Sunday 16 March 2014

RAIS KIKWETE AWAPA MILIONI 30 SIMBA SC KUCHANGIA UJENZI WA UWANJA WAO BUNJU, MAREKEBISHO YA KATIBA YAFANA


KLABU ya Simba SC imepewa Sh. Milioni 30 na Rais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ili washughulikie hati ya kiwanja chao kilichopo maeneo ya Bunju B, Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye Mkutano maalum wa marekebisho ya Katiba ya klabu hiyo uliofanyika asubuhi ya leo Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema pamoja na mchango huo, Rais JK aliwatakia heri katika mkutano huo huku akimkabidhi hundi ya fedha hizo kwa ajili ya upatikanaji wa  hati hiyo.
Mwanamichezo; Rais KIkwete (katikati) amewapa Simba SC Sh. Milioni 30

“Tunamshukuru Rais kwa msaada wake ameonyesha yeye ni mwanamichezo wa timu zote hivyo huu ni ushindi wa Simba na sio wa Rage,”alisema

Alisema kuwa Jumamosi ijayo atapitisha greda kwa ajili ya kusafisha Uwanja huo ili wachezaji waanze mazoezi kwenye Uwanja wao.

Rage alisema kuwa fedha hizo watazitumia vizuri ikiwa sambamba na kupunguza deni la wizara ya Ardhi wanaowadaiwa Sh41 Milioni kati ya Sh92 walizokuwa wanadaiwa.

Simba iliuziwa Kitalu 226 namba 1. Bunju mwaka 2006, uongozi wa Simba ulilipa Sh 50 Milioni Desemba 29, 2011.

Katika hatua hiyo hiyo, Simba imefanya marekebisho kwenye ibara ya 26(5 )sifa za wagombea ambapo kipengele hicho awali kilikuwa kinasomeka “Asiwe aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kwa kuhukumiwa kifungo.

Kipengele hicho sasa kinasomeka “Asiwe ametiwa hatiani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita bila mbadala wa adhabu. Na endapo ametiwa hatihani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita, awe amemaliza muda wa miaka 5, tangu kuisha kwa kifungo husika bila kitiwa hatiana kwa jingine lolote la jinai.

Wanachama hao hao wamegoma kukipitisha ibara ya 26 (9) Mgombea awe ametimiza angalau miaka mitatu ya uanachama. Ambapo sasa kinasomeka angalau awe na mwaka mmoja wa wanachama.

Pia ibara ya 25 (8) (iii) wajumbe watano wa kamati ya utendaji. Mwenyekiti aruhusiwe kuteuwa wajumbe wengine watano wa kamati ya utendaji ambao anaweza kubadilisha kwa kadri anavyoona inafaa.wajumbe hawa wa kuteuliwa wanatakiwa kuwa na sifa zilizile wanazotakiwa kuwa nazo wajumbe wa kuchaguliwa na wanachama.
 Na Zaituni Kibwana, Dar es Salaam
CHANZO BIN ZUBERRY BLOG

0 comments: