Wednesday 12 March 2014

WENGER AMBATIZA ARJEN ROBBEN ‘MWANGUKAJI STADI!’ RUBBENI NAIJIBU !!!!!

>>AITAJA BAYERN TIMU NZURI LAKINI MSIMU HUU NI DHAIFU!
>>ROBBEN AJIBU: ‘ÚKIWA MENEJA MKUBWA KUBALI KUFUNGWA! ACHA KULALAMIKA MAMBO YA KIPUUZI!’
WENGER_BAADA_KUFUNGWAMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amembatiza Fowadi wa Bayern Munich Arjen Robben kuwa ni ‘Mwangukaji Stadi’ kufuatia Jana Sare ya Bao 1-1 kati ya Bayern na Arsenal ambayo iliwatupa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Timu hiyo ya England.
Arsenal wametolewa nje ya UCL kwa kufungwa Jumla ya Mabao 3-1 baada kufungwa 2-0 huko London Mwezi uliopita katika Mechi ya Kwanza na sasa Bayern Munich, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, wanatinga Robo Fainali.
Hiyo Jana huko Allianz Arena, Munich, Bayern walitangulia kufunga kwa Bao la Bastian Schweinsteiger na Arsenal kusawazisha kupitia Lukas Podolski na pia kunusurika kufungwa kwa Penati ya Dakika za Majeruhi ambayo ilipigwa na Thomas Muller na kuokolewa Kipa Lukasz Fabianski ambae alikuwa Golini kuchukua nafasi ya Wojciech Szczesny aliepewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea vibaya Arjen Robben katika Mechi ya Kwanza na hivyo kufungiwa Mechi hii.
Robben ndie aliesababisha Penati hiyo ‘laini’ ya Jana iliyokoswa na Thomas Muller baada kuanguka alipokabiliana na Sentahafu wa Arsenal, Laurent Koscielny.
Mapema Kipindi cha Pili, huku akikabiliwa na Santi Cazorla, Robben alijiangusha lakini Refa kutoka Norway, Svein Oddvar Moen, hakutoa Penati lakini pia hakumpa Kadi ya Njano Robben kwa kujiangusha.
Akikumbusha pia tukio la Robben la Mechi ya Kwanza aliposababisha Kipa Wojciech Szczesny kupewa Kadi Nyekundu na kutolewa Penati, Wenger alifoka: “Robben ni mzuri sana katika kupata mengi bila kuwepo kitu. Ni Mchezaji mzuri na pia mwangukaji mzuri! Yeye hukatiza mbele ya Mtu na kupunguza kasi na kujiangusha. Anapata frikiki. Ndio maana Jana tuliongea kuhusu Marefa. Kama Refa angempa Kadi kwa tukio la kwanza lile la pili lisingetokea!”
Wenger pia alisema tofauti yao na Bayern ilikuwa kwenye Mechi ya Kwanza na kile kilicholeta tofauti ni Kadi Nyekundu kwa Kipa Wojciech Szczesny.
Wenger aliwatakia heri Bayern na kusema: “Nawatakia heri Bayern, ni Timu nzuri lakini Msimu huu wapo dhaifu kupita Mwaka Jana.”
Nae Arjen Robben amejibu mapigo kwa kusema: “Siku zote nimesema ukiwa Meneja mkubwa kubali kufungwa. Ukishinda, furahia na ustarehe lakini ukifungwa acha kulalamika mambo ya kipuuzi!”

0 comments: