Saturday 15 March 2014

LIGI KUU ENGLAND: VILLA YAIPIGA CHELSEA 1-0! MOURINHO ATOLEWA NJE!

>>CHELSEA WAMALIZA GEMU MTU 9 NA MOURINHO ATOLEWA NJE!

LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumamosi Machi 15
Hull 0 Man City 2
Everton 2 Cardiff 1
Fulham 1 Newcastle 0
Southampton 4 Norwich 2
Stoke 3 West Ham 1
Sunderland 0 Crystal Palace 0
Swansea 1 West Brom 2
Aston Villa 1 Chelsea 0

CHELSEA-RED_CARD_RAMIRESUWANJANI VILLA PARK, Chelsea, Vinara wa Ligi Kuu England, wamekiona cha moto baada kufungwa 1-0 na Aston Villa na pia kumaliza Gemu wakiwa Mtu 9 Uwanjani baada ya Kadi Nyekundu kwa Wachezaji wao wawili kutoka Brazil, Willian na Ramires, na pia Meneja wao Jose Mourinho kutolewa nje na Refa Chris Foy.
Balaa kwa Chelsea lilianza Dakika ya 69 baada ya Willian kumwangusha Mchezaji Bora wa Mechi hii, Fabian Delph, na kulambwa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Katika Dakika ya 82, Delph alikokota Mpira na kuwatambuka Wachezaji kadhaa wa Chelsea na kumpasia kwenye Winga Mark Albrighton ambae alitoa krosi ya chini iliyochezwa kwa kisigino na Delph na kufunga Bao zuri na la ajabu.
Huku Dakika zikiyoyoma, Ramires wa Chelsea alipewa Kadi Nyekundu kwa kumkita El Ahmadi na tukio hilo lilimfanya Meneja wa Chelsea Jose Mourinho akasirike na kutoa maneno yasiyofaa kitendo ambacho kilimfanya Refa Chris Foy amtoe nje.
Chelsea bado imebaki kileleni ikiwa Pointi 6 mbele ya Man City lakini wao wamecheza Mechi 3 zaidi ya City.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Bacuna, Vlaar, Baker, Bennett, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Benteke, Agbonlahor
Akiba: Clark, Albrighton, Steer, Sylla, Holt, Lowton, Robinson.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian, Oscar, Hazard, Torres
Akiba: Lampard, Mikel, Schurrle, Salah, Ba, Schwarzer, Kalas.
Refa: Chris Foy
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 16
1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
30
33
66
2
Man City
27
44
60
3
Liverpool
28
38
59
4
Arsenal
28
24
59
5
Tottenham
29
0
53
6
Man United
28
12
48
7
Everton
27
11
48
8
Newcastle
28
-2
43
9
Southampton
30
2
42
10
Aston Villa
29
-6
34
11
West Ham
28
-4
31
12
Stoke
29
-14
31
13
Hull
29
-7
30
14
Swansea
28
-4
29
15
Norwich
29
-22
29
16
Crystal Palace
28
-19
27
17
West Brom
28
-11
25
19
Cardiff
29
-28
25
18
Sunderland
26
-16
24
20
Fulham
29
-36
21

0 comments: