Monday 16 November 2015

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Atengua Uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na kumteua kuwa Mbunge.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo asubuhi ametengua uteuzi wa Naibu Mwanasheria Mkuu Dr Tulia Ackson, Mwansasu na kumteua kuwa Mbunge.

Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene, amethibitisha kutenguliwa na kuteuliwa kwa Dk. Tulia.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila, amekiri kupokea taarifa ya uteuzi wa Dk. Tulia mapema leo asubuhi.

Awali kabla ya uteuzi huo, Dr Tulia alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo pia hapo jana Novemba 15, 2015 alikuwa ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.

0 comments: