MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday 16 March 2014

ALIBINO ATIWA MBARONI KWA KUMCHUNA NGOZI MTOTO SEHEMU YAKE YA SIRI

DSC001791
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA mkazi wa kijiji cha Nkalankala kata ya Mwanga,tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) ,Hidaya Omari (20),anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumnyonga hadi kufa, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka moja na nusu,na kisha kumchuna ngozi katika sehemu yake ya siri.
Mtoto aliyenyongwa na kuchunwa ngozi ya sehemu yake  ya siri na kutupwa kwenye kisima cha maji chenye kina cha mita moja,ni Richard Paulo.
Imedaiwa pia mama yake mzazi na mtuhumiwa Hidaya,Neema Paulo (35), naye anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuhusika  kumnyonga Daudi Richard na kumsababishia kifo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida,SACP,Geofrey Kamwela,alisema tukio hilo la kusikitisha,limetokea machi 13 mwaka huu saa moja na nusu asubuhi huko katika kijiji cha Nkalankala wilayani Mkalama.
Alisema mtoto huyo Daudi,aliokotwa akiwa anaelea juu ya maji ya kisima chenye urefu wa mita moja.
Kamwela alisema uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi,umebaini kuwa Daudi (marehemu) aliuawa na kuchunwa ngozi yake na kutumbukizwa katika kisima hicho.
Alisema mwili wa marehemu ulipofanyiwa uchunguzi na daktari katika eneo la tukio na kubaini kuwa kabla ya mauaji jhayo,mtoto huyo alinyongwa shingo yake.Chanzo cha mauaji hayo,inasadikiwa kuwa ni imani ya kishirikina.
Kamanda Kamwela alisema mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa mtu na mama yake,watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.

MOTO WATEKETEZA NYUMBA ZA POLISI TANGA


moto_24117.jpg
Nyumba za Askari wa jeshi la polisi zilizopo eneo la chumbageni nyuma ya kituo cha polisi kikuu cha chumbani jijini Tanga zaungua moto.
moto2_6ee0c.jpg
moto3_335a7.jpg
(J M)
moto4_d2b1b.jpg
mhe_71664.jpg
Mh.Halima Dendegu akishuhudia ajali ya moto katika nyumba za polisi chumbageni,jijini Tanga hapo jana

MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBU WALIPONGEZA BUNGE LA KATIBA KUONYESHA USAWA WA JINSIA

 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao akizungumza.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP
Na Thehabari.com
MTANDAO wa Wanawake na Katiba wenye mashirika zaidi ya 50 yanayotetea haki za wanawake katika Katiba mpya, umelipongeza mchakato na matokeo ya  uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Bunge Maalum la Katiba (Mwenyekiti na Makamu wake) ambao umezingatia usawa wa jinsia.
Kauli hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Lilian Liundi wa TGNP Mtandao kwa niaba ya Mtandao wa Wanawake na Katiba jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa licha ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Mwaka 2012 haikuanisha kuwa uchaguzi wa uongozi wa Bunge hili uzingatie usawa wa jinsia bunge hilo limeona umuhimu huo.
“…Tumetambua busara na hekima za wajumbe za kuonyesha nia ya kujenga msingi wa usawa wa jinsia katika uongozi na vyombo vya maamuzi nchini. Kwetu sisi, hili si suala la uwepo wa mwanamume na mwanamke katika uenyeketi  wa Bunge Maalumu tu, bali pia ni ukomavu wa kipekee wa wajumbe katika kuuona ukweli kuwa suala la kuimarisha sauti za wanawake na wanaume ni nyeti sana, haswa wakati wa ujenzi wa maridhiano muhimu kikatiba,” alisema Liundi.
“Tunawapongeza waliochaguliwa ambao ni Mhe. Samweli Sitta (Mwenyekiti) na Mhe.  Samia Hassan Suluhu (Makamu Mwenyekiti) kwa kuaminiwa katika nyadhifa hizo muhimu.  Mtandao wa Wanawake na Katiba  unatambua uwezo wao katika utendaji na una matumaini makubwa kuwa pamoja na mengine mengi watakayoyasimamia, watatoa uongozi ulio imara na wenye weledi wakati wakiongoza Bunge hili katika kujadili na kupitisha misingi muhimu itakoyopelekea katika ujenzi wa usawa wa kijinsia nchini.”
Alisema mtandao huo unategemea kuona usawa wa jinsia ndani ya Katiba mpya, ambao sio ule tu wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika  ngazi mbalimbali, lakini pia usawa ulio na nia ya kujenga misingi ya kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi walio wengi na haswa wanawake nchini.
“…Kwa mtazamo huu, tunatarajia kuwa busara za Wenyeviti hawa na washauri wao zitatumika pia kuzingatia usawa wa kijinsia  katika Kamati zitakozoundwa pamoja na kuwa kuzingatia ustadi na uzoefu wa wanakamati unahitajika. Nia kubwa ikiwa kuona wanawake kwa wanaume watatoa sauti zao kuhakikisha na kulinda, pamoja na mengine, uzingatiwaji wa usawa wa jjinsia katika vifungu vyote vya Katiba mpya.”
Aidha alifafanua kuwa Mtandao wa Wanawake na Katiba, unawapongeza wajumbe wote wanawake kwa umoja wao, mshikamano na ushirikiano imara, ambao umeleta mafanikio makubwa katika michakato inayoendelea huko Dodoma kwenye Bunge Maalumu.
“…Huu ni mwanzo wenye kuonyesha mifano mizuri, na ambao tunapenda  kuuona ukiendelezwa na kusimamiwa imara wakati wote Bunge Maalumu litakapokuwa likifanya kazi yake ya kuchambua na kupitisha vifungu mbalimbali vya Katiba,” alimalizia Bi. Liundi.

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA TAREHE 17 -21 MARCH,2014

  DCIM100GOPRO
Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dododma kesho kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na  kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa. Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa  kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa 2:00  asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha  Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum  na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum.
Atakayeipata taarifa hii amjulishe mwenzake. 
Imetolewa na Ofisi ya
KATIBU WA BUNGE MAALUM

KAMATI YA PAC LEO IMEKUTANA NA BENKI KUU YA TANZANIA (B.O.T)

 
Zitto-Kabwe 
Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.
Kamati imeamua kwamba;
 
1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya tegeta escrow.2) TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP. Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.
PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.
PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.
 
Imetolewa na Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014

RIDHIWANI KIKWETE ADHAMIRIA KUWAKOMBOA WANA CHALINZE

CHZ 4Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.Picha na Othman Michuzi CHZ 10Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang’ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 16,2015.Picha na Othman Michuzi
CHZ 15Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea Jogoo kutoka kwa kina Mama wa Kijiji cha Kwamsanja,Kata ya Kibindu leo Machi 16,2914.Picha na Othman Michuzi
CHZ 16 
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwarihombo,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.Picha na Othman Michuzi

HOT NEWS MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA CCM YASHINDA KWA KISHINDO


1 (7)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Ndg. Godfrey Mgimwa akibebwa juu juu na wanachama na wapenzi wa CCM baada ya matokeo kuonyesha ameshinda kwa kishindo Kalenga.
Matokeo Kalenga CCM 16861, Chadema 4273, Chausta 78, Umoja wetu ndio Ushindi Wetu!
ush1 Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juu na wanachama wa CCM huku wakiserebuka kusherekea ushindi katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo inaonyesha CCM wanaongoza kwa mbali katika matokeo ya awali kwenye uchaguzi wa mbunge wa jimbo la Kalenga uliofanyika leo mkoni Iringa watu wengi walijitokeza asubuhi kupiga kura na hali ilikuwa ni ya utulivu kabisa watu wengi waliopiga kura wameishukuru serikali na tume ya uchaguzi kwa kuandaa utaratibu mzuri na kufanyika kwa uchaguzi wenye utulivu. mpaka sasa matokeo hayo yanaonyesha CCM inaongoza kata kumi na mbili  kati ya kata kumi na tatu za jimbo hilo.  ush3Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akipiga picha na wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa ambapo wana CCM wamefurika wakishangilia matokeo ya awali ya uchaguzi huo ambapo inaonyesha CCM inaogoza kwa mbali. ush4Ni fullshangwe nderemo na vifijo katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa kutokana na CCM kuongoza katika matokeo ya uchaguzi Kata ya Kalenga.ccm1Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakisherehekea ushindi jioni hii  ccm2 
Wana CCM wakiendelea kuserebuka kwa muziki kama wanavyoonekana. ccm3 
Ni raha kwa kwenda mbele kweli ushindi ni raha.
Matokeo ya Awali   baadhi ya vituo yako hivi CCM inaongoza
TOSA no.1 CCM 98 ,Chadema 20, CHAUSTA 0
Ipamba no2. CCM 104, Chadema 10,CHAUSTA 0
Isakulilo CCM 83,Chadema 8,CHAUSTA 0
Kilindi A CCM 69 ,Chadema 23, CHAUSTA 0
Ofisi ya Kijiji(Kilindi) CCM 117, Chadema 53, CHAUSTA0
Zahanati  CCM 117,Chadema 67, CHAUSTA 1
Ifunda
Kivalali A CCM 99 Chadema 19 CHAUSTA 0
Kivalali B CCM 109 Chadema 14, CHAUSTA 1
Muwimbi CCM164, Chadema 22 CHAUSTA 0
Mahanzi CCM 130 Chadema 46 CHAUSTA 0
Ikungwe A CCmM 131 Chadema 23 CHAUSTA 0
Ikungwe B CCM 216 Chadema 13 CHAUSTA 0
Magunga CCM 184 ,Cadema 4 CHAUSTA1
Wasa CCM 149,Chadema 15 CHAUSTA 0
Usengelidete CCM 260,Chadema 46,CHAUSTA O
CHANZO MOBLOG

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MARCH 17/ 2014MBEYAGREENNEWSBLOG

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.