MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday 29 August 2014

HOT NEWS WATU ZAIDI YA KUMI WAFARIKI KATIKA AJALI MBALIZI MBEYA








Habari kamili  endelea kutufuatilia

MCHUNGAJI KOTINI KWA KOSA LA KUISHI NA MKE WA MTU



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, ambapo wananchi wengi wanaamini Mchungaji ni sehemu ya kukimbilia kueleza matatizo yao hususani migogoro ya kindoa, hali imekuwa tofauti jijini Mbeya.

Utata umeibuka baada ya Mchungaji, Israel Mwakifuna, wa Kanisa la Jeshi la Bwana(JB)lililopo Nzovwe jijini Mbeya amefikishwa katika Mahakama ya mwanzo ya Iyunga jijini Mbeya akituhumiwa  kuishi na mke wa mtu ambaye ni muumini wake.

Mchungaji huyo alifikishwa juzi mbele ya ×Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Iyunga, Nuru Lyimo akisaidiwa na ×Washauri wa mahakama ×Edson Mbeba na Rehema Haonga.
Kesi hiyo ya madai namba 51/2014 imepelekwa mahakamani hapo na  William Daimon Mwasubila(23)mkazi wa Nzovwe ambapo imedaiwa mahakamani Mchungaji kuishi na mke wake aitwaye Helena Mkea(21) kwa muda wa miezi minne sasa.
Mlalamikaji katika ×Kesi hiyo, Mwasubila aliiambia mahakama kuwa alikuwa akiishi na mkewe bila tatizo lakini matatizo yalianza pindi mkewe aliposhika ujauzito na kuamua kwenda kwa wakwe zake kwa matazamio baada ya mapishano yaliyodhaniwa kusababishwa na ujauzito hali ambayo alikubali.
Mwasubila alieendelea kuiambia mahakama kuwa mkewe alimuoa kihalali kupitia mshenga wake aliyefahamika kwa jina la ×Edward Mwangoje ambapo walifuata taratibu zote za mila kwa kulipa kiingilio cha mlangoni 50,000,kufungua 20,000,adhabu 50,000, kuku wawili, mashuka, mablanketi mawili na majembe mawili.

Alivitaja vitu vingine alivyolipia kama mahali kuwa ni mkaja wa mama 150,000 ambapo alilipa elfu hamsini,×Mbuzi wawili jike na dume,n'gombe watatu dume ambao kila mmoja akiwa na thamani ya shilingi 300,000 na kupokelewa na wazazi kupitia kwa mshenga Octoba 20 mwaka 2013 eneo la Airport Jijini Mbeya.

Alisema mgogoro katika ndoa yao ulianza baada ya ×Mume kuzikuta SMS za mapenzi kwenye simu ya mkewe kwenda kwa mchungaji ×Mwakifuna ambapo alitoa taarifa kwa wazazi wapande zote mbili ambapo walijadili na kuondoa tofauti hizo na kuamua kuwasamehe.

Aliongeza kuwa  muda mfupi baada ya mazungumzo Mchungaji aliendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muumini wake hali iliyosababisha mke wa mchungaji Mwakifuna kuondoka kwa mumewe miezi minne iliyopita baada ya yeye(Mlalamikaji) kwenda kikazi Sumbawanga Mkoani Rukwa ambapo mkewe alihamia kwa Mchungaji wake na kuanza kuishi kama mke na mume.

Aliendelea kuiambia Mahakama kuwa Baada ya kutoka Sumabwanga  alipata taarifa kuwa mkewe anaishi na mchungaji ambapo aliamua kutoa taarifa Polisi kituo cha Nzovwe.

Alisema Jeshi la Polisi lilifika nyumbani kwa Mchungaji na Kumkuta  mkewe akiwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa wiki moja na nusu ndipo alipokamatwa  Agosti 25 na kufikishwa mahakamani Agosti 26, mwaka huu.

Baada ya kusikiliza shahidi mmoja wa upande wa mlalamikaji Hakimu Lyimo aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu mlalamikaji atakapoleta mashahidi wengine kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

MAANDAMANO YA WANAWAKE KUPINGA MAUAJI YAYEYUKA

 Wanawake waliotaka kuandamana mkoani Arusha mandamano  yao ya yayeyuka katika mazingira ya kutatanisha,maandamano  yaliyopangwa kufanyika jana kupinga mauaji waliyodai kuwa ya wanawake wanaoendesha magari pekee yameyeyuka kutokana na kutojua nani anayeratibu na ushahidi wa wanawake wanaodaiwa kuuawa yaliokuwa yafanyike jijini hapa.
Mauaji hayo yanaelezwa kutekelezwa na watu wanaotumia usafiri wa bodaboda kwa kumfuata mwanamke anayeendesha gari na kisha kumsimamisha na pindi anapofungua kioo cha gari wanamfyetulia risasi pasipo kupora kitu chochote.
Maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kuanzia majira ya saa nne asubuhi kwa wanawake hao kukutana katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha pia yalikosa nguvu kutokana na kutoelezwa mahali pa kuanzia wala saa ya kukutana.
Taarifa za kuwataka wanawake hao kuandamana zilitolewa kwa njia ya mtandao wa kijamii ambao ulisambaa katika simu za mikononi uliokuwa ukihamasisha kila mwanamke na wasichana jijini Arusha kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo kama hatua ya kupinga mauaji hayo waliyodai kuwahusu wanawake wanaoendesha magari.
Kuhusu wanawake hao kukosekana kwa ushahidi wa mauaji hayo kunatokana na maswali yaliyoulizwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas kwamba wanawake waliouawa ni wapi kutokana na taarifa za kuwepo kwa wanawake sita waliouawa katika matukio hayo.
Kamanda Sabas hapo juzi alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa hizo za uzushi alisema ni mwanamke mmoja tu Shamimu Yulu ndiye aliyeuawa kwa kupiwa risasi maeneo ya Sakina Kwa Idd mnamo mwezi huu tena katika tukio la uporaji wa kawaida kwa kutumia silaha na siyo kama inavyoelezwa kuwa lengo ni kuua wanawake wanaoendesha magari.
Kamanda Sabas alitaja tukio lingine la mauaji ya kutumia silaha yaliyotokea kipindi hichi kuwa ni lile lililohusisha kifo cha mtoto wa miaka mitatu maeneo ya Olasiti baada ya watu waliokuwa na bodaboda kumsimamisha baba aliyekuwa akiendesha gari na kisha kukataa na ndipo walipofyetua risasi iliyompata mtoto huyo na kisha kupora shilingi 2000.
Mapema leo asubuhi wanawake wachache walionekana wakiwa katika vikundi vikundi katika maeneo ya hoteli ya Goldenrose,Bwalo la maafisa wa polisi jijini hapa na wengine wakiwa wamejificha katika magari yao maeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa wakiangalia iwapo kuna wenzao waliojitokeza.
Hata hivyo polisi wa FFU walionekana katika baadhi ya maeneo ya mji wakipitapita kuona iwapo kutakuwa na maandamano hayo ambayo hata hivyo jeshi la polisi liliyazuia kwakua hayakuwa na ukweli wowote wala kibali.
Hata hivyo jana mkuu wa mkoa wa Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari aliwata wanawake mkoani Arusha kusitisha maandamano hayo kwakua vyombo vya ulinzi na usalama vimeingia kazini na mapema 
Kamanda Sabas akizungumzia matukio hayo alisema tayari watuhumiwa saba wameshakamatwa na wawili kati ya wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo wakati wengine watano wakiendelea kuhojiwa na msako mkali dhidi ya wengine waliobaki ukiendelea.
 
 NA MAHMOUD AHMAD,ARUSHA.
 

SHAHIDI AELEZEA JINSI ALIVYOFANYISHWA MAPENZI NA MGANGA WA JADI

mganga





 
Mwanahamisi Omary (26) alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma kuwa alimfahamu mganga huyo baada ya kusumbuliwa na tumbo la uzazi kwa muda mrefu.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Felista Mosha, Mwanahamisi alidai alikuwa akitibiwa ugonjwa huo bila ya kutoa taarifa kwa mumewe Edrick Elinezer. Alidai alitibiwa kwa miezi sita bila ya mafanikio.
 
Shahidi huyo alidai Aprili, mwaka huu, Michael alimwambia kuwa ana majini hivyo hawezi kupata mtoto na kumpatia dawa kwa ajili ya kunywa na kuoga.
 
Alidai mganga huyo alikuwa akimtibu nyumbani kwake lakini baadaye alihamishia ofisi yake katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Kigogo Luhanga na kudai kuwa mganga huyo alikuwa akipaka dawa katika uume wake na kumuingilia kimwili huku akiwa hajitambui kwa madai kwamba atamsaidia kupata mtoto.
 
Aliendelea kudai kwamba baada ya kutokuwa na mawasiliano kwa muda mrefu na mumewe, alipata taarifa kuwa mume wake alipigiwa simu na mganga huyo na kumtaka apeleke gari lake Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 139 BSG maeneo ya Jangwani kwa kuwa majini ya mkewe yanataka mtoto.
 
Awali, Hakimu Juma alisema wadhamini wa mshitakiwa wanatakiwa kumtafuta mshitakiwa huyo na kumfikisha Mahakamani hapo, aliwatahadharisha wasipofanya hivyo kwa wakati watalipa faini ya Sh milioni sita kwa kila mmoja.
 
Michael alidaiwa Aprili 29, mwaka jana, maeneo ya Jangwani Wilaya ya Ilala, alijipatia gari aina ya Toyota Rav4 T 139 BSG lenye thamani ya Sh milioni 12 mali ya  Eliezer kwa njia ya udanganyifu. Kesi hiyo itasikilizwa  tena Septemba 18, mwaka huu.

NYOTA YA ROONEY YAZIDI KUNG'ARA, AWA NAHODHA WA TIMU YAKE YA TAIFA YA UINGEREZA.

 

Mshambuliajiwa Manchester utd na timu ya taifaya Uingereza, Wayne Rooney ametangazwa rasmi kuwa nahodha wa timu ya taifaya Uingereza kuchukua mikoba iliyo wachwa na Steven Gerrard aliye staafu kuchezea timu hiyo yataifa Julai mwaka huu mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Wayne Rooney has been given the England armband
Wayne Mark Rooney.

Rooney mwenye umri wa miaka 28 alitangazwa pia kuwa nahodha wa klabu yake ya Manchester utd mapema mwezi huu, amefanikiwa kuichezea timu yake ya taifa ya England mechi 95 huku akiifungia magoli 40. Uteuzi huo metangazwa na meneja wa timu hiyo Roy Hodgoson.

England inajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Norway September 3 mwaka huu katika uwanja waWembley kablaya mechiya kufuzu kwa michuano ya mataifa ya ulaya dhidi ya Switzerland September 8 mwakahuu, michuano hiyo ya Ulaya yatafanyika mwaka 2016.

MKURUGENZI WA ZAMANI WA TANZANIA (TBS), ATUPWA JELA MWAKA MMOJA

 Charles Ekelege akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo ambapo alihukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kulipa faini ya sh.milioni 68.
 Hapa Ekelege akiwa amekaa nje ya Mahakama hiyo na familia yake  kabla ya kuhukumiwa. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Ekelege akiteta jambo na familia yake akiwa Mahakamani hapo.
 Askari polisi akiwa na familia ya Ekelege (wa pili kulia), wakati akitoka kwenye mahakama hiyo.
Ekelege akiteta jambo na kijana aliyedaiwa kuwa ni mtoto wake.

KIFAA CHA KUCHUNGUZIA UGONJWA WA EBOLA CHAWEKWA AIR PORT ZANZIBAR

Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni akionesha Kifaa “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine. ??????????????????????????????? 
Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Zanzibar wakionesha baadhi ya Vifaa Vitalavyotumika kuwachunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine ??????????????????????????????? 
Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni akionesha matumizi ya Kifaa cha “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.

Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha THERMAL SCANNER kwa ajili ya kuchunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
Kifaa hicho kilichowekwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kitatumika kwa ajili ya kuwachunguza zaidi Wageni ambao watatoka katika nchi zilizoathiriwa na Ugonjwa wa Ebola.
Akikabidhi kifaa hicho Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni amesema THEMO SKAN kitasaidia katika kuwabaini watu ambao wameathirika au kuwa na dalili za Ungojwa wa Ebola na kuchukuliwa hatua zaidi.
Dkt Salma amesema iwapo mgonjwa atabainika hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Chumbuni ambacho kimetayarishwa kwa ajili hiyo.
Aidha Dkt Salma amefahamisha kuwa Kituo cha Afya cha Chumbuni kimetengwa kama eneo litakalotumika kwa ajili ya Matibabu kwa mgonjwa atakayebainika kuambukizwa Ugonjwa wa Ebola nchini.
Amesema Wizara ya Afya katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa kuambukiza imekuwa ikifanya Jitihada mbalimbali za kutoa elimu na njia mbali mbali za kinga kabla ya Zanzibar kuathirika na Ebola.
Amesema licha ya Vifaa hivyo vilivyotolewa Vifaa vingine vitakuja wiki inayokuja ili viendelee kutumika katika maeneo ya Bandarini na Viwanja vya ndege Unguja na Pemba
Dkt. Salma amesema Ugonjwa huo haujaingia nchini bali Serikali inajiandaa na juhudi zake za kukabiliana na Ugonjwa huo ili usiweze kuingia na kuathiri Zanzibar.


Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar  28/08/2014

Viongozi, wanaharakati wataka Katiba Mpya Imtambue mtoto na haki zake

Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe.

MCHAKATO wa kujadili na kuandika Katiba Mpya unaendelea bungeni mjini Dodoma, licha ya kuwepo kwa mvutano na mgawanyiko wa makundi ya wabunge wa bunge maalumu wanaojadili Rasimu ya Pili iliyowasilishwa kwao. Wakati hayo yakiendelea viongozi, wanaharakati na wadau wa watoto wanapendekeza masuala ya haki za msingi za watoto yatambulike vizuri katika katiba ijayo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe anashauri ibara ya 43 ambayo inataja haki za msingi za watoto iendelee kuwepo mpaka Katiba inakamilika na iboreshwe zaidi katika mchakato unaoendelea Bungeni. Nasema haya maana tayari kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji kwamba kwanini hata watoto wanaingia kwenye katiba ilhali wao ni sehemu ya watu kama wazazi wao.
Anasema pamoja na kuingizwa kipengele cha mtoto kwenye rasimu ya pili ya katiba bado kuna mambo ambayo wao kama wadau wangependa yaingizwe tena hivi sasa katika mchakato wa majadiliano unaoendelea. Anasema baadhi ya mambo hayo ni kama umri wa mtoto mwenyewe kutaja wazi kwamba ni kuanzia umri gani.
“…Unaweza ukaangalia hili ni suala la msingi sana kutaja umri wa mtoto mwenyewe anayezungumziwa…kwa sisi wadau wa watoto tunashangaa sana kwa maana nyingine tunaona suala hilo ni kama linaongeza utata, kumuweka mtoto kwenye katiba ilhali umeshindwa kumtambua (kiumri) mtoto ni yupi ni sawa na vichekesho…tunashauri mtoto huyu umri utajwe wazi kuondoa utata…,” anasema.
Mfano ukisema wazee wana haki ya kutibiwa bure lazima useme huyu mzee anaanzia umri gani na kuishia wapi. Huwezi kusema wazee watibiwe bure alafu unashindwa kuainisha vitu vya muhimu kama umri wao, bila hivyo utaleta mkanganyiko wa tafsiri…ndiyo maana hata sasa mtoto anayetajwa tunataka tujue anaanzia umri gani na kuishia umri gani. Sasa hili pekee linatushangaza watu wasomi wanajadili bila kuliona hili.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na mwandishi wa makala haya.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na mwandishi wa makala haya.

Huyu mtoto akiingia kwenye mgongano katika sheria anashughulikiwa namna gani kwasababu hili linaweza kuwa na mgongano kama pia litashindwa kutajwa kwenye katiba chombo ambacho ni sheria mama ya nchi. Masawe anasema mambo mengine ambayo yanatakiwa kuainishwa ni pamoja na kuelekeza namna ya kuwawajibisha wazazi ambao wamekuwa wakikimbia majukumu yao ya kulea watoto na kuwapeleka katika vituo vya yatima eti kwa madai wamewashinda.

WAZIRI MKUU ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI IRELAND

index 
* Asaini kitabu cha maombolezo ya Waziri Mkuu wa zamani
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametumua salamu za rambirambi kwa Serikali ya Ireland kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Bw. Albert Reynolds.
Hayati Reynolds ambaye amefariki akiwa na miaka 81, alikuwa Waziri Mkuu wa nane wa nchi hiyo kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1992. Atakumbukwa kwa kuanzisha mchakato wa kuleta amani Ireland Kaskazini dhidi ya kundi la IRA.
Waziri Mkuu Pinda ambaye aliwasili jana (Alhamisi, Agosti 28, 2014) jijini Dar es Salaam akitokea Dodoma, alikwenda moja kwa moja ubalozi wa Ireland na kusaini kitabu cha maombolezo cha kiongozi huyo.
Katika salamu za rambirambi, Waziri Mkuu amemwelezea Bw. Reynolds kuwa ni kiongozi atakayekumbukwa kwa kuleta amani duniani na misaada ya kimaendeleo nchini Tanzania.
“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, ninawapa pole sana kwa kufiwa na Kaka yetu na ndugu yetu, Waziri Mkuu wa zamani wa Ireland, Albert Reynolds. Tunashirikiana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Tutaendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri alizofanya kwa nchi yetu na duniani. POLENI SANA KWA MSIBA HUU MKUBWA,” inasomeka sehemu ya salamu za rambirambi alizotoa Waziri Mkuu.
Akipokea salamu hizo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bibi Fionnuala Gilsenan alimshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa kufika ubalozini hapo na kuwapa pole kwa kifo cha Waziri Mkuu wao wa zamani.
“Tutamkumbuka kiongozi wetu kwa mambo mengi aliyoifanyia nchi yetu… Tunafarijika kwa salamu hizi za rambirambi. Tutafikisha kitabu hiki cha salamu za rambirambi kwa familia yake, naamini nao watafarijika sana,” alisema Balozi Gilsenan.
Balozi Gilsenan alimweleza Waziri Mkuu kwamba kitabu cha maombolezo kitafungwa leo.

Matukio katika picha Bunge Maalum la Katiba leo 29 Agosti, 2014 Mjini Dodoma

PIX 1. 
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
PIX 2.Mwakilishi wa Watanzania waishio Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Kadari Singo (kushoto) akifurahia jambo akiwa pamoja na waandishi wa Habari leo 29 Agosti, 2014 Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma
PIX 3.Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kulia ni Mhe. Stella Manyanya akiwa amefuatana na Mhe. Reuben Matango wakielekea ndani ya Bunge Singo leo 29 Agosti, 2014 Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma
PIX 4.Mwakilishi wa Watanzania waishio Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Kadari Singo (kushoto) akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzie, Mhe. Yusuph Singo leo 29 Agosti, 2014 Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.

ANGLIA RONALDO ALIVYOSHEREHEKEA TUZO YA MWANASOK BORA WA ULAYA



Busu kwenye tuzo: Nyota wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akibusu tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kukabidhiwa usiku wa leo mjini Monaco, Ufaransa
Cristiano Ronaldo akifurahia na tuzo yake
Ronaldo (katikati) akifurahia baada ya kushinda. kushoto ni wachezaji wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi Arjen Robbe kulia

XABI ALONSO AKAMILISHA UHAMISHO WAKE BAYERN MUNICH


KIUNGO Xabi Alonso amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 5 kutua Bayern Munich akitokea Real Madrid.
Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool, alikuwa akihusishwa na mango wa kuhamia Manchester United baada ya miaka mitano ya kupiga kazi Bernabeu, lakini sasa anakwenda kuungana na Mspanyola mwenzake, kocha Pep Guardiola.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 anakwenda kwa mabingwa hao wa Ujerumani katika wakati ambao wanakabiliwa na majeruhi wengi, wakiwemo Javi Martinez, Bastian Schweinsteiger na Thiago Alcantara. 
Salamu Munich: Xabi Alonso amejiunga na Bayern Munich akitokea Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 5Touch down: Former Liverpool man Alonso arrived in Munich ahead of his medical
Anamwaga wino: Nyota wa zamani wa Liverpool, Alonso akiwasaini mashabiki mjini Munich wakati anakwenda kufanyiwa vipimo vya afya

Thursday 28 August 2014

LIGI YA MABINGWA, MAKUND I YAWEKWA HADHARANI ANGALIA HAPA

 


MABINGWA wa England, Manchester City wamepangwa kundi moja na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na CSKA Moscow na Roma, wakati Liverpool wao wamepangwa na mabingwa watetezi, Real Madrid.
Mabingwa mara tano Ulaya, Liverpool mbali na kupangwa na mabingwa mara 10 wa taji hilo, Real pia wapo na Basle na Ludogorets.
Arsenal, imepangwa na Borussia Dortmund pamoja na Galatasaray na Anderlecht katika Kundi D, wakati Chelsea imepangwa na imepangwa na wakali wengine wa Ujerumani, Schalke, Sporting Lisbon na Maribor.

KUNDI A 

Atletico Madrid 
Juventus 
Olympiakos 
Malmo 

KUNDI B 

Real Madrid 
Basle 
LIVERPOOL
Ludogorets 

KUNDI C 

Benfica 
Zenit St Petersburg 
Bayer Leverkusen 
Monaco 

KUNDI D 

ARSENAL
Borussia Dortmund 
Galatasaray 
Anderlecht 

KUNDI E 

Bayern Munich
MANCHESTER CITY
CSKA Moscow 
Roma 

KUNDI F 

Barcelona 
Paris St-Germain 
Ajax 
Apoel Nicosia 

KUNDI G 

CHELSEA
Schalke 
Sporting Lisbon 
Maribor 

KUNDI H 

Porto 
Shakhtar Donetsk 
Athletic Bilbao 
Bate Borisov 
Mkali wao: Cristiano Ronaldo akiwasili kwenye drop ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo mjini Monaco, Ufaransa

OKWI AREJEA SIMBA SC ILA KESI YAKE NA YANGA IKOPALE PALE

STAILI ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inaitumia kumrejesha kundini Mganda huyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam, Okwi amesema kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.

Msimbazi ni nyumbani; Okwi akiwa na jezi ya Simba SC baada ya kurejea timu yake ya zamani leo

“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.  
Yanga mtanikoma; Okwi akiwa ameshika jezi yake nbamba 25 kwa pamoja na Hans Poppe

Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni.
“Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.
Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia.
Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.
Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.
Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.
Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo.
Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.
Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.
Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.

RONALDO APEWA TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA


MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya msimu wa 2013-2014 katika sherehe zilizofanyika jioni ya leo mjini Monaco, Ufaransa. Nyota huyo wa Real Madrid amewapiku nyota wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi, Arjen Robben alioingia nao fainali.


Wakati Neuer alishinda taji la Bundesliga na Kombe la Dunia msimu uliopita, Robben alifunga mabao 22 kwa klabu na timu yake ya taifa msimu uliopita na Ronaldo alifunga mabao 56 na kutoa pasi 15 za mabao Real Madrid na Ureno. Mshindi wa mwaka jana, Mfaransa Franck Ribery hakuingia fainali. Ronaldo pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia na ushindi huu ni pigo lingine kwa mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina na Barcelona.

Balozi wa Guinea ampiga vibaya na kumjeruhi mwanawe

 
Polisi wa jiji la Washington

Polisi nchini Marekani wameshindwa kumkamata balozi wa Equatorial Guine mjini Washngton, kwa tuhuma za kumpiga binti yake kwa mguu wa kiti cha mbao, balozi huyo hajakamatwa mpaka sasa kutokana na kinga yake ya kibalozi alonayo .
Msemaji wa polisi Dustin Sternbeck amesema kwamba walipewa taarifa mapema wiki hii kua kuna tukio nyumbani kwa balozi huyo, na walipofika wakamkuta binti huyo mdogo akiwa na jeraha kubwa kichwani mwake ambaye alihitaji tiba na hivyo kumpeleka hospitalini kwa matibabu.
Pamoja na hayo yote Dustin alisema kua polisi hawana mamlaka kwa kesi za namna hiyo zinazowahusisha wanadiplomasia lakini wamekwisha iarifu serikali juu ya suala hilo.

MECHI ZA TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUPIGWA TANGA, BUKOBA.


Mechi nyingine ya tiketi za elektroniki siku hiyo itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuzikutanisha timu za Kagera Sugar na Geita Gold SC ya mkoani Geita. Geita Gold iko Daraja la Kwanza Kabla ya mechi hizo, Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) saa 3 asubuhi kwenye viwanja hivyo kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki pamoja na jinsi mfumo huo unavyofanya kazi. Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa vituo vya Tanga na Bukoba, viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (KRFA) na Tanga (TRFA), makatibu na maofisa habari wa klabu za Kagera Sugar, Mgambo Shooting, African Sports na Geita Gold, mameneja wa viwanja vya Kaitaba na Mkwakwani na wasaidizi wao, maofisa usalama wa TRFA na KRFA, wachanaji tiketi, wasimamizi wa milangoni, wasaidizi (stewards) na waandishi wa habari.