Thursday 13 March 2014

ANGALIA SUTI YENYE BEI GHALI KULIKO ZOTE DUNIA DOLA ZA KIMAREKANI 3.2 MILION

most_exp_suit_46Cwq_12
. Suti kali kupitia zote ambayo haiingii risasi, maji na ina kiyoyozi ndani  

Mara nyingi, watu mashuhuri na wasanii ni watu muhimu sana duniani kote na kuvaa vitu kadhaa ndani ili kuzuia risasi au aina yeyote ya kitu ambayo kinaweza kumdhuru nah ii tabia ipo zaidi kwa viongozi wa kitaifa.
Kwa kawaida watu hawa mashuhuri na maarufu kupendelea kuvaa suti za aina mbalimbali zenye bei kubwa na suti zenye urembo au vitu vya kuvutia lakini wengi wao kuvaa kitu ndani cha kinga (Bullet proof).
Lakini hatimaye watu hawa mashuhuri wanalo jambo moja kubwa la kufurahia nalo ni uzinduzi wa suti mpya ambayo risasi haipenyi na ni ulinzi mkubwa kwa maisha ya watu hawa mashuhuri duniani.
Suti hiyo si nyingine ni ‘Diamond Armor’ ambayo kwa muonekano wa nje ni kama vile zile suti za mcheza filamu maarufu duniani James Bond za filamu yake ya 007.
Kampuni inayoitwa ‘ Suitart ‘, makao makuu yake yapo Zurich, Uswisi ndio wametengeneza suti hizi ghali zaidi duniani ikiwa pamoja na kiyoyozi ndani kwa ajili ya kujisikia maraha.
most-expensive-suit
Wachambuzi wa mambo wanasema suti hiyo itapata wateja wengi ndani ya muda mfupi kabisa baada ya kuzinduliwa hivi karibuni.
Suti hiyo ni bulletproof ( imethibitishwa kwa viwango vya NATO) kama ilivyoelezwa kabla na wachambuzi wa kimataifa pamoja na kifaa maalum cha kiyoyozi na mfumo maridadi wa kuzuia maji kuingia ndani.
Ni suti tu ya aina yake ambayo ina mfumo wa hali ya hewa na imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kwa sababu ukishika kifungo tu inatoa ubaridi mwanana kabisa.
Kuongeza umaridadi na daraja ya suti, Diamond Armor sehemu ya vifungo kuna almasi nyeusi ambayo nayo inasaidia kuzuia risasi kupenya ndani.
CHANZO  Na Damas Makangale, 
MOblog kwa Msaada wa Mtandao

0 comments: