Friday 14 March 2014

VAN PERSIE AFUNGUKA KUSEMA" NITAZEEKEA MAN UNITED"


MSHAMBULIAJI Robin van Persie amepuuza tetesi kwamba atahama Manchester United mwishoni mwa msimu baada ya kutofautiana na David Moyes kwa kusema atamalizia maisha yake yaliyobaki katika soka ya ushindani akiwa Old Trafford.
Van Persie aliiongoza United kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza uliopita baada ya kununuliwa kwa Pauni Milioni 24 kutoka Arsenal, lakini amekuwa akisotea kucheza kwa kiwango chake tangu Moyes achukue nafasi ya Sir Alex Ferguson.
Imezalisha maoni kwamba mshambuliaji huyo wa Uholanzi anaweza kuuzwa mwishoni mwa msimu na Moyes amepanga kukisuka upya kikosi chake kwa kusajili nyota kadhaa akiweo Edinson Cavani.
Bado nipo nipo sana: Robin van Persie akionekana  mwenye furaha wakati wa mazoezi Uwanja wa Carrington jana
Robin reliant: Van Persie is still Manchester United's main striker despite a difficult season
Getting stuck in: The Dutchman flies into a tackle in training
Robin haondoki: Van Persie bado ni mshambuliaji chaguo la kwanza Manchester United licha ya kuwa na msimu mgumu

But Van Persie mwenye umri wa miaka 30, amesema anataka kuona kumalizia miaka miwili iliyobaki katika mkataba wake na pengine akafuata nyayo za Wayne Rooney kwa kusaini Mkataba mpya.
"Ukweli ni kwamba, nina furaha sana hapa katika klabu,"alisema katika mahojiano maalum kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu Liverpool Jumapili.
"Nimesaini miaka mnne na nitafurahi kubaki kwa muda mrefu, zaidi ya miaka miwili niliyobakiza katika Mkataba wangu. Hivi ndivyo ninavyohisi,"amesema.
Imekuwa ikielezwa kwamba Van Persie amesikitishwa na kustaafu kwa Ferguson na havutiwi na mfumo wa mazoezi ya Moyes.

0 comments: