Saturday 15 March 2014

YANGA IPO TAYARI KWA KAZI NA MTIBWA SUGAR,LEO HII

Mabingwa wa Soka Tanzania, Yanga wametua mjini Morogoro tayari kwa mechi yao ya leo hii kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea leo hii  (Machi 15 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo mabingwa watetezi Yanga wataumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Nao vinara wa ligi hiyo, Azam wanaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.


Mechi nyingine itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.

0 comments: