Thursday 4 December 2014

BETREAM MWOMBEKI ATUA RUVU SHOOTING

MSHAMBULIAJI huru Betram Mwombeki amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumia klabu ya Ruvu Shootings ya Pwani inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara.
Nyota huyo wa zamani wa Simba ameanza mazoezi na kikosi cha Shootings kinachonolewa na kocha Mkenya, Tomy Alex Olaba.
Mazoezi hayo yanafanyika katika kambi iliyopo Mabatini Mlandizi mkaoni Pwani.
IMG_1011
Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire amethibitisha taarifa hiyo jioni ya leo na amesema bado kocha Olaba yupo katika mawindo ya kuongeza nyota wengine.
Bwire amesema kwa sasa hawawezi kutaja wachezaji wanaotakiwa na kocha huyo aliyewahi kuifundisha kwa Mtibwa Sugar ya Morogoro.

0 comments: