Thursday 21 August 2014

Arsenal,Basiktas kuingia dimbani leo?



Kocha wa Arenal, Arsene Wenger
Beki wa kushoto wa Arsenal, Kieran Gibbs atakosa mechi zote za ligi ya mabingwa dhidi ya Besiktas baada ya kuumia eneo la uvungu wa goti.
Gibbs atakaa benchi kwa takriban majuma matatu baada ya kuumia wakati wa mchuano kati ya Arsenal na Crystal Palace siku ya jumamosi.
Pia mshambualiaji Yaya Sanogo hajasafiri kwenda uturuki kwa ajili ya mpambano wa leo
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema anatamani kupambana na timu zilizo juu zaidi barani ulaya.
Siku ya jumanne Arsenal itacheza mechi ya kwanza dhidi ya Basiktas nchini Uturuki.
Arsenal iliidhidbiti klabu nyingine ya Uturuki Fenerbahce katika hatua ya makundi msimu uliopita.

0 comments: