Friday 6 November 2015

HII NDYO TATHIMINI YA CHEDEMA/UKAWA BAADA YA LOWASA KUINGIA CHADEMA ANGALIA HAPA

 
LOWASSA ni "Asset  

-Kabla ya ujio wa Lowassa ndani ya chadema, chadema ilikuwa na majimbo 23 tu na viti maalumu 26 na kuwa na wabunge 49 ktk bunge la 10 la 2010-2015, ujio wa Lowassa umeongeza wabunge kutoka majimbo 23 mwaka 2010 hadi majimbo 35 mwaka 2015 na viti maalumu kutoka 26 hadi 43 na kufanya jumla ya wabunge wa chadema 78 ktk bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na chama cha upinzani tangu Tanzania ipate uhuru,
-Kabla kuondoka kwa Lowassa ndani ya ccm, ccm ilikuwa na wabunge wa viti maalumu 79 mwaka 2010, sasa ccm itakuwa viti maalumu 62 tu kwa maana hiyo nguvu ya Lowassa imeondoka na viti maalum 17 ambao wote imebidi wapewe chadema, na ndiyo maana sasa chadema itakuwa na viti maalumu 43, which means, chukua viti 26 vya cdm 2010 + viti 17 alivyokuja navyo Lowassa = 43,

-Mwaka 2010-2015, ccm ilikuwa inapokea ruzuku zaidi ya 78% ya ruzuku yote ya vyama vya siasa kutokana na kura za urais alizopata JK, mwaka huu ccm itapokea ruzuku isiyozidi 59% ya ruzuku yote ya vyama ni sawa pungufu ya 20% waliyopoteza ccm, Na kwa mara ya kwanza chama cha upinzani chadema kitapokea 40% ya ruzuku yote ya vya siasa, hii ni kutokana na kura mil 6=39% alizopata Mhe. Lowassa.

-Kabla ya ujio wa Lowassa, katika majiji matano (5), Mbeya, Dar, Tanga, Mwanza & Arusha, cdm ilikuwa haiongozi hata jiji moja kati ya hayo kwa mwaka 2010-2015, yote yalikuwa chini ya ccm, Ujio wa Lowassa umeifanya chadema kuongoza majiji 4 (Mbeya, Dar, Arusha & Tanga japo Tanga itakuwa chini ya UKAWA) kutokana na ushindi wa madiwani wake ktk majiji hayo na ccm imebaki na jiji la Mwanza pekee, which means ccm imepoteza majiji 4 kutokana na kuondoka kwa Lowassa.

-Mwaka 2010-2015 chadema ilikuwa inaongoza halimashauri 5 nchi nzima mfano: Moshi & Karatu, mwaka 2015 kwa mara ya kwanza chadema itakuwa inaongoza halimashauri 30 Tanzania hii ni kutokana na Ushindi wa madiwani na wabunge ktk halimashauri husika.



NB: Kwa mtu wa kawaida na anayefikiria ya leo bila kujua kesho itakuwaje alibeza ujio wa Lowassa ndani ya chadema, lakini kwa anayefikiria leo na kesho na kuangalia kwa jicho la tatu atakuwa amegundua umuhimu wa ujio wa Mhe. EDWARD LOWASSA.

Ahsante...!!!

0 comments: