Tuesday 2 December 2014

YAYA TOURE NA ASAMOAH GYAN KWENYE KINYANGANYIRO CHA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA


SHIRIKISHO la Soka Afrika leo limetoa orodha fupi ya wachezaji watano walioingia katika fainali ya kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa mwaka 2014.
Taaria ya CAF iliyoifikia BIN ZUBEIRY imetoa orodha fupi mbili za wawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa ujumla na Mchezaji Bora wa Afrika anayecheza hapa barani.
Wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa ujumla ni Ahmed Musa wa Nigeria na klabu ya CSKA Moscow, Asamoah Gyan wa Ghana na Al Ain, Pierre – Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund, Vincent Enyeama wa Nigeria na Lille na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, ambaye ndiye anashikilia tuzo hiyo kwa sasa.
 
Kwa upande wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika anayexheza hapa barani walioingia ni Akram Djahnit, El Hedi Belamieri wote wa Algeria na E.S. Setif, Fakhreddine Ben Youssef wa Tunisia na C.S. Sfaxien, Firmin Mubele Ndombe wa DRC na AS Vita na Senzo Robert Meyiwa (marehemu) aliyekuwa akichezea Afrika Kusini na Orlando Pirates.

0 comments: