Thursday 4 December 2014

KOLO HABIB TOURE, AMETANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Mlinzi wa timu ya taifa ya Ivory Coast Kolo Habib Toure, ametangaza kustaafu soka la kimataifa. Mara baada ya kumalizika kwa Michuano ya Kombe la Mataifa huru barani Afrika mwakani
Nyota huyo mwenye miaka 33- anayecheza klabu ya Liverpool ya Uingereza ameitumikia timu yake ya taifa mara 109.
Alikuwa mmoja wa wachezaji walikuwa kwenye kikosi kilichofuzu kucheza Michezo ya Kombe la Mataifa huru mwaka 2015 inayotarajiwa kufanyika kuanzia17 Januari mpaka 8 Februari huko Equatorial Guinea.
“Nina mpango kuwa hii ni Michezo yangu ya mwisho ya kimataifa nataka kujitolea kwa Taifa langu na tumetafuta medali kwa muda mrefu”.
kolo
“Kama kocha wangu (Herve Renard) atanipa nafasi ya kucheza katika michuano ijayo ya Afrika nitacheza kwa kadri ya uwezo wangu na kisha nitaaga kwa kustaafu Soka la kimataifa”.
Huu ndio utakua mwisho wa kolo na Tembo hao wa Afrika
Toure alikua ni sehemu ya kikosi cha ivory coast kilichocheza Kombe la Dunia alicheza mchezo mmoja wa makundi dhidi ya Ugiriki.
Kolo bado anahangaika kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Liverpool mpaka sasa amecheza michezo sita katika michuano

0 comments: