MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Monday 29 December 2014

Timu ya taifa ya Tanzania yaanza kambi leo Dar es Salaam




Timu ya taifa ya Tanzania inaanza kambi leo Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya kriketi ya Afrika chini ya miaka 19 daraja la 1 itakayofanyika nchini Namibia mapema mwakani.
Kambi hiyo chini ya kocha mchezaji Hamis Abdallah inakuja baada ya majuma mawili ya michuano ya majaribio yaliyofanyika Nairobi, Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu baada ya wenyeji kuwafunga Uganda.
Namibia itakuwa wenyeji wa michuano hiyo itakayokuwa ni sehemu ya kufuzu kucheza kombe la dunia chini ya miaka 19.
A wali michuano hiyo ilipangwa kuanza Januari Mosi na kupelekwa mbele hadi Februari.
Kenya na Uganda zitakuwa miongoni mwa nchi shiriki kutoka Afrika Mashariki na michuano ya Nairobi ilikuwa na lengo la kuziandaa timu zao.
Abdallah ameiambia BBC kuwa baada ya mapumziko ya Christmas wanaanza mazoezi wakiwa na ari na nguvu.
Timu ya Tanzania hivi karibuni ilichukua ubingwa Wa Afrika chini ya miaka 19 ligi daraja la 2, hivyo kufuzu michuano ya Namibia itakayoanza mapema mwezi wa pili

Mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake kuzinduliwa Januari Mosi


Mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) yanazinduliwa rasmi Januari Mosi mwakani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa mechi kati ya wenyeji Mwanza na Mara. Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam itachezwa kuanzia saa 10 jioni. Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin yatachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya kwanza.
Januari 10 mwakani ndipo zitachezwa mechi kwa mikoa yote ambapo Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora vs Kigoma (Ali Hassan Mwinyi), Simiyu vs Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha vs Manyara (Sheikh Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika).
Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma vs Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya vs Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi vs Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma vs Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.
Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwakani, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.
Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwakani wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwakani.
Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.
Mdhamini atatoa jezi kwa timu zote zinazoshiriki kabla ya kuanza mashindano hayo.

ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.

Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

Abiria miamoja wakwama:ATC

  

Shirika la ndege Tanzania ATC
Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya ATC wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari zao kuarishwa. Wengi wao wakielekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, kuelekea Mtwara na Kigoma wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
Abiria hao imebidi wakodiwe hoteli ilivyo ada wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini
Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo.
Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro….Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.

Wednesday 24 December 2014

Bolton yamsajili mgongwe E mile heskey kwa mkataba wa muda mfupi

 

Klabu ya Bolton Wanderers imetangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Emile Heskey kwa mkataba wa muda mfupi.
Heskey mwenye umri wa miaka 36 amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo huku akikitumikia kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 katika mchezo dhidi ya Reading Jumatatu iliyopita.
Mkongwe huyo ambaye ameitumikia Uingereza mechi 62 alikuwa akicheza katika klabu ya Newcastle Jets ya Australia ambayo ilimuachia April mwaka huu.
Bolton kwasasa inasubiri ITC ya mshambuliaji ili kukamilisha usajili wake.

Huyu ndiyo ww jamaa aliye kula tumbo mayai 150 na mayai ya kuku 10 kwa dakika 37

A man challenged himself to eat 150 quail eggs and 10 chicken eggs in 37 minutes at a restaurant in Changsha, central China's Hunan province, December 23. ,   yu

Amwacha mumewe na dadake uchi baada ya wakifanya mapenzi

 

Wawachwa uchi

Mwanamke kwa jina Ting Su nchini Uchina alimwacha mumewe na dadake bila nguo barabarani baada ya kuwapata wakifanya mapenzi Ting Ting Su aligundua kwamba mumewe alikuwa akimdanganya na dadaake na kuwafuata hadi katika kituo kimocha cha maduka akitumia teknologia katika simu yake ambapo aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.
Wawili hao walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili kujaribu kumuelezea kilichokuwa kikendelea lakini waliwachwa na mshangao mkubwa wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka na kuwawacha wawili hao barabarani bila nguo.
Kulingana na gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na yeye hakubakia nyuma.
Mumuwe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka.

APORWA NA KUJERUHIWA KWA RISASI

Mpita njia ajeruhiwa kwa Risasi na Majambazi waliovamia na kupora ktk duka la Pesa Morocco Kinondoni


Less than one hour ago here at Morocco nyuma ya Airtel Building a lady was shot to dead!!

Bodaboda walivamia kiduka cha M-PESA, tiGO PESA na Airtel Money; wakati wanaondoka wakawa wanapiga risasi ikampata huyu dada alikuwa anajipitia barabarani hajui hili wala lile.


- Kumbe huyu dada hakufa. Risasi ilimpalaza upande wa kulia. Walimshoot baada ya kuonekana anaongea na simu, baada ya tukio la kumuibia dada mwingine, ambaye inasemekana alikuwa ametokea Mlimani City na Hela.

- Taarifa za usiku wa leo, Disemba 23, 2014 zinadai Glory kaaga dunia! R I P
 

Wednesday 17 December 2014

MUNGU WANGU MSAIDIZI WA MAXIMO NAYE ASEPA KWENDA KWAO BRAZIL


NEIVA...


Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva naye yuko njia moja kurejea kwao.
Taarifa za uhakika zinaeleza, Neiva anaondoka na nafasi yake itachukuliwa na Boniface Mkwasa.

Usiku wa kuamkia jana kumekuwa na kikao kizito cha viongozi wa Yanga kujadili mustakabari wa Wabrazil hao.
"Ni kweli Neiva ataondoka, hilo suala limejadiliwa. Maana anatakiwa Mkwasa kuja kuziba nafasi yake," kilieleza chanzo.

"Kama akija kocha Pluijm, lazima atataka kufanya kazi na Mkwasa."



Tuesday 16 December 2014

VAN GAAL KOCHA BORA WA MWAKA, VAN PERSIE ABEBA TUZO, ROBBEN MWANA MICHEZO BORA


kocha louis van gaal ameibuka na kupewa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa uholanzi baada ya kuifikisha nchi hiyo kwenye nusu fainali ya kombe la dunia 2014. mshambuliaji wake, robben van persie amepewa tuzo ya bao bora, lile alilofunga kwenye kombe la dunia akipaa kama ndege na mshambuliaji wa bayern munich, arjen robben ameteuliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka wa uholanzi. tuzo hizo zimefanyika juzi usiku nchini humo.





Amissi Tambwe kutua Yanga asema Ndipo alipo pataka ili awaanyeshe makali walio muacha

  
tambwe yanga
 HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa dakika chache zilizopita ni kwamba klabu ya Yanga imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
 Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Emerson Oliveira wa Brazil aliyetemwa kwa kukosa ITC.
Tambwe ametua Yanga ikiwa ni siku chache baada ya Mganda Hamis Kiiza kuachwa na klabu hiyo na kukimbilia URA ya Uganda baada ya Kpeh Seen Sherman wa Liberia kupewa kandarasi ya kuichezea timu hiyo.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
 Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
 Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
 Yanga imekamilisha usajili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa leo na TFF.

Sakata la Escrow lafanya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema kuaachia ngazi



http://2.bp.blogspot.com/-HfIVzV9HEPE/Uq2Qh28re9I/AAAAAAAALfk/iZ76iAX0yLA/s640/1.png
jaji Werema aliyetangaza kuachia ngazi mwenyewe

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema ametangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo.
Habari hizo zinasema Jaji Werema mmoja wa vigogo wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la uchotwaji wa fedha za Akaunti za Tegeta Escrow zipatazo zaidi ya Sh Mil 300.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zinasema kuwa Jaji Werema ameamua kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake na kwamba Rais Jakaya Kikwete ameafikiana na maamuzi hayo na kumshukuru kwa ujtendaji wake na kumtakia kila la heri katika maisha yake mapya.
Hata hivyo taarifa hizo zinasema kuwa, maamuzi hayo yamekuja baada ya shinikizo kubwa ambalo limekuwa likitolewa kila pembe ya nchi kwa Rais JK kuwawajibisha wote waliotajwa kwenye mapendekezo nane ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusiana na sakata hilo ambalo limeitia doa Tanzania mbele ya nchi wahisani.

Monday 15 December 2014

Breaking news ya kocha Marcio Maximo kuondoka Yanga.


BreakingHabari rasmi toka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu hiyo ambapo habari hizi zinakuja dakika chache baada ya vyombo vya habari kuripoti tetesi zinazohusu mustakabali wa kocha huyo Mbrazil.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba aada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi.
Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri Mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo.
Nafasi ya Maximo sasa itachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts.
Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.

Simba kusajili beki, kutoka mtibwa sukari usiku wa leo kabla ya kufungwa kwa usajili


Katika usiku ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Kessy.
Beki huyo ambaye ametokea kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kutumainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro, anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma, Danny Sserunkuma, na Juko Murshid wote kutoka Uganda.
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kuwa mmoja ya wachezaji wa Timu ya Taifa Stars alichezea Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1.
hassan kessy
Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa, Jamal Bayser.
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30.

ENRIQUE ASISITIZA LICHA YA SARE, BARCELONA BADO NI BORA


Kocha Luis Enrique amesema hajakatishwa tamaa na uchezaji wa kikosi chake cha Barcelona.

Barcelona ilibanwa na kutoka sare na Getafe katika mchezo ulioonyesha kuwaudhi mashabiki wa Barcelona.
“Unajua inavyokuwa ngumu kama umeingia na sasa ndiyo tuko kwenye mabadiliko.

“Lakini ugumu unaongezeka kama haukutumia nafasi vizuri,” alisema.
“Nisisitize, kama utazungumzia ubora wa timu, basi timu yetu ni bora na sare haiwezi kutuondoa katika hilo,” alisistiza.


“Kikubwa kinachotakiwa ni kutatua matatizo yaliyotokea katika mechi hiyo, halafu tusonge mbele, hilo ndilo jambo la msingi zaidi.”

LIVE: UPANGAJI MAKUNDI UEFA CHAMPIONS LEAGUE 16 BORA


Upangaji wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 Bora unaendelea sasa:


Chelse Vs PSG
Man City Vs Barcelona
Bayer Leverkusen Vs Atletico Madrid
Juventus Vs Borrusia Dortmund
FC Schalke Vs Real Madrid  

FC Shaktar Vs Bayern Munich
Arsenal Vs AS Monaco

Basel FC Vs FC Porto

Aliye mchapa mtoto wa mwajiri wakeafungwa jela miaka ...........


Jolly Tumuhirwe apatikana na hatia ya kumtesa mtoto mdogo na kufungwa jela miaka 4

Yaya wa Uganda aliyejipata pabaya kwa kumchapa mtoto wa mwajiri wake, amehukumiwa jela miaka minne kwa kosa la kumtesa mtoto.
Kisa cha yaya huyu kilizua hasira miongoni mwa watu wengi katika mitandano ya kijamii pale kanda ya video iliibuka mitandaoni ikimwonyesha yaya huyo akimchapa na kumkanyaga mtoto mwenye mwaka mmoja unusu.
Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, alinaswa kwa kamera ya siri akionekana akimchapa na kumkanyaga mtoto huyo pamoja na kumzaba kofi.
Mnamo siku ya Ijumaa, Jolly alikiri kumshambuilia mtoto akisema alikuwa analipiza kisasi kwani mamake mtoto huyo naye alikuwa amezoea kumchapa.
Hata hivyo mama huyo alikanusha madai ya Jolly ambaye polisi walikuwa wamesema wangemshitaki kwa kosa la jaribio la mauaji ila kiongozi wa mashitaka akasisitiza kuwa ingekuwa vigumu kuthibitisha hilo.
Hakimu mkuu Lillian Buchan aliambia Tumuhirwe kwamba alitenda uhalifu ambao hauna hata kisingizio.
Alisema adhabu aliyompa inamtosha kulingana na makosa yake kwa kumtesa mtoto ambaye hana hatia.
Babake mtoto huyo, Eric Kamanzi alisema aliweka kamera ya siri nyumbani kwake baada ya kuwa na shauku kumhusu mfanyakazi huyo.
Kanda ya video iliyomuonyesha Jolly akimtendea unyama mtoto, ilitoka kwenye kamera ambayo Bwana Kimanzi aliweka nyumbani kwake baada ya kushuku kuwa mtoto wake alikuwa anatendewa unyama na pia baada ya kumapata mtoto wake akiwa na alama za majeruhi mwilini mwake.
Alimshitaki mwanamke huyo kwa polisi na kisha kuisambaza kanda hio kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu kutolewa,Kamanzi alisema: "sio juu yetu kuamua adhabu anayofaa kupewa Jolly. ''
"tunatumai kuwa hili ni funzo kwa wafanyakazi wengi wa nyumbani kwamba huwezi tu kwenda kwa nyumba ya mtu na kumtesa mtoto na kutarajia kuondoka tu kama ulivyoingia. ''

Wachezaji wa ti mu ya Zambia wapata ajali mbaya


  •  
Maafisa wakuu wa klabu hio wanasema hali ya wachezaji waliojeruhiwa imeweza kuimarika
Wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia waliohusika katika ajali ya barabarani Jumapili, wanasemekana kuwa katika hali nzuri.
Wachezaji hao Nyambe Mulenga, ambaye huchezea klabu ya Zesco United, Changwe Kalale wa Power Dynamos na Satchmo Chakawa kutoka Green Eagles walikuwa wanakwenda mjini Lusaka kwa basi ndogo la klabu ya Zesco United.
Basi hilo liligongana ana kwa ana na gari lengine katika eneo la Kabwe.
Shirikisho la soka nchini humo lilisema watu kadhaa walijeruhiwa na kwamba Mulenga alivunjika mguu.
Duru katika eneo hilo zilisema kuwa dereva wa basi la Zesco alifariki katika eneo la ajali huku watu wangine watatu waliokuwa kwa gari la pili pia wakifariki.
Klabu hio imetoa taarifa kuhusu hali ya wachezaji waliohusika na ajali hio pamoja na maafisa wengine wa klabu waliokuwa ndani ya basi hio.
Mhasibu wa klabu hio, Lomuthunzi Mbeba, afisa wa mauzo Fusya Bowa, afisa Frank Chitambala na mwanchama wa kamati Peter Mutale pia walijeruhiwa ingawa wanasemekana kua katika hali nzuri.
Kalusha Bwalya, Rais wa shirikisho la soka Zambia, alithibitisha kuwa maafisa waliojeruhiwa walifikishwa hospitalini na kwamba hali zao zimeimarika.
Wachezaji walikua wanasafiri kuelekea mjini Lusaka kwa maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya afrika 2015. Michuano hio inaanza tarehe 17 Januari nchini Equatorial Guinea.
Zambia itacheza katika kundi B pamoja na DR Congo, Cape Verde na Tunisia.

Manchester United wanataka kumsajili winga Gareth Bale toka klabu ya Real Madrid

Manchester United wanataka kuendelea kuimarisha kikosi chao kwa kumsajili winga Gareth Bale, mwenye miaka 25, toka klabu ya Real Madrid kwa dau la £90milion, pesa za mauzo ya Bale zitatumika kuwasajili nyota Eden Hazard wa Chelsea na kinda wa Liverpool Raheem Sterling.
Kocha wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier, ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa michezo wa timu ya New York Red Bulls yuko tayari kumpa ofa kiungo Steven Gerrard kujiunga na miamba hao wa ligi ya Marekani.
Manchester City imeingia katika vita na timu ya Manchester United katika mbio za kuwania saini ya mlinzi kisiki Mats Hummels, wa klabu ya Borussia Dortmund,Man City wako tayari kutoa kitita cha £47milioni ili kumtwaa mchezaji huyo.
Klabu yaTottenham wanafanya jitihada za kumsajili mshambuliaji Eran Zehavi, toka timu ya Maccabi Tel-Aviv inaaminika mchezaji huyo anapatika kwa kwa dau la £1.6milioni. Tottenham wanataka kuondoa tatizo la safu ya ushambuliaji inayoshindwa kufanya vizuri msimu huu.
Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amewataka Reds na meneja Brendan Rodgers kutoa £ 20milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Wilfried Bony mwenye 26, toka Swansea katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Inter Milan wanapigana vikumbo na Ajax pamoja naReal Sociedad kuwania kupata nafasi ya kumchukua kwa mkopo winga kinda Adnan Januzaj. Manchester United wako tayari kumuachia winga huyo mwenye miaka19, akapate uzoefu Zaidi baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Cristiano Ronaldo atwaa tuzo ya BBC.

 

Cristiano Ronaldo na kidole cha ushindi
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo nyingine baada ya kutangazwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka na shirika la utangazaji la BBC.
Ronaldo alishindwa kuhudhuria sherehe za utoaji tuzo hizo zilizofanyika Glasgow Scotland.kwasababu yuko Morocco na klabu yake ya Real Madrid.
Ronaldo anasema, "Nawashukuru BBC, na mashabiki wangu wa zamani wa Uingereza kwa kunichagua mimi,asanteni sana” Ronaldo amefunga magoli 281 kwenye mechi 267 alizochezea Real Madrid.
Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo akiwashinda mcheza tenesi Serena Williams, bondia Floyd Mayweather na Marc Marquez.

Watu kadhaa wanashikiliwa mateka Sydney

  •  
Baadhi ya waliookolewa kutoka ndani ya mgahawa wa Lindt
Watu kadhaa wanashikiliwa mateka na mtu mmoja au zaidi wenye silaha katika mgahawa wa Lindt mjini Sydney, Australia.
Mamia ya Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira eneo lilipotokea tukio hilo.
Takriban watu watatu wameonekana ndani ya mgahawa wakiwa wamenyanyua mikono juu wakiwa wameiegesha kwenye dirisha wakiwa wameshika bendera nyeusi ikiwa na maandishi ya kiarabu.
Mmoja wa waliokuwa ndani ya mgahawa ambao uliovamiwa na watekaji nyara mjini Sydney
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot amesema tuki hilo linahuzunisha sana.
Abbot amesema haijajulikana nani alihusika na tukio hilo hata hivyo anahisi huenda ni njama za kisiasa na kuwa tayarikamati ya usalama ya taifa imepewa taarifa.
Kamishna wa Polisi wa South Wales Andrew Scipione amesema tukio hilo halichukuliwi kuwa la kigaidi lakini imethibitishwa kuwa kuna mtu mwenye silaha anayewashikilia mateka watu kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo wamesema walimuona mtu akiwa na begi na silaha akiingia kwenye mgahawa, polisi wamefunga eneo hilo, barabara na kuwaondoa watu katika eneo hilo.

Zaidi ya watu 129 wazama Ziwa Tanganyika DR Congo


Maboti katika eneo hilo mara nyingi hujazaa abiria na mizigo kupita kiasi na ajali kutokea ni jambo la kawaida

Miili ya watu 129 imepatikana katika Ziwa Tanganyika baada ya boti kuzama Ijumaa

Miili ya watu wapatao 129 imepatikana kutoka Ziwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya feri kupinduka na kuzama mapema Ijumaa.
Waziri wa Uchukuzi nchini humo Laurent Sumba Kahozi amesema msako unaendelea kuwatafuta watu waliopotea katika ajali hiyo.
Wafanyakazi wa uokoaji waliwapata abiria wakielea katika maji Jumapili, wakiwa katika mapipa ya petroli na vifaa vingine.
Habari zinasema ajali kama hiyo ni za kawaida katika eneo hilo kutokana na boti kujaa abiria na mzigo kupita kiasi.
Maboya ya kujiokoa mara nyingi hayamo katika maboti hayo na watu wengi hawawezi kuogelea.
Maafisa katika jimbo la Katanga wamesema upepo mkali na kujaza abiria na mizigo kupita kiasi kumesababisha boti MV Mutambala, kupinduka.
Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu waliokumbwa na ajali hiyo ambayo ilitokea mapema Ijumaa asubuhi.
Taarifa za awali zilisema watu 26 wamekufa katika ajali hiyo.
Idadi ya watu walionusurika imetajwa kuwa watu 232, wengi wakiwa ni wanaume, amesema waziri wa uchukuzi katika eneo hilo