Thursday 13 March 2014

WANACHAMA SIMBA WALIANZISHA TENA, WASEMA HAIWEZEKANI MKUTANO WA JUMAPILI AJENDA MOJA TU WAKATI MATATIZO KIBAO


VIONGOZI wa matawi ya Simba, wamepinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura Jumapili ukiwa na ajenda moja tu badala yake wametaka kuwe na ajenda tano.

Kamati ya Utendaji ya Simba chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage imeitisha mkutano huo wenye ajenda moja tu ya kufanya marejkebisho ya katiba kuingiza kipengele cha kuwa na Kamati ya Maadili ya klabu kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa wanachama wake Desemba mwaka jana.
Ajenda moja haiwezekani; Chuma Sulaiman maarufu kama Bi Hindu akizungumza na Waandishi Idara ya Habari (MAELEZO).

Wakizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) mchana wa leo, baadhi ya viongozi wa matawi na wanachama wa Simba walimtaka Rage na kamati yake ya utendaji waongeze ajenda nyingine ili mkutano huo uwe na ajenda tano.

"Tunataka kujua uwanja wetu wa kisasa unajengwa lini, pesa za mauzo ya wachezaji wetu, mauzo ya jezi, kesi zilizopo mahakamani dhidi ya Simba na uchaguzi Makamu Mwenyekiti baada ya kujiuluzu kwa Kaburu (Geofrey Nyange)," amesema Bi. Chuma Suleiman. "Pasipo kuyafanya hayo, tunaamini kutakuiwa na vurugu katika mkutano huo."
 Chanzo bin zuberry blog
 Na Renatus Mahima, Dar es Salaam

0 comments: