Monday 16 November 2015

Zitto Kabwe Atoa Kauli Nzito Kuhusu Uchaguzi wa Spika wa Bunge.....



Ameandika Maneno haya Kwenye Ukurasa wake wa Facebook:

|Hata Nyerere hakuwahi kujaribu kuleta Spika wake au Naibu Spika wake mfukoni. Alipomteua Chief Adam Sapi Mkwawa kuwa Waziri alifanyiwa rebellion na wabunge ( wakati wa chama kimoja) akamrudisha mpaka alipostaafu tena kwa kumtungia sheria ya ustaafu ( wakati wa Mwinyi) . Unapoona Rais anajaribu ku impose Kiongozi wa Bunge anayemtaka mjue huko mbele Bunge litafanywa kibogoyo. Kwa mfano, hakuna Naibu Spika yeyote katika nchi hii ambaye hakuwahi kuwa Mbunge wa Jimbo. Nawakumbusha tu kwamba; Bunge huendeshwa kwa kutumia Katiba, Sheria, Kanuni na DESTURI au maamuzi yaliyokwishafanywa. Underline DESTURI" Zitto Kabwe

0 comments: