Saturday 15 March 2014

MALAYSIA :JUHUDI ZA KUISAKA NDEGE ZASHIKA KASI

 
140314092902 malaysia 304x171 ap 65b82
Wiki moja tangu ndege ya Malaysia iliyokuwa imewabeba abiria 239 kutoweka, juhudi za kimataifa kuisaka ndege hiyo bado zinaendelea.
Mataifa kumi na mbili sasa yamejiunga pamoja kuisaidia serikali ya Malaysia na msako huo, juhudi zenyewe zikijikita zaidi Magharibi mwa rasi ya Malaysia.(Hudugu)
Marekani imesema kuwa inatuma manowari zake za kivita, pamoja na ndege maalum ya uchunguzi katika maeneo ya Bengal, Bahari ya Andaman na sehemu za Bahari hindi.
Mnamo Ijumaa taarifa ziliibuka kuwa ndege hiyo ilituma mawasiliano katika kituo cha trafiki ya ndege kwa karibu saa tano baada ya taarifa ya kupotea kwake kutolewa.
Taarifa zinasema kuwa mawasiliano hayo yanaweza kusaidia katika kujua iliko ndege hiyo na ndio maana Marekani ikaamua kutuma meli zake za kivita katika Bahari Hindi.CHANZO BBC

0 comments: