Wednesday 12 March 2014

HULK ANAYETAKIWA NA CHELSEA ATUA LONDO NA MENEJA WAKE

MSHAMBULIAJI wa Zenit St Petersburg, Hulk amezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii kwa kuposti picha akiwa na wakala wake wakisafiri kwenda London - katika siku ile ile ambayo klabu hiyo ya Urusi imemfukuza kocha wake Luciano Spalletti.
Chelsea ilitoa ofa ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil Agosti mwaka jana, lakini hawakufanikiwa kukamilisha uhamisho wake.
Kocha Jose Mourinho alipigwa picha mwezi uliopita akilalamikia timu yake kutokuwa na washambuliaji na pia kuhoji umri wa Samuel Eto'o kama ni sahihi au amejipunguza.
Unakwenda wapi? Hulk amesema anakwenda kazini  mjini London akiwa na meneja wake ambaye pia ni rafiki yake

Hulk, alipiga picha akiwa kwenye ndege binafsi na kuiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram sambamba na ujumbe usemao: "Nakwenda kazini London. Nikiwa na meneja wangu na rafiki# Teo,".

0 comments: