Monday 16 November 2015

WATANZANIA INAKUJE MAGARI YA WASHAWASAHA YANAPATIKANA WAKATI MRI na CT-Scan ZINASHINDWA KUFANYA KAZI MPAKA HUDUMA ZINASITISHWA TUTA FIKA

 


Leo hospitali ya taifa ya Muhimbili imesitisha matumizi ya mashine za MRI na CT-Scan baada ya kupata hitilafu kwa mara nyingine.

Hii inatokea siku chache baada ya taarifa kutolewa kuwa mashine hizo zilitengamaa na tayari kutumika baada ya kupata hitilafu kwa muda wa miezi miwili iliyopita.
 
SOMA HII

Sisi ni taifaTaifa la Watu wajinga mno duniani!vipimo viwili vya ct scanner na MRI kutotengenezwa na Kampuni ya Phillips ni kutokana na kutolipwa deni lake kuvifanyia ukarabati vipimo hivyo ambalo limefikia bil. 7. juzi wamelipwa bil. 3 ili kikafanyiwa matengenezo. Kwa maana hiyo serikali bado inadaiwa bil.4.
Tanzania inamashine hii katika hospitali moja tu ya muhimbili kati ya hospitali zote za serikali nchini, hiki ni kichekesho na tena aibu! Hapa marekani vipo Kati ya 7000 na 10,000 kabla ya mwaka 2014!Google Kama unabisha!Wakija wanashindwa hata kukopa Au kuomba msaada Kweli ?
Kwa mujibu wa kampuni ya Phillips, moja ya makampuni yanayotengeza hivi vipimo, bei ya hivi vipimo ni kati ya USD 150,000 - 250,000 yaani sh. Mil 300 _ 500 za kitanzania kwa ct scanner ya slice 16 na USD 250,000 - 300,000 yaani Tsh. Mil. 500 - mil 600. Kwa ct scanner ya slice 64. Na gharama za kuifunga pamoja na mafunzo ni tsh mil. 200.
Kipimo cha MRI chenyewe huuzwa kwa USD 400,000 ambazo ni sawa na tsh mil. 840. Na gharama za mafunzo na kuifunga ni tsh. Mil. 300.
Kwa mujibu wa deni wanalodai hao Phillips la matengenezo tu tz ingeweza kununua mashine mbili za mri na ct scanner tatu.
Tarehe 20 october kabla ya uchaguzi aliyekua rais ( mpumbavu na mjinga kuliko wote niliowahi shuhudia ) alipokea magari mapya ya washawasha 399, ambayo ni miongoni mwa magari 777 ambayo serikali imeyaagiza kwa ajili ya uchaguzi, ambayo hayakutumika hata magari 50. Hapa ndio pakujiuliza magari yote 777 yalikuwa ma umuhimu gani!
gari moja la washawasha(Riot control vehicle) lenye uwezo wa kubeba little 11500 za cinamon water(maji ya kuwasha), linauzwa kwa USD 250,000 - 400,000. Ambazo ni sawa na tsh mil 500 - 800!
Kwa maana hiyo gari ya washawasha moja na mashine ya mri moja bei hazitofautiani. Kwa maana hiyo yangepunguzwa magari 50 tu, serikali ingeweza kuzifunga mashine za mri na ct scanner katika hospitali zote za rufaaa/mikoani
Tunacheza na kitu kinaitwa maendeleo! Acha kabisa! Waone wamevaa mashati ya vitenge ,viatu vya mokasini na degree za kwenye makaratasi lkn hawana cha Maana wanacho-deriver!tuliwafuga wenyewe hivyo tusilalamike Pia!
Ndio maana shabikia na kuchekea na tukaishia kuchagua viwanda hewa, Barabara za chini ya viwango na madaraja yanayo bomoka na mvua za kiangazi, NA kuancha Vipaombelele Elimu, Elimu, Elimu.
Tutaisoma numbe kweli maana kwa watanzania hapo kazi tuu.

CHANZO: 
UKAWA Northwest Washington STATE


0 comments: