Thursday 13 March 2014

CHECKI HAPA GIGGS AKWAA TUZO NYINGINE!!

>>NI ‘TOPPS STICKERS’, AMBAZO WATU HUKUSANYA PICHA ZA MASTAA!!
GIGGS-TUZO_TOKA_FAVETERANI Ryan Giggs, ambae sasa ni Kocha-Mchezaji waTOPPS_STICKERSMabingwa wa England Manchester United, ametunukiwa Tuzo maalum toka kwa TOPPS, ambao ndio Wasambazaji rasmi wa Stika za Ligi Kuu England, ambayo inadhaminiwa na Barclays.
Giggs alipewa zawadi Maalum ya Kumbukumbu ambayo ina mkusanyiko wa Stika maalum za Misimu yote 21 ya Ligi Kuu England ambayo yeye ndie Mchezaji pekee kucheza Misimu yote hiyo.
Kampuni ya TOPPS imekadiria kuwa tangu Giggs, mwenye Miaka 40, aanze kucheza Ligi Kuu England ilipoanzishwa Mwaka 1992, ni zaidi ya Nusu Bilioni za Stika zilitengenezwa na kati ya hizo za Ryan Giggs ni zaidi ya Milioni 7.
Akijiona kwenye Stika hizo za kila Msimu kwa Misimu 21, Giggs amesema ni furaha kubwa na hasa kujiona kwenye Jezi tofauti za kila Msimu lakini Jezi ambayo anaikumbuka zaidi ni ile ya Mwaka 1999 ambapo walitwaa Trebo na Man United, yaani FA CUP, Ubingwa wa England na UEFA 

CHAMPIONZ LIGI.
Giggs amekiri kuwa hivi sasa Wachezaji wenzake wanamcharura kuhusu Nywele zake ambazo Stika hizo zinaonyesha zilianza ndefu na nyeusi wakati yu mdogo na sasa zenye mvi na chache.
Nae Chris Rodman, Kiongozi wa TOPPS, ametamka: “Ryan Giggs amepata mafanikio makubwa kupita Mchezaji yeyote kwenye Miaka 22 ya Ligi Kuu England. Ametwaa Ubingwa mara 13 na kucheza Mechi zaidi ya 600. Yeye ndio Mchezaji pekee ambae ametokea kwenye Matoleo Rasmi ya Stika za Ligi Kuu England kila Msimu.”

0 comments: