Saturday 15 March 2014

ANGALIA KUHUSU JIMBO LA KALENGA KINACHOENDELEA


DOKII-KALENGA-538_5149e.jpg
chadema_fe0fb.jpg
Inasikitisha, kuwa chaguzi ndogo kama hii ya Kalenga ni kielelezo cha udhaifu wetu kama taifa. Kwamba wapiga kura wasiozidi 70 elfu ' wanavamiwa' jimboni na watu kwa maelfu kutoka pande mbali mbali za nchi katika kushiriki kupigania kititi cha Ubunge. Na imefika mahala hata wapiga kura wale wa Kalenga wapatao 70 elfu hawapati nafasi ya kuwasikliliza wagombea ubunge bali wanawasikiliza waliokuja kupiga kampeni na kisha kuondoka ifikapo kesho Jumapili. Wagombea wao wamefunikwa. Ni laiti nusu tu ya fedha inayotumiwa na vyama kule Kalenga kwa kugharamia kampeni ingetumika kwa maendeleo, basi, ingetosha kuzisaidia kata kadhaa za Kalenga katika kuboresha huduma ya afya na elimu.... Inasikitisha.
 Imeandikwa na Maggid,mjengwa
Kunduchi Mtongani

0 comments: