Friday 29 August 2014

MAANDAMANO YA WANAWAKE KUPINGA MAUAJI YAYEYUKA

 Wanawake waliotaka kuandamana mkoani Arusha mandamano  yao ya yayeyuka katika mazingira ya kutatanisha,maandamano  yaliyopangwa kufanyika jana kupinga mauaji waliyodai kuwa ya wanawake wanaoendesha magari pekee yameyeyuka kutokana na kutojua nani anayeratibu na ushahidi wa wanawake wanaodaiwa kuuawa yaliokuwa yafanyike jijini hapa.
Mauaji hayo yanaelezwa kutekelezwa na watu wanaotumia usafiri wa bodaboda kwa kumfuata mwanamke anayeendesha gari na kisha kumsimamisha na pindi anapofungua kioo cha gari wanamfyetulia risasi pasipo kupora kitu chochote.
Maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kuanzia majira ya saa nne asubuhi kwa wanawake hao kukutana katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha pia yalikosa nguvu kutokana na kutoelezwa mahali pa kuanzia wala saa ya kukutana.
Taarifa za kuwataka wanawake hao kuandamana zilitolewa kwa njia ya mtandao wa kijamii ambao ulisambaa katika simu za mikononi uliokuwa ukihamasisha kila mwanamke na wasichana jijini Arusha kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo kama hatua ya kupinga mauaji hayo waliyodai kuwahusu wanawake wanaoendesha magari.
Kuhusu wanawake hao kukosekana kwa ushahidi wa mauaji hayo kunatokana na maswali yaliyoulizwa na kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas kwamba wanawake waliouawa ni wapi kutokana na taarifa za kuwepo kwa wanawake sita waliouawa katika matukio hayo.
Kamanda Sabas hapo juzi alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa hizo za uzushi alisema ni mwanamke mmoja tu Shamimu Yulu ndiye aliyeuawa kwa kupiwa risasi maeneo ya Sakina Kwa Idd mnamo mwezi huu tena katika tukio la uporaji wa kawaida kwa kutumia silaha na siyo kama inavyoelezwa kuwa lengo ni kuua wanawake wanaoendesha magari.
Kamanda Sabas alitaja tukio lingine la mauaji ya kutumia silaha yaliyotokea kipindi hichi kuwa ni lile lililohusisha kifo cha mtoto wa miaka mitatu maeneo ya Olasiti baada ya watu waliokuwa na bodaboda kumsimamisha baba aliyekuwa akiendesha gari na kisha kukataa na ndipo walipofyetua risasi iliyompata mtoto huyo na kisha kupora shilingi 2000.
Mapema leo asubuhi wanawake wachache walionekana wakiwa katika vikundi vikundi katika maeneo ya hoteli ya Goldenrose,Bwalo la maafisa wa polisi jijini hapa na wengine wakiwa wamejificha katika magari yao maeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa wakiangalia iwapo kuna wenzao waliojitokeza.
Hata hivyo polisi wa FFU walionekana katika baadhi ya maeneo ya mji wakipitapita kuona iwapo kutakuwa na maandamano hayo ambayo hata hivyo jeshi la polisi liliyazuia kwakua hayakuwa na ukweli wowote wala kibali.
Hata hivyo jana mkuu wa mkoa wa Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari aliwata wanawake mkoani Arusha kusitisha maandamano hayo kwakua vyombo vya ulinzi na usalama vimeingia kazini na mapema 
Kamanda Sabas akizungumzia matukio hayo alisema tayari watuhumiwa saba wameshakamatwa na wawili kati ya wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo wakati wengine watano wakiendelea kuhojiwa na msako mkali dhidi ya wengine waliobaki ukiendelea.
 
 NA MAHMOUD AHMAD,ARUSHA.
 

0 comments: