Saturday 15 March 2014

VPL: YANGA YABANWA NA MTIBWA, AZAM FC YAMNYOA COASTAL BAO 4-0

 
>>MZIZI WA FITINA KUKATWA JUMATANO: YANGA v AZAM!!
 
VPL-LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumamosi Machi 15
Azam FC 4 Coastal Union 0
Mtibwa Sugar 0 Yanga 0
Kagera Sugar 2 Tanzania Prison 1

VPL, Ligi Kuu Vodacom, iliendelea Leo na Mabingwa Watetezi, Yanga, walibanwa huko Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kutoka Sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar.
Ingawa Mtibwa walicheza pungufu Kipindi cha Pili baada ya Mchezaji wao Abdala Juma kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga kiwiko Kevin Yondani katika Dakika ya 56, Yanga walishindwa kutumia pengo hilo.

Huko Chamazi, Azam FC waliibamiza Coastal Union Bao 4-0 na kuendelea kujizatiti kileleni.
Bao za Azam FC zilifungwa na Kipre Tchetche, Bao 2, John Bocco na Kevin Friday.
Azam FC wamecheza Mechi 19 na wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 43 na kufuata Yanga waliocheza Mechi 18 na wana Pointi 39.
MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD PTS
1 Azam FC 19 12 7 0 27 43
2 Yanga SC 18 11 6 1 29 39
3 Mbeya City 21 10 9 2 10 39
4 Simba SC 21 9 9 3 17 36
5 Kagera Sugar 21 8 8 5 3 32
6 Ruvu Shooting 20 7 7 6 -4 28
7 Coastal Union 21 5 11 5 1 26
8 Mtibwa Sugar 21 6 8 7 -1 26
9 JKT Ruvu 21 8 1 12 -13 25
10 Prisons FC 20 3 10 7 -4 19
11 Mgambo JKT 20 4 6 10 -17 18
12 Ashanti United 21 4 6 11 -18 18
13 JKT Oljoro 21 2 9 10 -16 15
14 Rhino Rangers 21 2 7 12 -14 13
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Machi 19
Yanga v Azam FC
Jumamosi Machi 22
JKT Ruvu v Mbeya City
Rhino Rangers v Yanga
Kagera Sugar v Tanzania Prisons
Jumapili Machi 23
Simba v Coastal Union
Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting v Ashanti United
Azam FC v JKT Oljoro

0 comments: