanya Milioni 80 wakati wa gulio la mwaka huu jijini Dar es Salaam

.
Umoja wa Wake za Mabalozi  wa nchi za nje hapa nchini unatarajia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 80 wakati wa gulio la mwaka huu lililofanyika katika Shule ya Kimataifa Tanganyika jijini Dar es salaam.
Wake wa Mabalozi wa nchi za mbalimbali waliopo hapa nchini wanatarajia kukusanya kiasi hicho cha fedha kutokana na mauzo ya bidhaa mbalimbali zilizoletwa katika gulio la mwaka huu, na kutumia mapato hayo kugharamia miradi mbalimbali ya kuwakwamua wananchi wanaoishi katika mazingira duni.
 
Mgeni maalum katika hafla hiyo Bi.Jacquline Mengi amewapongeza Wake wa Mabalozi hao kwa kujitolea kwao muda na raslimali zao kwa ajili ya kuchangisha fedha za kugharimia miradi ya kuwakwamua wananchi wa Tanzania.
 
Mapema Mgeni Bi.Jacquiline Mengi alitembelea mabanda ya nchi mbalimbali  zilizoshiriki kuona  bidhaa za nchi hizo  zilizokuwa zinauzwa.
 
Mratibu wa hafla hiyo Bi. Geua Baunsgaard (Tamka Gewa baungad), na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyanchi wamesema Wake hao wa Mabalozi  wamekuwa wakifanya gulio kama hili kwa zaidi ya miaka 10 sasa ili  kukusanya fedha kwa ajili ya kugharimia miradi ya kuwasaidia watu wasiojiweza, ambapo kwa mwaka jana pekee kukusanya shilingi milioni 80.

0 comments: