Friday 14 March 2014

ANGALIA BOSI WA BAYERN MUNICH ALIVYO PIGWA JELA!!


ULI_HOENESS
MAHAKAMA ya huko Ujerumani imemhukumu Kifungo Rais wa Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich, Uli Hoeness, kwa ukwepaji kulipa Kodi.
Hoeness, licha ya kuungama mwenyewe kwamba alikwepa Kodi, Mahakama hiyo haikumwonea huruma na kuamua kumpa Kifungo cha Miaka Mitatu na Nusu Jela.
Jaji wa Mahakama, Rupert Heindi, aliamua kuwa kuungama kwa Hoeness kulikuwa na kasoro na pia hakutimiza matakwa ambayo yangempa Msamaha wa Kifungo.
Hoeness alikiri kukwepa Kodi ya Euro Milioni 27.2 ambayo alipaswa kulipa kufuatia kuwa na Akaunti kwenye Benki ya Uswisi.
Hoeness, mwenye Miaka 62 na ambaye akiwa kama Mchezaji aliisaidia Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 1974 na kama Kiongozi wa Bayern aliinua sana Klabu hiyo Kiuchumi na Kimafanikio, aliondoka Mahakamani bila kuzungumza na Wanahabari.
Hata hivyo, Mawakili wake wamesema watakata Rufaa Mahakama ya Juu huko Germany.
Huko Germany, ukwepaji kulipa Kodi ni kosa kubwa na huvuna Kifungo cha Juu cha Miaka 10 lakini kwenye Kesi ya Uli Hoeness, Waendesha Mashitaka walitaka afungwe Miaka 5 na Nusu kwa vile alikiri na kuisaidia Mahakama.
Awali Hoeness alishitakiwa kwa kukwepa Kodi ya Euro Milioni 3.5 lakini Kesi ilipoanza Jumatatu hii, Hoeness aliistua Mahakama kwa kukubali kuwa alikwepa Kodi ya Euro Milioni 18.5 na hii iliongezeka na kufikia Euro Milioni 27.2 Siku ya Pili ya kusikilizwa Kesi kufuatia ushahidi wa Inspekta wa Kodi.
Hadi sasa haijulikani kama Hoeness atabaki kuwa Kiongozo wa Bayern Munich na Klabu hiyo imesema itajadili suala hilo.
Bayern Munich inamilikiwa Kibinafsi lakini Kampuni kubwa za Germany, Adidas AG, Allianz na Audi AG, kila moja inamiliki Hisa za Asilimia 8.3 kila moja huku Deutsche Telekom AG wakiwa ndio Wadhamini wakubwa.

0 comments: