Sunday 16 March 2014

JOSE MOURINHO AMPONDA REFA CHRIS FOY BAADA CHELSEA KUFUNGWA!

MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amemponda Refa Chris Foy baada Jana Chelsea kufungwa Bao 1-0 na AstonMOURINHO.MSTARINI_MIKONO_JUU Villa huko Villa Park kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Wachezaji wake wawili kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Vile vile, Mourinho mwenyewe alitimuliwa na Refa Foy na kuamriwa kuondoka Benchi kwenda Jukwaani kufuatia rabsha baada kutolewa kwa Ramires aliecheza Rafu mbaya na mapema Willian nae alitolewa nje baada kuzoa Kadi za Njano mbili.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Mourinho alilalamika: “Lazima tulikuwa hatuna bahati kabisa baada uchezeshaji wa Refa wa namna hii. Hii si kosa moja toka kwa Refa bali uchezeshaji wa aina hiyo tangu Dakika ya 1 hadi 94.”
CHELSEA-RED_CARD_RAMIRES
MAREFA NA CHELSEA:
-REFA Chris Foy amewatoa Wachezaji 6 wa Chelsea katika Ligi Kuu England akipitwa tu na Refa Mike Dean ambae ameshawapa Wachezaji 7 wa Chelsea Kadi Nyekundu kwenye Ligi hiyo.

Akiongea kuhusu kutolewa kwake nje na Refa Chris Foy, Mourinho alisema: “Sijui kwanini nilitolewa. Nilimuuliza lakini Refa alikataa kuniambia!”
Aliongeza: “Gabriel Agbonlahor alikuwa Benchi na yeye akaingia Uwanjani na kumvuta Ramires. Kisha kila Mtu aliingia Uwanjani, mimi, Paul Lambert [Meneja wa Villa] na Wasaidizi wangu! Kama ni kutolewa wote ilibidi tutolewe.”
LIGI KUU ENGLAND:
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
30
33
66
2
Man City
27
44
60
3
Liverpool
28
38
59
4
Arsenal
28
24
59
5
Tottenham
29
0
53
6
Man United
28
12
48
7
Everton
27
11
48
8
Newcastle
28
-2
43
9
Southampton
30
2
42
10
Aston Villa
29
-6
34
11
West Ham
28
-4
31
12
Stoke
29
-14
31
13
Hull
29
-7
30
14
Swansea
28
-4
29
15
Norwich
29
-22
29
16
Crystal Palace
28
-19
27
17
West Brom
28
-11
25
19
Cardiff
29
-28
25
18
Sunderland
26
-16
24
20
Fulham
29
-36
21

0 comments: