Thursday 13 March 2014

RIDHIWANI ARUDISHA FOMU ZA UBUNGE CHALINZE

 
 MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi, akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega. 
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega wakifurahia jambo. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na  washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega na wadau wengine akielekea kurejesha fomu.
 Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia tukio la Urudishwaji fomu wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo.
 
===========  ======== ======
Ridhiwani
arudisha fomu za Ubunge Chalinze.
 
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze
kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya
kugombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi.
 
Akisindikizwa na washindani wake
katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani
Madega, Ridhiwani aliwashukuru wana CCM na wakazi wa Chalinze kwa ujumla kwa
kumuunga mkono.
 
Ridhiwani pia ameahidi kushirikiana na
wanachalinze katika kutekeleza yote yaliyofanywa na wabunge waliotangulia
lakini pia amewataka wakazi wa Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombe wa
Chadema inayodhihaki kuwa yeye sio mkazi wa Chalinze. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze
kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey alinukuliwa akisema kuwa Ridhwani hawezi
kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa sio mkazi wa Jimbo hilo.
 
Aliongeza kuwa ili kuwahakikishia
wakazi wa Chalinze maendeleo inatakiwa kwa wagombea kutangaza sera
zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia ya kuwapumbaza wakazi wa
Chalinze.
 
Alisema kuwa
hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza kurumbana na
kukejeli kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya kisiasa. 
Alisema
hajatokea chumbani kugombania Ubunge badala yake amekuwa katika misingi ya kisiasa
tangia mdogo na amechukua uamuzi wa kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia
wananchi.
 
Alisema kuwa
kero kubwa inayowakabili wakazi wa Chalinze ni kukosekana kwa maji ya uhakika,
kero ambayo kwa sasa inatatuliwa kwa kuanzishwa kwa mradi wa maji ya uhakika. 
Aliongeza kuwa
pia kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za afya uhakika za afya kwa
wakazi wa eneo la Chalinze. 
“Najua
awali wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa kuna
ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji nayo
yanaongezeka”alisema Ridhwani.
 
Aliongeza kuwa
ongezeko hilo limepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa huduma mbalimbali kama hizo
za za kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua kero hizo.
“Watu
wanadhania kuwa mimi nimetokea chumbani kuja kwenye siasa hapana yani tena hata
sio kwa sababu ya kuwa mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura
huku sio, ila ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni
wakati wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa huku”alisema Ridhiwani.
 
Kuhusiana na
tatizo la migogoro katika jimbo hilo alisema kuwa anaona kuwa analo jukumu
kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM kwa muda mrefu
imekuwa ikifanya hivyo. 
Alisema kuwa
atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu ya
wafugaji na wakulima.
 
Ridhwani
anatarajia kuzindua rasmi kampeni yake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze. 
Uchaguzi mdogo
wa Jimbo la Chalinze unafanyika kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo
Said Bwamdogo.

0 comments: