Saturday 15 March 2014

DROO ZA ROBO FAINALI ZA UEFA CHAMPIONZ LIGI & EUROPA LIGI IJUMAA!

>>DROO HAIBAGUI, KLABU NCHI MOJA ZINAWEZA KUKUTANISHWA!!
DROO za Robo Fainali za Mashindano makubwa ya Klabu Barani Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI,UCL-DROOUCL, na EUROPA LIGI, zitafanyika ndani ya House of European Football huko Nyon, Uswisi hapo Ijumaa Machi 21.
Droo ya UCL itafanyika kuanzia Saa 8 Mchana na kuendeshwa na Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, akisaidiwa na Mkurugenzi wa Mashindano ya UEFA, Giorgio Marchetti, pamoja na Balozi wa Fainali yake itayochezwa huko Lisbon, Ureno Mwezi Mei, Luis Figo.

UEFA CHAMPIONZ LIGI:
-KLABU ZIPO ROBO FAINALI:
-Bayern Munich
-Atletico Madrid
-Barcelona
-Paris Saint-Germain
-Washindi 4 kwenye Marudiano kati ya [Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]:

Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]


Droo ya EUROPA LIGI pia itaendeshwa na Gianni Infantino na Giorgio Marchetti na safari hii atakuwepo Balozi wa Fainali yake itayochezwa huko Turin, Italy, Ciro Ferrara..
Kwenye Droo hizi za Robo Fainali kutakuwa hamna kubagua Timu hivyo Timu za Nchi moja zinaweza kupangiwa kukutana.
Mechi za Robo Fainali za UCL zitachezwa Aprili 1 na 2 na Marudiano ni Aprili 8 na 9 wakati zile za EUROPA LIGI zitachezwa Aprili 3 na Marudiano ni Aprili 10.
Droo za Nusu Fainali zitafanyika Ijumaa Aprili 11 huko Nyon, Uswsi.

0 comments: