Saturday 15 March 2014

ANGALI MATIKIO YALIYOTOKEA MECHI YA MTIBWA SUGAR NA YANGA KATIKA UWANJA MOGORO


Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Iliyoanza Leo Dhidi Ya  Yanga.
Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema 

Kikosi cha Timu ya  Yanga Kilichoanza Leo : Kutoka Kushoto Didier Kavumbangu, Haroub Canavaro,Khamis Kiiza,Oscar Joshua,Frank Domayo,Simon Msuva, Juma Abdul,Nizar Khalifan,Mbeleni Juma Kaseja. (P.T)
Na  MATUKIO NA VIJANA   
Ligi Kuu Tanzania Bara Imendelea Leo Ambapo Katiak uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kulikuwa na Mchezo Mkali Dhidi ya Wenyeji Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogogo Dhidi ya Mabingwa Watetezi  Yanga ya Dar es Salaam . Katika Mchezo Huo Hadi Dakika 90 za Mchezo Zinamalizika Matokeo Timu Hizo Zmetoka sare ya Bila Kufungana.Mchezo Ulikuwa Mkali na wakukamiana Pamoja na Hali ya Uwanja Kutokuwa nzuri kutoka na Mvua Zianzoendelea Kunyesha Mkoani Hapa.Timu ya   Yanga walitengeneza Nafasi Nyingi za Kufunga lakini walishindwa Kuzitumia .Wachezaji Emanuel Okwi na Didie Kavumbangu walipata nafasi za kufunga katika dakika ya 80 na 88 lakini awalishindwa kufunga, Yanga walifanya Mabadiliko katika Dakika ya 65 Alitoka Nizar Khalifan  na Kuingia Said Dilunga,Dk78 Alitoka Khamis Kiiza na Kuingia  Husein Javu. 
Mtibwa Sugar Walipata Pigo katika Dakika ya 70 Ambapo Mshambuliaji Wao Abdalah Juma  Alionyeshwa Kadi Nyekundu kwa Kumchezea Rafu mbaya.

 Mashabiki wa Timu ya  Yanga waliojitokeza kwa Wingi katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani morogoro

Benchi la Timu ya Soka ya Mtibwa ya Morogoro  Lilkiongzwa na Kocha wa Timu Hiyo  Meky Mexime Wa Kwanza Kushoto..

Makocha wa  Yanga 

Mashabiki waliojitokeza kwa Wingi Katika Uwanja w Jamhuri Mkaoni Morogoro Leo Katika Mcheza Kati ya Yanga Dhidi ya Mtibwa Sugar 

Mshambuliaji wa Timu ya  Yanga Emanuel Okwi akitafuta Mbinu za Kufunga katika Lango la Timu ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro Katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro.

Moja ya Purukushani katika Lango la Timu ya  Yanga Katika Mchezo Uliochezwa katika Uwanja wa Jamuhuri Mkaoni Morogoro  

Mchezaji wa  Yanga Simon Msuva Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Timu ya Mtibwa Sugar Paul Ngalema 

 

 

0 comments: