Sunday 10 August 2014

REAL MADRID YAMWAGA MAMILIONI KWA BIMA ZA NYOTA WAKE



JAMES
Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid wamemwaga mamilioni ya euro kwa ajili ya wachezaji wake wa wapya.
Kati ya waliokatiwa bima kubwa ni mshambuliaji mpya, James Rodríguez, kiungo kisheti, Toni Kroos na nyanda wa Costa Rica, Keylor Navas.
Bima hiyo kwa watatu hao ni kuwalinda iwapo watatokewa na majanga ya kuumia vibaya na kushindwa kuendelea kucheza au ulemavu.
Maana yake, Madrid imejiweka salama kwa vile haitalazimika kulipa fedha yoyote kama wachezaji hao wataingia matatizoni.
Kawaida ni 1% ya kile ilichotoa kwenye usajili, mfano euro milioni 80 zilizotolewa kwa Monaco kumsajili James, hivyo bima yake ni €80 million.
Wenye bima kubwa zaidi ni Cristian Ronaldo na Gareth Bale, ambao kila mmoja bima yake imefikia euro milioni moja.

0 comments: