Wednesday 27 August 2014

Burundi yazuru Tanzania kujifunza kuhusu madini na nishati

burundi 2 
Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi Mhe. Côme Manirakiza (aliyeinua mkono), akiomba kupewa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini hapa nchini, baada ya uwasilishwaji mada zilizohusu sekta za nishati na madini za Tanzania. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walitembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kwa lengo la kujifunza namna sekta husika zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania (kushoto) na Ujumbe ulioongozana na Waziri (Kulia).
burundi 4 
Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake (Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 – 28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.
Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.
Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

0 comments: